Kwanini mechi za CHAN zimekosa hamasa na mahudhurio mazuri viwanjani Tanzania?

Tanzania hujinasibu kama taifa linalohusudu zaidi mpira na la viwango vya juu vya mpira Africa Mashariki, ajabu ni kwamba mahudhurio katika viwanjani katika CHAN ni haba sana na tunazidiwa hadi na taifa la wanariadha la Kenya!

Nimeshangaa hata mechi za timu ya Ibrah Traore (Burkinafaso) zilikuwa zimelala doro sana hakuna watazamaji kabisa pamoja pamoja na ufuasi mkubwa na hamasa aliyonao Ibrah Traore hapa bongo!
Usisiemu
 
Tatizo ni muda wa mechi
 
Simba na Yanga hata wakicheza saa saba usiku watu watajaa tu kiwanjani.
Unadhani wangeshuka kina Mo Salah na Victor Osimhen mambo yangekuwaje ? Ni vitu vingi vinachangia watu kutokujaa uwanjani pili huwezi kulinganisha Derby ambayo inakamiwa mwaka mzima (watani wa jadi) na haya mashindano yasiyo na ushindani....

Tatu sasa hivi watu wanacheki vitu kwenye luninga na kizazi hiki sidhani kama kinashobokea sana kwenda Ground....; Entertainment zimekuwa nyingi mpaka uwavute watu lazima ufanye kazi ya ziada; Mwisho kabisa ulianze ujinga kuanzia kipindi cha JPM kuifanya hii timu kama ni ya watu fulani na sio Taifa Stars
 
wanasema hiyo ni michuano midogo, wanasema AFCON ndio michuano mikubwa na ina msisimko
 
Muda unaochezwa hizo mechi nao unachangia mechi inaisha saa nne hapo uanze kutafuta usafiri na kesho inabid uende kazini
 
Simba na Yanga hata wakicheza saa saba usiku watu watajaa tu kiwanjani.
Timu ya taifa ni tofauti na Simba na Yanga
Mechi za Kenya zote wamecheza mchezo ndio watu walikuwa wengi
 
Hii mada ndio inazingumzwa azam tv muda huu kupitia sports am,wanasema kuwa:
1.foleni zinakera
2.muda wa usiku ni shida kwa watu wengi
3.ukosefu wa huduma za chakula na vinywaji pembezoni mwa uwanja.
Ni baadhi ya sababu sasa kama kuna mwingine ana hoja aziweke hapa
nilimwambia chawa mwenzio hapa juu ya michuano kutokujaza watu viwanjani AKANITUKANA SANA, hakujua kwamba ni mjinga ndo mana akaamua kuwa CHAWA. Sababu za viwanja kutojaa zilikuwa hivi
1. No reforms no election. timu ya taifa huchukuliwa kama ni timu ya serikali. kitendo cha serikali kugombana na wananchi wake kwa kesi ya lisu kilisababisha watu pia kususia kwenda uwanjani (hili lipo wazi ila wapuuzi watabisha)
2. ishu ya KARIA na uchaguzi wa TFF Uliojaa mizengwe, bwana karia aliwaletea wapenzi wa soka ghiriba kwenye uchaguzi watanzania siyo watu wa fujo ila kwa hapa tulipofikia upashanaji wa habari umerahishwa sana na ni rahisi watu kupashana habari juu ya mambo kama haya ya karia
wakamsusia michuano yake ingekuwa amri yangu ningewambia ile chan ya 2027 wapewe hata ,alawi
 
hoja dhaifu hizo
 
Siasa imeharibu mpira pia watanzania hawana furaha bora kunakucha na kuzama.
 
Back
Top Bottom