HOJA Kwanini mfumo wa benki wa kutathmini nyumba hautumiki kwenye mauziano na upangishaji kupata bei halisi?

HOJA Kwanini mfumo wa benki wa kutathmini nyumba hautumiki kwenye mauziano na upangishaji kupata bei halisi?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Ukienda kuomba mkopo benki, na nyumba au kiwanja ndio kikawa kama dhamana wathamini hufika na kufanya tathmini ya nyumba au kiwanja chako, kwa kuangalia eneo ulipo, thamani ya ardhi katika maeneo hayo, gharama za ujenzi, nk, na hapo hupata thamani halisi ya nyumba yako.

Au inapotokea kuna mradi wa serikali umepita kwenye kiwanja/nyumba yako na ukatakiwa kuhama, napo utafanyiwa tathmini kwa kuzingatia yote hayo ili kupata thamani halisi.

Tathmini haidanganyi, hata ukisema nyumba yangu ina thamani ya Bilioni 2, wakifika unaweza kukuta imeenda sana labda mil 100 - 200.

Sasa kwanini mfumo huu usiingie kwenye kupangisha na kununua nyumba au viwanja?

Maana bei zinazowekwa kwa wanaopangisha, kuuza nyumba na viwanja ni za ajabu. Mtu anaamka anajiamulia tu mambo kwasababu dalali kamwambia weka bei hii wateja wapo!

Ukienda Mbezi Beach, Mikocheni nyumba nyingi ni magofu, zimejengwa zamani, hakuna ukarabati wowote umefanyika kwa muda mrefu, unaambiwa vyumba vitatu dola elfu 3 (suala la kupangishwa kwa dola badala ya Tsh. kwa baadhi ya maeneo nchini tutajadili siku nyingine)! Yaani kivipi? Unaenda Makongo, vyumba viwili sebule na jiko unaambiwa laki 9, au Milioni!

Na kinachonishangaza zaidi eti nyumba ikiwa na tiles, mita ya peke yako, madirisha ya alminium, bei ndio inapanda maradufu, kama ingekuwa upange kwa laki 5 unaenda kupanga kwa Milioni! Hizi hesabu zinafanyikaje hapa?!

Utaratibu unatakiwa kuwa hivi, kila anayetaka kuuza au kupangisha nyumba yake lazima awe na cheti, fomu inayoonyesha thamani ya jengo, au kiwanja chake, na wananchi wapate range ambayo kweli inaendana na thamani ya jengo au kiwanja.

Tunasubiri mpaka crisis ifike ndio tuamke? Au mnapenda kuona vile wananchi tunahangaika na makazi? Eti Wizara ya Ardhi.

Serikali inaona hili haliwahusu lakini kodi zinazovyopanda zinafanya watu waishi katika mazingira yasiyo rafiki.

Kutokana na kuwa wengi hawawezi kumudu bei hizo, mwisho huyu mtu anaenda kukaa Mbagala, Kibaha, Mapinga, Bagomoyo, nk, wakati anafanya kazi katikati ya mji, mzigo unaongezeka mara mbili!

Huyu ataweza kufanya kazi vizuri au kila atakapopata nafasi ya kuiba, atahakikisha ameiba hadi ya kustaafia?

Hasara inaenda kwa nani? Kama wengi hawawezi kumudu gharama hizi, hii miradi ya nyumba inayofanyika kila leo itakosa watu, na gharama iliyotumika haiwezi kurudi, faida ndio kabisa itabaki kuwa ndoto, hasara inarudi kwa nani?

Kwanini hatuna usimamizi kwenye sekta hii? Eti Wizara ya Ardhi, Dr. Mwigulu Nchemba?

Eti Goba mtu anauza nyumba Bilioni 1.5, ukiangalia nyumba ya bei hiyo Kenya tu hapo ni mjengo wa maana, angalia nyumba zinazouzwa Bilioni 1.5 Marekani, halafu njoo ulinganishe na ya Tanzania, utachoka hadi kupumua!

Tupeni namba za mganga aliyeturoga Wakuu, dawa zake ni zenyewe!
 
Una hoja usikilizwe,
Kwa kifupi swala la ardhi kuna bei elekezi wizara ya atdhi per square meter lakini kama muuzaji ni serikali, ika watu binafsi wameachiwa huria.

Swala la kuover value vitu ukiachana na watu binafsi hakuna mtu mpumbavu, mpuuzi na bogus kama Mchechu aliyekuwa Boss wa NHC.

National housing ni huduma hata kama itakiwa kuendeshwa kubiashara isishindane na sekta binafsi si malengo ya kuanzishwa kwake.

Sasa wenye kipato cha chini wanauza haki zao za upangaji kuwapisha wsnye fedha maana hawana uwezo wa kulipa kodi alizoleta Mchechu, huyu mpuuzi amejenga appartment za NHC Morroco wanauza kwa million 400 wakati hakuna Mtanzania wa kawaida hata afanye kazi miaka 50 na kustaafu halipwi pesa hiyo, tuna wasomi wa hovyo walafi na waliohaa ubinafsi na roho mbaya kama hii takataka Mchechu.

Sasa ni kuchekesho eti Mbweni leo bei za Viwanja juu kisa nini? Upuuzi mtupu mtu anayejielewa akanunuwa viwanja kigamboni, napo bila Magufuli kupahujumu leo Kigamboni bei ya viwanja ingwkuwa kama Mbweni.

Bongo kuna upumbavu mwingi sana lakini usiingie mkenge wa kwenda kujenga kerege wakati mishe zako Town, wewe utakuwa ni mpumbavu zaidi ya bogus Mchechu.
 
Bado mnataka serikali ipange bei za kodi,nyumba? Acheni soko liamue. Kama Mikocheni nyumba ghali kapange au nunua huko Makongo. Soko ndio linaamua bei.

Yupo sahihi lazima kuwe na mamlaka ya kusimamia izo shughuli zote na udhibiti ,sidhani ata nchi zilizoendelea zinajifanyia vitu ivyo bila usimamizi wa mamlaka tz bado vitu vingi vinafanyika kienyeji sana na usimamizi mbovu.
 
Yupo sahihi lazima kuwe na mamlaka ya kusimamia izo shughuli zote na udhibiti ,sidhani ata nchi zilizoendelea zinajifanyia vitu ivyo bila usimamizi wa mamlaka tz bado vitu vingi vinafanyika kienyeji sana na usimamizi mbovu.
Hakuna nchi ilioendelea inapanga bei za nyumba za watu binafsi. Bei zinajipanga zenyewe kulingana na soko. Bei ya nyumba London sio sawa na bei ya nyumba Liverpool au Manchester.
 
Bado mnataka serikali ipange bei za kodi,nyumba? Acheni soko liamue. Kama Mikocheni nyumba ghali kapange au nunua huko Makongo. Soko ndio linaamua bei.
Kunatofauti kati ya serikali kupanga na serikali kusimamia(REGULATION).Kwa hali ilivyo kwa sasa BEI wala hazipangwi na SOKO,wala UBORA.Wamekaa wahuni fulani ambao hawalipi KODI TRA wala hawatoi EFD receipt wako tu mtandaoni wanapost NYUMBA wanasema CHUMBA na CHOO NDANI ni MASTER wanataka LAKI 2 KODI kwa Mwezi na ukilipa na wao uwalipe laki mbili ziada.

Binafsi naunga Mkono kabla hatujawa na CRISIS katika sekta ya REAL ESTATE ni MUHIMU Wizara ya Ardhi Ikaweka Regulations za kuongoza viwango vya RENT kama Ilivyo kwa Maji,Umeme na Basic Needs Nyingine.

Kumbuka Ardhi Mpya haizaliwi kila siku so inabdi tujifunze na tuzoee kuishi katika ardhi hii chache iliyopo kwa upendo na gharama nafuu.
 
Kunatofauti kati ya serikali kupanga na serikali kusimamia(REGULATION).Kwa hali ilivyo kwa sasa BEI wala hazipangwi na SOKO,wala UBORA.Wamekaa wahuni fulani ambao hawalipi KODI TRA wala hawatoi EFD receipt wako tu mtandaoni wanapost NYUMBA wanasema CHUMBA na CHOO NDANI ni MASTER wanataka LAKI 2 KODI kwa Mwezi na ukilipa na wao uwalipe laki mbili ziada.

Binafsi naunga Mkono kabla hatujawa na CRISIS katika sekta ya REAL ESTATE ni MUHIMU Wizara ya Ardhi Ikaweka Regulations za kuongoza viwango vya RENT kama Ilivyo kwa Maji,Umeme na Basic Needs Nyingine.

Kumbuka Ardhi Mpya haizaliwi kila siku so inabdi tujifunze na tuzoee kuishi katika ardhi hii chache iliyopo kwa upendo na gharama nafuu.
Chumba na choo ndani ni self contained na siyo Master bedroom.

Masters bedroom ni moja tu kwenye nyumba na ndio chumba kikuu kina space ya kutosha na mara nyingi ndio chumba cha Father house, hata kama nyumba nzima vyumba vyote vina choo na bafu bado huwezi kuita ni master bedroom, bali ni en-suite bedrooms.
 
Madalali ndo wanaharibu sana biashara ya nyumba/vyumba na kuumiza wapangaji. Fikiria mwenye nyumba anajenga nyumba yake vzuri tu, afu dalali anakuja anamwambia "hapa tupangishe kila chumba laki na nusu kwa sababu hapa goba kuna uhitaji sana" na mwenye nyumba nae anakubali bila ku-reason. Yaan dalalali anajipangia tu bei bila kuangalia ubora wa nyumba, wala factors nyngne za msingi. Mm binafsi nlikua sina mpango wa kujenga nyumba ya kuisho but kwa sababu ya huu upuuzi wa madalali, itabidi nijenge tu.
 
Wakuu,

Ukienda kuomba mkopo benki, na nyumba au kiwanja ndio kikawa kama dhamana wathamini hufika na kufanya tathmini na ya nyumba au kiwanja chako, kwa kuangalia eneo ulipo, thamani ya ardhi katika maeneo hayo, gharama za ujenzi, nk, na hapo hupata thamani halisi ya nyumba yako.

Au inapoteka kuna mradi wa serikali umepita kwenye kiwanja/nyumba yako na ukatakiwa kuhama, napo utafanyiwa tathmini kwa kuzingatia yote hayo ili kupata thamani halisi.

Tathmini haidanganyi, hata ukisema nyumba yangu ina thamani ya Bilioni 2, wakifika unaweza kukuta imeenda sana labda mil 100.

Sasa kwanini mfumo huu usiingie kwenye kupangisha na kununua nyumba au viwanja! Maana bei zinazowekwa kwa wanaopangisha, kuuza nyumba na viwanja ni ridicules, mtu anajiamlia tu mambo kwasababu dalali kamwambia weka bei hii wateja wapo!

Ukienda Mbezi Beach, Mikocheni nyumba nyingi ni magofu, zimejengwa zamani, hakuna ukarabati wowote umefanyika unaambiwa vyumba vitatu dola elfu 3! Yaani kivipi? Unaenda Makongo, vyumba viwili sebule na jiko unaambiwa laki 9, au milioni za zaidi!

Na kinachonishangaza zaidi eti nyumba ikiwa na tiles, mita ya peke yako, madirisha ya alminium, bei ndio inapanda maradufu, kama ingekuwa upande kwa laki 5 unaenda kupanga kwa milioni!
Yaani nini kinashindikana hapa? Kila anayetaka kuuza au kupangisha nyumba yake lazima awe na cheti, fomu inayoonyesha thamani ya jengo, au kiwanja chake, na wananchi wapate range ambayo kweli inaendana na thamani ya jengo au kiwanja.

Tunasubiri mpaka crisis ifike ndio tuamke, kama wengine wanaweza na hawana bei za kipuuzi kama sisi, hapa kwetu kinashindikana nini? Au mnapenda kuona vile wananchi tuhangaika na makazi? Wizara ya Ardhi

Serikali inaona hili haliwahusu lakini kodi zinazovypanda zinafanya watu waishi katika mazingira magumu, kutokana na kuwa wengi hawawezi kumudu bei hizo, mwisho huyu mtu anaenda kukaa mbagala, Kibaha, Mapinga, Bagomoyo, nk, anafanya kazi mjini, mzigo unaongezeka mara mbili Huyu ataweza kufanya kazi vizuri au kila atakapopata nafasi ya kuiba ataiba? Hasara inaenda kwa nani? Kama wengi hawawezi kumudu gharama hizi hii miradi ya nyumba inayofanyika kila leo itakosa watu, gharama iliyotumika haiwezi kurudi, faida ndio kabisa itabaki kuwa ndoto, hasara inarudi kwa nani? Kwanini hatuna usimamizi kwenye sekta hii? Wizara ya Ardhi Dr. Mwigulu Nchemba

Eti Goba mtu anauza nyumba B1.5, ukiangalia nyumba ya B1.5 Kenya tu hapo ni mjengo wa maana, angalia nyumba zinazouzwa B1.5 Marekani, halafu njoo ulinganishe na ya Tanzania, alooooo!

Tupeni namba za mganga aliyeturoga Wakuu, dawa zake ni zenyewe!
Ulianza vizuri ukamalizia vibaya. Kwani Mbagala, Kibaha, Mapinga, Bagamoyo n.k. kuna shida gani? Mara ya mwisho umefika lini? Kariakoo (hata Sinza, Bunju, Mikocheni) pale hakuna aliyekuwa anapataka kwenye miaka ya 70 mpaka 90. Leo bei zake unazifahamu? Ndiyo maana wanakuja wageni wananunua maeneo kama hayo nyinyi mnasubiri Sinza mpya huku mkiidai Tanganyika yenu msiyoijenga. Lakini usisahau na MONEY LAUNDERING ni sababu kubwa pia.
 
Nimeandika nyumba za watu binafsi. Hata Tz nyumba za NHC serikali ndio inafanya bei iwe chini vinginevyo ingekuwa kwenye market price.
Market ipi? The market in Tanzania is already distorted by many factors! Serikali inatakiwa iingilie kati. Kwani sekta binafsi serikali huwa haiingilii? Ni nini maana na lengo la Economic Regulation! Lengo mojawapo ni ku-correct market distortion. Serikali isiyoingilia ni ile isiyowajibika kwa raia wake.
 
Market ipi? The market in Tanzania is already distorted by many factors! Serikali inatakiwa iingilie kati. Kwani sekta binafsi serikali huwa haiingilii? Ni nini maana na lengo la Economic Regulation! Lengo mojawapo ni ku-correct market distortion. Serikali isiyoingilia ni ile isiyowajibika kwa raia wake.
Sawa.
 
Back
Top Bottom