Umetumia njia ya kiboya sana kutaka kujua jinsi gani huyo Majaaliwa wako anakubalika.
Watanzania tuna upumbavu mmoja wa kutarajia mabadiliko yatatokana na mtu ambae misingi yake ya utawala itasimamiwa na katiba hii hii ya kipumbavu ikisindikizwa na chama hiki hiki kilichopoteza tija na muelekeo miaka 30 iliyopita.
For as long as katiba ni hii iliyopo na chama ni CCM madarakani tusitarajie mabadiliko yeyote.
Hata akija malaika kuwa raisi, akikuta kiasi cha nguvu alichonacho kwa mujibu wa katiba iliyopo atabadilika na kuwa shetani tu.
Msingi wa uongozi wa nchi hii naumithilisha na mtu anaetunga mtihani, anaufanya mwenyewe na kujisahihishia halafu utarajie apate chochote pungufu ya alama ya juu kabisa.
Raisi anateua msimamizi wa tume ya uchaguzi, raisi ana uwezo kuingilia mahakama na kuamua hatia ama innocence ya mtu, raisi ana uwezo wa kujilimbikizia kila aina ya kinga halafu unatarajia kutakuwa na kiongozi mwema.