HOJA Kwanini mfumo wa benki wa kutathmini nyumba hautumiki kwenye mauziano na upangishaji kupata bei halisi?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mbona ipo hivyo ni vile tu watu hawapendi urasimu na mambo mengi
 
Uko sahihi Msechu aliharibu sana nhc. Moja ya sababu ya NHC kutobinafusishwa ni umuhimu wake kwa wananchi kupata malazi bora kwa bei nafuu. Unaposhindanisha shirika la umma na watu binafsi haya ndio matokeo yake.
 
Sahihi!

Kama uswahilini wanauza nyumba kutokana na idadi yao na ili akapate kibanda baada ya mgawanyo na sio thamani ya eneo halisi.
 
Kwa ufupi, hiyo inawezekana lkn je nani atagharamia gharama za hiyo valuation, mwenye nyumba gani akubali kuingia gharama ya kumleta mthamini.
Baadhi ya taasisi kubwa au makampuni makubwa yanafanya, kujua bei ya soko kabla ya kupangisha.
Kitu simple tu: Valuation for Rental Purpose, mambo ya Years Purchase:
CV= NI x YP.
 
Kuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,
Mfuko wako utaamua upate nyumba ya bei gani?
 
Bado mnataka serikali ipange bei za kodi,nyumba? Acheni soko liamue. Kama Mikocheni nyumba ghali kapange au nunua huko Makongo. Soko ndio linaamua bei.
Tatizo watu wengi wana ji brand katika position ambazo hawana uwezo nazo,mimi nipo mbagala,siwezi kuishi masaki, ""ukijikweza sana utachanika msamba""
 
Kwa nilichokiona kwenye uthamini kupisha SGR ni bora hata hizi bei za madalali wa mjini.

Nyumba za tope slope vijijini huko watu wanakunja hadi 40M

Ndiyo maana hakuna mahali watu wamegomea fidia toka mradi uanze ni neema tupu.
 
Kuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,
Mfuko wako utaamua upate nyumba ya bei gani?
Market distortion
 
Ndio maana mfumo rasmi unatakiwa kuwepo, gharama na kila kitu kiwekwe. Hutaki kufanya evaluation hupangishi au kuuza eneo lako.

Bila evaluator kupita nyumba au kiwanja chako hakiingii sokoni, na evaluator akipiga bei ya juu mteja akaenda kulalamika na ikabainika ni kweli Evaluator na nyumba/kiwanja wote mnapigwa fine na record yenu ya udanganyifu inaingia kwa public record kwa kila mtu kuona!
 
Kuna nyumba za aina mbalimbali kwa kadri ya mfuko wako ulivyo,ukitaka nyumba ya 50,000/- utapata,ya 150,000/- utapata, ya 250,000/- utapata,ya 500,000/- utapata, ya 1000,000/- utapata,
Mfuko wako utaamua upate nyumba ya bei gani?
Sio kadri ya mfuko wako ni kadri ya THAMANI ya kiwanja au nyumba yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…