Kwanini Messi anachukiwa sana, aliwakosea nini wanadamu? Je, chanzo ni kipaji chake au kuna jingine?

Hiyo ilikua ni trip nzima ya Barca. Hiyo kuchukiwa sana sidhani.
 
Mimi mbona simchukii.Messi asingezaliwa tungedanganywa sana Ronaldo anajua bolu.
 
Kwa takribani miongo miwili sasa Dunia ya soka imekua ni mpambano wa watu wawili tu Ronaldo Vs Messi……. Wengine wanaibuka miaka miliwili au mitatu wanapotea

Kwa muktadha huo wapenda soka wamegawanyika mara mbili bila wao kujijua, kuna mashabiki wa Messi B Ronaldo

Hizi makasiriko yote haya kwa Messi ni kwasababu amefanya makubwa na kiwaziba midomo team Ronaldo

Kwahiyo kama unampenda Ronaldo automatically utamchukia Messi
 

Analifahamu Sana Hilo,,Na Ndio Maana Anafanya Sana Vile....​
 
Hii nakataa
 
Hapa umeweka hasira zako tu..hata Ronaldo hamfikii Mess kwa Fair play nje ya uwanja...hapo sababu ni moja tu jamaa kaielezea hapo juu..kutendo cha kuzifunga team nyingi pamoja na zile alizokuwa anachezea Ronaldo ndo sababu ya kuchukiwa kweke
 
Haswa
 
Sababu ya kuchukiwa kwake ni kwakuwa anazifunga team nyingi ambazo Zina mashabiki wengi wa league ya england na mashabiki wa real Madrid and cr7 fans nothing else
Sio kweli. Gaucho alizigaraza timu zetu pendwa zote lakini hauwezi kumwona shabiki wa soka anamchukia au hamkubali Gaucho. Gaucho alishawahi kupigiwa makofi mpaka na mashabiki wa real madrid pale pale santiago bernabeu. Mimi nafikiri messi hana tu aura ya kupendwa
 
Kumpenda ronaldo haimaanishi automatically unamchukia Messi. Nyota ya kupendwa ni aura tu ya mtu. Huyo Ronaldo ndio kiumbe ambae anaongoza kuwa na followers wengi kwenye mitandao yote ya kijamii ambayo yupo active. Ronaldo kuwa na ushawishi zaidi messi ni aura tu, sio chuki.
 
Hivi messi ni myuda (judaism)?
Myahudi damuni bali mkristo mkatoliki. Ni kama mark zugerback, Albert eilstin, sergeant brim, zelensky ni wayahudi lakini hawafati Judaism. Rais wa Misri el sis, ukoo wa kifalme Saudia ni wayahudi lakini waislamu
 
Ronaldo ana nyota tu ya kupendwa, na kwa sababu kwa miongo miwili hawa jamaa wamekua wakishindanishwa ndipo hapo watu wana tafsiri kwamba messi anachukiwa. Lakini messi achukiwi na wapo wengi tu wanaompenda. Sema kwenye suala la kupendwa au ushawishi, messi hajafikia aura ya ronaldo.

Kama tunavyowahukumu kwenye ball na kusema messi anajua mpira. Haimaanishi kwamba ronaldo hajui mpira. Ronaldo mpira anajua lakini hajafikia kipaji cha messi
 
Sema tu mu argentina maana wa Argentina wote ni discendants wa Italian na spain
Siyo wote mkuu kuna native argentina ambao walimigrate kutoka Bolivia kwenda kusini ndio kina Diego Maradona, Sergio Aguro na Tevez wale ndio asili ya native Argentinian.
 
Sio kweli mkuu……..

Mara nyingi kwenye michezo ya USHINDANI automatically mtu utajikuta tu unapendelea upande fulani ushinde, hata sasa hivi ukifungua Tv ligi huijui au mabondia huwajui au wanariadha huwajui lazima itajikuta unataka fulani ashinde

Kinacho onekana kama ni CHUKI huwa ni hali ya kawaida tu kwenye ushindani………. Hakuna mshabiki wa Simba ataonyesha mapenzi kwa Pacome au Yanga kumpenda Mpanzu

Ronaldo ana mashabiki wengi zaidi ya Messi na ndio maana inaonekana kama anachukiwa na wengi sababu watakua wanaponda mafanikio yake
 
Unatumia kigezo gani kua “Ana nyota tu ya kupendwa?”

Ronaldo anajua zaidi kuji BRAND kuliko Messi

Wachezaji wengi wa Africa na America wao wanakomaa zaidi uwanjani lakini wachezaji wa Ulaya wanajua zaidi kuji brand na kwenda mbali zaidi nje ya soka uwanjani

So hiyo sio AURA ni BRANDING
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…