Kwanini Membe alazimishwe kumsamehe Musiba wakati maaskofu hao walikaa kimya Musiba alipomtukana Membe?

Kwanini Membe alazimishwe kumsamehe Musiba wakati maaskofu hao walikaa kimya Musiba alipomtukana Membe?

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
Watanzania tuache unafiki. Wakati Musiba anamtukana membe watu wote tulisikia na hao maaskofu walisikia.

Wananchi tulinyamaza hakuna aliyesimama kumkaripia au kumkataza musiba asimtukane membe na hata hao maaskofu walikaa kimya.

Mzee Membe na familia yake na marafiki zako walikubali aibu ya kutukanwa na musiba na kuamua kumshtaki na kushinda kesi. Mzee Membe bado alionesha uungwana wa kumtaka Musiba aombe msamaha lakini alikataa na wala hao maaskofu hawakutaka kumsihi Musiba akamwuombe msamaha mzee Membe bali walikaa kimya.

Najiuliza kwanini leo hao maaskofu ndio wanajitokeza kumtaka Membe amsamehe Musiba?

Kwanini kipindi Musiba anamtukana Membe walikaa kimya?

Kwanini Membe alipotaka musiba amwombe msamaha hawakumtaka Musiba aende?

Kwanini leo maji yamemfika Musiba shingoni ndio hao maaskofu wajitokeze?

Maaskofu acheni unafiki, Membe hamkumtendea haki na Musiba mwacheni apambane kama membe alivyopambana.

Unafiki ni dhambi.
 
Ndio tujitambue na kujitafakari Sana juu ya Imani tunayoweka kwa binadamu ( maaskofu na manabii)
badala ya kuiwekeza kwa Mungu.
 
Maaskofu Wanaa. Ndio tulitegemea wamwambie Magu aache udikteta ila wakaa kimya
Uki rudisha akili nyuma, hawa maaskofu walijua kila alicho kifanya Magu. Na walikuwa wakiunga mkono matendo yake ya kinyama.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba walikuwa wafuasi wa maovu ya mwenda zake. Team Magu kwa lugha nyingine . ambayo hata Musiba alikuwepo. Hivyo wana tumia kivuli cha kanisa kumuombea muovu mwenzao.
 
Ni unafiki tu
Woga wao umedhihirika ya kuwa wanapenda Dunia zaidi ya mwisho wao
Na moto ni mkali jamani ila wakamuogopa binadamu mwenzao ambae kawaacha
 
Wanaelewa thamani ya aliekuwa anamtetea.
 
Nadhani maaskofu wamshauri musiba aombe msamaha,na pia watoe somo kwa waumini wenye tabia kama za musiba wakome
 
Maaskofu wapumbavu pumbavu tu hao ukitoa hayo majoho yao wanayotishia watu wanabaki kuwa very average people walio jaa unafiki
 
MAASKOFU Acheni UNAFIKI MEMBE hamkumtendea HAKI na MUSIBA mwacheni APAMBANE kama MEMBE alivyopambana.
UNAFIKI ni DHAMBI.
Mwene kulifafuta mwene kulipata ndio hio definition kamili ya kilichompata Bwana Muziba
 
R.I.P Bernard Kamirius Membe

Mbele yeko nyuma YETU
In rairai wa rairai rajun
Bwana alitoa Bwana ametwa
Upumzike kwa amani
Nuru ya milele umpe eeh Bwana na
Mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa Amani
 
Watanzania tuache unafiki. Wakati Musiba anamtukana membe watu wote tulisikia na hao maaskofu walisikia.

Wananchi tulinyamaza hakuna aliyesimama kumkaripia au kumkataza musiba asimtukane membe na hata hao maaskofu walikaa kimya.

Mzee Membe na familia yake na marafiki zako walikubali aibu ya kutukanwa na musiba na kuamua kumshtaki na kushinda kesi. Mzee Membe bado alionesha uungwana wa kumtaka Musiba aombe msamaha lakini alikataa na wala hao maaskofu hawakutaka kumsihi Musiba akamwuombe msamaha mzee Membe bali walikaa kimya.

Najiuliza kwanini leo hao maaskofu ndio wanajitokeza kumtaka Membe amsamehe Musiba?

Kwanini kipindi Musiba anamtukana Membe walikaa kimya?

Kwanini Membe alipotaka musiba amwombe msamaha hawakumtaka Musiba aende?

Kwanini leo maji yamemfika Musiba shingoni ndio hao maaskofu wajitokeze?

Maaskofu acheni unafiki, Membe hamkumtendea haki na Musiba mwacheni apambane kama membe alivyopambana.

Unafiki ni dhambi.
Endelea kumshauri sasa.
Kuna wakati tutumie busara kushauri ili kudumisha utu na ustawi pia.
 
Yaan niugue kifua ghafla niwahishwe Kairuki alafu nife kirahisi rahisi tu ?
 
Maaskofu Wanaa. Ndio tulitegemea wamwambie Magu aache udikteta ila wakaa kimya
IMG-20230512-WA0069.jpg
 
Back
Top Bottom