Kwanini Mchezaji akitoka Yanga kwenda Timu Nyingine Lazma Achemshe

VP Okwi
 
Amri Kiemba timu aliyochezea mda mrefu ni Simba.
Amri, alitoka Simba akaenda Yanga Akacheza mwaka mmoja, akarudi Simba.
Labda umepoteza kumbukumbu.

Alipotoka Yanga nakumbuka alikwenda kwanza huko Zanzibar, angalau hili nina uhakika nalo, alicheza huko Zanzibar ndipo akaenda tena Simba
 
Amri Kiemba timu aliyochezea mda mrefu ni Simba.
Amri, alitoka Simba akaenda Yanga Akacheza mwaka mmoja, akarudi Simba.
Labda umepoteza kumbukumbu.
Alianzia Yanga akashindwa akaenda kagera sugar msimu mmoja akaenda miembeni Zanzibar ndipo aliporejea Simba na kucheza misimu mitatu kwa mafanikio sana mpaka Rajer Casablanca wakataka kumsajili Simba wakagoma kumwachia
 
Kelvin Yondan

Amis Tambwe

Nurudin Bakari

Deo Munish

N.k
 
Hamis Kiiza
 
Namkumbuka Edibily Jonas Lunyamila

Namkumbuka Mwinyi Rajab (Mrundi)

Hawa pia walicheza mpira Yanga, Simba wakaenda kula hela
Mwinyi Rajabu alikakishwa benchi na Issa Abushiri akakimbia.
Kikosi cha simba hii hakikuwa cha mchezo.

Nyuma JUMA kaseja kulia said sued kati pawasa na victor costa, kushoto Ramadhani Wasso dimba la kati yupo veron mwenyewe akisaidiwa na Christopher Alex au shekhani rashid pembeni kulia Ulimboka Mwakingwe kushoto issa abushiri au akilimali yahya mbele Golota na Emanuel Gabriel Batistuta au Machuppa huyo Rajabu mwinyi wako na lunyamila wangecheza wapi ? Bila kumsahau nteze John Rungu
 
Mmetoka kuto wika mpaka kuto wika kwa mda mrefu
 
Kama alivoondoka Kessy
Niyonzima ndiye anayenishangaza zaidi! Jamaa walitoa hela ndefu ya kumsajili na anakula bonge la mshahara! Ukiondoka Yanga kwa adabu kama Msuva huwezi shindwa huko uendako
 
Najiuliza awa
1- Mohamed Banka Simba
2 - Yusuph Macho
3 - Athuman China
4 - Steven Nemesi
5 - Aizakiel Grayson Jujuman
6 - Amri Kiemba
Nao hao walichemsha
yanga wanakutandika misumari..labda uwe fiti pande hizo au wakuachie kiroho safi kama kizota
 
Hugo unaebishana nae mpira bongo kaanza kuujuua juzi, hivyo yote utakayo muelewesha atabisha tu. Yeye anao wajua ni kina Yondani, Ajibu, Niyonzima basi
 
Hugo unaebishana nae mpira bongo kaanza kuujuua juzi, hivyo yote utakayo muelewesha atabisha tu. Yeye anao wajua ni kina Yondani, Ajibu, Niyonzima basi
Okwi alipoenda Yanga kiwango chake kilishuka sana, aliporudi Simba akarudi kwenye form, hata Kiiza alicheza vizuri sana akiwa Simba
 
Unamshauri nini BM33
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…