Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,488
- 20,051
Mbona ipo hivyo ni vile tu watu hawapendi urasimu na mambo mengi
Uko sahihi Msechu aliharibu sana nhc. Moja ya sababu ya NHC kutobinafusishwa ni umuhimu wake kwa wananchi kupata malazi bora kwa bei nafuu. Unaposhindanisha shirika la umma na watu binafsi haya ndio matokeo yake.Una hoja usikilizwe,
Kwa kifupi swala la ardhi kuna bei elekezi wizara ya atdhi per square meter lakini kama muuzaji ni serikali, ika watu binafsi wameachiwa huria.
Swala la kuover value vitu ukiachana na watu binafsi hakuna mtu mpumbavu, mpuuzi na bogus kama Mchechu aliyekuwa Boss wa NHC.
National housing ni huduma hata kama itakiwa kuendeshwa kubiashara isishindane na sekta binafsi si malengo ya kuanzishwa kwake.
Sasa wenye kipato cha chini wanauza haki zao za upangaji kuwapisha wsnye fedha maana hawana uwezo wa kulipa kodi alizoleta Mchechu, huyu mpuuzi amejenga appartment za NHC Morroco wanauza kwa million 400 wakati hakuna Mtanzania wa kawaida hata afanye kazi miaka 50 na kustaafu halipwi pesa hiyo, tuna wasomi wa hovyo walafi na waliohaa ubinafsi na roho mbaya kama hii takataka Mchechu.
Sasa ni kuchekesho eti Mbweni leo bei za Viwanja juu kisa nini? Upuuzi mtupu mtu anayejielewa akanunuwa viwanja kigamboni, napo bila Magufuli kupahujumu leo Kigamboni bei ya viwanja ingwkuwa kama Mbweni.
Bongo kuna upumbavu mwingi sana lakini usiingie mkenge wa kwenda kujenga kerege wakati mishe zako Town, wewe utakuwa ni mpumbavu zaidi ya bogus Mchechu.
Umesoma kilichoandikwa lakiniNimeandika nyumba za watu binafsi. Hata Tz nyumba za NHC serikali ndio inafanya bei iwe chini vinginevyo ingekuwa kwenye market price.
Kuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,Wakuu,
Ukienda kuomba mkopo benki, na nyumba au kiwanja ndio kikawa kama dhamana wathamini hufika na kufanya tathmini na ya nyumba au kiwanja chako, kwa kuangalia eneo ulipo, thamani ya ardhi katika maeneo hayo, gharama za ujenzi, nk, na hapo hupata thamani halisi ya nyumba yako.
Au inapoteka kuna mradi wa serikali umepita kwenye kiwanja/nyumba yako na ukatakiwa kuhama, napo utafanyiwa tathmini kwa kuzingatia yote hayo ili kupata thamani halisi.
Tathmini haidanganyi, hata ukisema nyumba yangu ina thamani ya Bilioni 2, wakifika unaweza kukuta imeenda sana labda mil 100.
Sasa kwanini mfumo huu usiingie kwenye kupangisha na kununua nyumba au viwanja! Maana bei zinazowekwa kwa wanaopangisha, kuuza nyumba na viwanja ni ridicules, mtu anajiamlia tu mambo kwasababu dalali kamwambia weka bei hii wateja wapo!
Ukienda Mbezi Beach, Mikocheni nyumba nyingi ni magofu, zimejengwa zamani, hakuna ukarabati wowote umefanyika unaambiwa vyumba vitatu dola elfu 3! Yaani kivipi? Unaenda Makongo, vyumba viwili sebule na jiko unaambiwa laki 9, au milioni za zaidi!
Na kinachonishangaza zaidi eti nyumba ikiwa na tiles, mita ya peke yako, madirisha ya alminium, bei ndio inapanda maradufu, kama ingekuwa upande kwa laki 5 unaenda kupanga kwa milioni!
Yaani nini kinashindikana hapa? Kila anayetaka kuuza au kupangisha nyumba yake lazima awe na cheti, fomu inayoonyesha thamani ya jengo, au kiwanja chake, na wananchi wapate range ambayo kweli inaendana na thamani ya jengo au kiwanja.
Tunasubiri mpaka crisis ifike ndio tuamke, kama wengine wanaweza na hawana bei za kipuuzi kama sisi, hapa kwetu kinashindikana nini? Au mnapenda kuona vile wananchi tuhangaika na makazi? Wizara ya Ardhi
Serikali inaona hili haliwahusu lakini kodi zinazovypanda zinafanya watu waishi katika mazingira magumu, kutokana na kuwa wengi hawawezi kumudu bei hizo, mwisho huyu mtu anaenda kukaa mbagala, Kibaha, Mapinga, Bagomoyo, nk, anafanya kazi mjini, mzigo unaongezeka mara mbili Huyu ataweza kufanya kazi vizuri au kila atakapopata nafasi ya kuiba ataiba? Hasara inaenda kwa nani? Kama wengi hawawezi kumudu gharama hizi hii miradi ya nyumba inayofanyika kila leo itakosa watu, gharama iliyotumika haiwezi kurudi, faida ndio kabisa itabaki kuwa ndoto, hasara inarudi kwa nani? Kwanini hatuna usimamizi kwenye sekta hii? Wizara ya Ardhi Dr. Mwigulu Nchemba
Eti Goba mtu anauza nyumba B1.5, ukiangalia nyumba ya B1.5 Kenya tu hapo ni mjengo wa maana, angalia nyumba zinazouzwa B1.5 Marekani, halafu njoo ulinganishe na ya Tanzania, alooooo!
Tupeni namba za mganga aliyeturoga Wakuu, dawa zake ni zenyewe!
Tatizo watu wengi wana ji brand katika position ambazo hawana uwezo nazo,mimi nipo mbagala,siwezi kuishi masaki, ""ukijikweza sana utachanika msamba""Bado mnataka serikali ipange bei za kodi,nyumba? Acheni soko liamue. Kama Mikocheni nyumba ghali kapange au nunua huko Makongo. Soko ndio linaamua bei.
Market distortionKuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,
Mfuko wako utaamua upate nyumba ya bei gani?
Ndio maana mfumo rasmi unatakiwa kuwepo, gharama na kila kitu kiwekwe. Hutaki kufanya evaluation hupangishi au kuuza eneo lako.Kwa ufupi, hiyo inawezekana lkn je nani atagharamia gharama za hiyo valuation, mwenye nyumba gani akubali kuingia gharama ya kumleta mthamini.
Baadhi ya taasisi kubwa au makampuni makubwa yanafanya, kujua bei ya soko kabla ya kupangisha.
Kitu simple tu: Valuation for Rental Purpose, mambo ya Years Purchase:
CV= NI x YP.
Sio kadri ya mfuko wako ni kadri ya THAMANI ya kiwanja au nyumba yako!Kuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,
Mfuko wako utaamua upate nyumba ya bei gani?