Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja na WADUDUSi alituma mjumbe wake Prime Minister au mlitakaje?
Kwa sababu mwaka jana alitoa ahadi ya uongo, sura likamshuka mwaka huu akashindwa kuja kutoa uongo mwingine.Habari ya kazi wakuu!!
Naomba kwenda moja kwa moja kwenye hoja.
Hili nimekaa nalo sana tangu tarehe moja hadi leo na kila siku linaniumiza, nikikaa na wafanyakazi wenzangu naona wanahoja tofauti tofauti sasa leo nimeamua kuja mbele yenu wanajukwaa mnisaidie hili.
Nimetonywa hapa kuwa katiba ya JMT inamtambua moja kwa moja Mh Rais kama ndiye mgeni rasmi kwenye sherehe zote za kitaifa so kwa uelewa wangu mdogo najua kuwa ata hasipopata mwaliko ila akiamua kwenda kwenye sherehe husika bado atakuwa mgeni rasmi.
Sasa katika sherehe za Mei Mosi 2024 pale Arusha kwa baba Keegan hatukumuona mama yetu mpendwa na badala yake alikuepo Daktari Mpango. Hii ilikuwa ni tofauti na matarajio yetu watumishi kwani kwa miaka yote tumekuwa tukishuudia uwepo wa Top 3 (sasa Top 4) ya serikali yote ktk sherehe hizi.
Tunajua ratiba ya Rais ni ngumu sana ila kiukweli watumishi tumefadhaika sana kwa kutokuwepo kwa mama yetu katika sherehe zetu kwa sababu:
Sasa wanajukwaa kwa kuwa mimi nipo Kijijini Kidologwai na sina chaji na solar hazichaji kwa sababu jua halitoi kutokana na mvua na mawingu mazito, na pia uhenda kuna taarifa ilitoka ila sikuipata wala kuisikia naomba niishie hapa kwa kuwauliza, kwanini Mh Rais hakutokea kwenye sherehe za Mei Mosi2024 pale Arusha??
Rais Samia mgeni rasmi Mei Mosi mkoani Arusha, maandalizi yafana
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani ,Mei Mosi yanayotarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Arusha. Akiongea na vyombo vya habari Mkoani hapa, Rais wa Shirikisho la wafanyakazi Tanzania,TUCTA, Tumaini Nyamhokya alisema maadhimisho...www.jamiiforums.com
As long as mkazi wa kigoma yupo basi ataendelea kuwakwepa kadri iwezekanavyo.Atatukwepa hadi lini? SI angekuja tuyamalize tu