Binafsi huwa nina huruma sana na viumbe. Huwa naona kabisa, maisha ya mwanadamu hayatofautiani sana na ya viumbe wengine. Tumepewa utashi, ila haimaanishi tunapaswa kufanya mambo pasipo kutumia weledi kwenye fikra zetu.
Yule ni mnyama, anahitaji chakula, maji n.k kama ambavyo sisi tunahitaji. Hao wa kuzurura mtaani muda mwingine unakuta ni mazingira tu. Hata ingekuwa ni watoto hawapati matunzo majumbani, lazima wataonekana watoto wa mtaani. Watazurura ili wapate mahitaji yao.
wanyama wana uhai pia, na wao hufa kama ambavyo binadamu anakufa. Si jambo zuri kuwatesa wanyama. Wana hisia za maumivu pia, japo hawezi kusema lakini utagundua tu