Kwanini Mchezaji akitoka Yanga kwenda Timu Nyingine Lazma Achemshe

Kwanini Mchezaji akitoka Yanga kwenda Timu Nyingine Lazma Achemshe

Je Yanga ni wachawi? Je huwa wanatoa laana kwa wachezaji wanaohama klabu yao?

Mifano iko wazi kama ifuatavyo...

Frank Domayo alitoka Yanga akiwa fomu sana akaenda Azam Fc. Kila mmoja ni shahidi juu ya kilichomkuta Domayo. Goti linamuuma mpaka kesho, na hajawahi kurudi katika ubora wake.

Mrisho Ngassa alipoihama Yanga na kwenda Azam Fc uwezo ukaisha hapohapo.

Dider Kavumbagu alipoondoka Azam Fc kutoka Yanga aliishia kuchemsha.

Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima "Fabregas" alipoihama Yanga kwa mbwembwe na kutua Simba, hakuna asiyejua kinachomsibu kiungo huyo fundi wa mpira, amekuwa mchezaji.wa kawaida sana.

Yanga punguzeni misumari, msiwabanie wachezaji, wenzenu wanatafuta maisha
VP Okwi
 
Amri Kiemba timu aliyochezea mda mrefu ni Simba.
Amri, alitoka Simba akaenda Yanga Akacheza mwaka mmoja, akarudi Simba.
Labda umepoteza kumbukumbu.

Alipotoka Yanga nakumbuka alikwenda kwanza huko Zanzibar, angalau hili nina uhakika nalo, alicheza huko Zanzibar ndipo akaenda tena Simba
 
Amri Kiemba timu aliyochezea mda mrefu ni Simba.
Amri, alitoka Simba akaenda Yanga Akacheza mwaka mmoja, akarudi Simba.
Labda umepoteza kumbukumbu.
Alianzia Yanga akashindwa akaenda kagera sugar msimu mmoja akaenda miembeni Zanzibar ndipo aliporejea Simba na kucheza misimu mitatu kwa mafanikio sana mpaka Rajer Casablanca wakataka kumsajili Simba wakagoma kumwachia
 
Umeweka hapa hoja ya msingi sana siyo akienda Azam tu bali hata Simba...huo ndio ukweli na sijui kuna nini, binafsi huwa sielewi pia... historia inaonyesha hivyo...Ezeckiel Greyson ilikuwa hivyo aliwika Yanga miaka ya 70 na alipokwenda Simba ikawa nidyo mwisho wa enzi...wapo wengi tu akina Omari Hussein, Maulid Dilunga, Edibily Lunyamila na kadhalika na kadhalika...Baadhi yao kama akina Omari Hussein, Said Mwamba na Lunyamila na pia Mohammed Hussein walirudi tena Yanga na wakatulia...

Ila mchezaji akitoka Simba na kuja Yanga nyota yake huwaka maradufu...Kama akina Method Mogella, Yondan, Deo Munishi, Ajib na wengine wengi tu...

Ukiona mchezaji ametoka Yanga na kwenda Simba wewe mhurumie tu....ni sawa na wachezaji wa Arsenal wengi wao wakitoka timu hiyo na kwenda timu nyingine hucheza kwa msimu mmoja tu na kupotea...
Kelvin Yondan

Amis Tambwe

Nurudin Bakari

Deo Munish

N.k
 
Wachezaji wengi uliowataja hawakuwika kwa muda mrefu walipokuwa Simba..Kiemba alikaa muda mfupi sana labda mwaka na sawa na China ambaye baadaye alikwenda ulaya. Hata Kipese hakucheza misimu miwili Simba kwa kumbukumbu zangu na pia Maftah. Nico Bambaga naye hakudumu sana na hata Aswile hakuwika zaidi ya misimu miwili...Banka??? Huyo nadhani alidumu msimu mmoja tu...Nemes?? huyu labda misimu miwili au mmoja na nusu,
Hamis Kiiza
 
Namkumbuka Edibily Jonas Lunyamila

Namkumbuka Mwinyi Rajab (Mrundi)

Hawa pia walicheza mpira Yanga, Simba wakaenda kula hela
Mwinyi Rajabu alikakishwa benchi na Issa Abushiri akakimbia.
Kikosi cha simba hii hakikuwa cha mchezo.

Nyuma JUMA kaseja kulia said sued kati pawasa na victor costa, kushoto Ramadhani Wasso dimba la kati yupo veron mwenyewe akisaidiwa na Christopher Alex au shekhani rashid pembeni kulia Ulimboka Mwakingwe kushoto issa abushiri au akilimali yahya mbele Golota na Emanuel Gabriel Batistuta au Machuppa huyo Rajabu mwinyi wako na lunyamila wangecheza wapi ? Bila kumsahau nteze John Rungu
 
Wachezaji wengi uliowataja hawakuwika kwa muda mrefu walipokuwa Simba..Kiemba alikaa muda mfupi sana labda mwaka na sawa na China ambaye baadaye alikwenda ulaya. Hata Kipese hakucheza misimu miwili Simba kwa kumbukumbu zangu na pia Maftah. Nico Bambaga naye hakudumu sana na hata Aswile hakuwika zaidi ya misimu miwili...Banka??? Huyo nadhani alidumu msimu mmoja tu...Nemes?? huyu labda misimu miwili au mmoja na nusu,
Mmetoka kuto wika mpaka kuto wika kwa mda mrefu
 
Kama alivoondoka Kessy
Niyonzima ndiye anayenishangaza zaidi! Jamaa walitoa hela ndefu ya kumsajili na anakula bonge la mshahara! Ukiondoka Yanga kwa adabu kama Msuva huwezi shindwa huko uendako
 
Najiuliza awa
1- Mohamed Banka Simba
2 - Yusuph Macho
3 - Athuman China
4 - Steven Nemesi
5 - Aizakiel Grayson Jujuman
6 - Amri Kiemba
Nao hao walichemsha
yanga wanakutandika misumari..labda uwe fiti pande hizo au wakuachie kiroho safi kama kizota
 
Pitia kumbukumbu zako vizuri
China amecheza miaka mingi Simba baada ya kutoka England kutafuta timu na kumalizia mpira wake Simba alipotoka hapo alienda kwa vitu vingine
Kipese alijiunga na Simba alicheza miaka mingi na miongoni mwa wwchezaji waliowezesha Simba kufika fainal ya kombe la CAF hadi ameacha kucheza mpira
Amri Kiemba amecheza Simba na alikuwa Star kipindi chake
Yusuph Macho pia
Nico Bambaga amecheza Simba kwa mafanikio sana hadi ameacha kucheza
Banka amecheza vizuri Simba kuliko Yanga kumbuka wakati yupo Yanga alikuwa ana majeraha kila wakati
Hugo unaebishana nae mpira bongo kaanza kuujuua juzi, hivyo yote utakayo muelewesha atabisha tu. Yeye anao wajua ni kina Yondani, Ajibu, Niyonzima basi
 
Hugo unaebishana nae mpira bongo kaanza kuujuua juzi, hivyo yote utakayo muelewesha atabisha tu. Yeye anao wajua ni kina Yondani, Ajibu, Niyonzima basi
Okwi alipoenda Yanga kiwango chake kilishuka sana, aliporudi Simba akarudi kwenye form, hata Kiiza alicheza vizuri sana akiwa Simba
 
Je Yanga ni wachawi? Je huwa wanatoa laana kwa wachezaji wanaohama klabu yao?

Mifano iko wazi kama ifuatavyo...

Frank Domayo alitoka Yanga akiwa fomu sana akaenda Azam Fc. Kila mmoja ni shahidi juu ya kilichomkuta Domayo. Goti linamuuma mpaka kesho, na hajawahi kurudi katika ubora wake.

Mrisho Ngassa alipoihama Yanga na kwenda Azam Fc uwezo ukaisha hapohapo.

Dider Kavumbagu alipoondoka Azam Fc kutoka Yanga aliishia kuchemsha.

Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima "Fabregas" alipoihama Yanga kwa mbwembwe na kutua Simba, hakuna asiyejua kinachomsibu kiungo huyo fundi wa mpira, amekuwa mchezaji.wa kawaida sana.

Yanga punguzeni misumari, msiwabanie wachezaji, wenzenu wanatafuta maisha
Unamshauri nini BM33
 
Back
Top Bottom