KWANINI MBILIKIMO WENGI WANAFANANA?

KWANINI MBILIKIMO WENGI WANAFANANA?

pabro11

Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
60
Reaction score
104
Habari wakuu naomb kujuzwa kuhusu hili jambo kwa wenye ujuzi wa masuala haya ya genetics ....(lengo kujuzwa sio ubaguzi kama Kuna jina lingine sahihi zaidi nilipaswa nitumie mtanisamehe)

Kwanini hawa jamaa wanafanana sana hasa wa kiume ?
Nishapishana nao kama Sita hivi maeneo tofauti ajabu wanafanana fanana sana.......wajuzi
 
Exactly!
Sijui ni kwa nini tena siyo mbilikimo pekee bali kuna albino wengi wao wanafanana

Pia wasomali, wahabeshi, wachina, nk (kwa ujumla watu wote tofauti na watu weusi) nao wananichanganyaga sana kwa kufanana kwao
 
Onaa chief,

Mambo kama hayo ni ya kijenetiki. Hivyo unakuta labda wenye jeni hizo wote wana pua ya namna fulani. Kwa hiyo ukimuona huyu au yule utaona wanafanana kwa kuwa tu wameshea sifa fulani.

Ni sawa na useme watu wenye 'trisomy' wanafanana wote kutokana na namna wanavyoweka ulimi na midomo.

Si ushasikiaga kata pua uunge wajihi, ndo mambo kama hayo sasa. Kitu kidooooogo kikifanana basi utasema wote wanafanana.
 
Kwenye dwarfism head is not affected kichwa huwa kinaendelea kukua especially eneo la ubongo kwakuwa ana upungufu wa growth hormone lile eneo hutanuka ili kukidhi space ya ubongo ndio maana wengi wao wana vichogo na makomwe ..mbilikimo wachache sana wana vichwa vidogo.
 
Hata wenye autism wanafanana hata kama ni race tofauti, sijui kwanini!!!
 
Ni kama vile ukiwa China, Wachina wanavyotuona watu weusi wote tunafanana...


Cc: Mahondaw
 
Kwa sababu ya condition inayoitwa achondroplasia hii hutokea kwa aina ya kwanza ya dwarfism (Disproportionate dwarfism), ambayo ni hali ya kijenetiki inayosababisha ufupi wa miguu na mikono, kichwa kikubwa na uso kuwa na muonekano unaoendana...
 
Hawa wanaoana vipi?? Wenyewe Kwa wanyewe au wanachanganya? Kama wao Kwa wao gene za mfanano ndio zitaendelea kudominate.
 
Back
Top Bottom