Kwanini Mchezaji akitoka Yanga kwenda Timu Nyingine Lazma Achemshe

Je Yanga huwa wanatoa laana kwa wachezaji wanaohama klabu yao?

Mifano iko wazi kama ifuatavyo...

Frank Domayo alitoka Yanga akiwa fomu sana akaenda Azam Fc. Kila mmoja ni shahidi juu ya kilichomkuta Domayo. Goti linamuuma mpaka kesho, na hajawahi kurudi katika ubora wake.

Mrisho Ngassa alipoihama Yanga na kwenda Azam Fc uwezo ukaisha hapohapo.

Dider Kavumbagu alipoondoka Azam Fc kutoka Yanga aliishia kuchemsha.

Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima "Fabregas" alipoihama Yanga kwa mbwembwe na kutua Simba, hakuna asiyejua kinachomsibu kiungo huyo fundi wa mpira, amekuwa mchezaji.wa kawaida sana.

Yanga msiwabanie wachezaji, wenzenu wanatafuta maisha
😁😂
 
HUuu Uzi utaishi miaka Elfu.
Utopolo siyo sehemu sahihi kwa Mchezaji mwenye malengo tulishasema na tutaendelea kusema. Kuanzia Viongozi na Mashabiki ni watu wenye akili kisoda na husda sana. Hizi aibu zitaendelea kuwaandama wasipo badilika
 
Endeleeni hivyo hivyo na ujinga wenu
 
Usisahau msuva alitoka yangu
Vipi upande wa simba
Luis Micquison alienda Al ahaly
Chama alitoka simba kwenda al ahly pia, mkude alitoka simba kaenda yanga
Nasoro Kapama saivi sijui yupo wapi yule jamaa.

Sio kwa ubaya lakini tuweke kumbukumbu sawa
 
Je Yanga huwa wanatoa laana kwa wachezaji wanaohama klabu yao?

Mifano iko wazi kama ifuatavyo...

Frank Domayo alitoka Yanga akiwa fomu sana akaenda Azam Fc. Kila mmoja ni shahidi juu ya kilichomkuta Domayo. Goti linamuuma mpaka kesho, na hajawahi kurudi katika ubora wake.

Mrisho Ngassa alipoihama Yanga na kwenda Azam Fc uwezo ukaisha hapohapo.

Dider Kavumbagu alipoondoka Azam Fc kutoka Yanga aliishia kuchemsha.

Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima "Fabregas" alipoihama Yanga kwa mbwembwe na kutua Simba, hakuna asiyejua kinachomsibu kiungo huyo fundi wa mpira, amekuwa mchezaji.wa kawaida sana.

Yanga msiwabanie wachezaji, wenzenu wanatafuta maisha
baada ya miaka mitano jibu ndio limepatikana, mayele amesema utopolo Wana majini
 
Back
Top Bottom