Kwanini Mh Rais hakutokea kwenye sherehe za siku ya wafanyakazi (Mei Mosi)

Watoto wamekataliwa na Taifa/Mamlaka kwa kutoboresha maslahi ya mwalimu. Waache liwe Taifa la watu mbumbumbu.
Sasa tutamwachia nani ajenge hii nchi kama tutaendelea kususiana
 
Unaweza kwenda kwa mtu anaekudai kama hunauwezo wa kulipa deni?
 
Kwa sababu mwaka jana alitoa ahadi ya uongo, sura likamshuka mwaka huu akashindwa kuja kutoa uongo mwingine.
 
Aliogopa masuala ya Kikokotoo kwa Wastaafu. Kuna Ile Aibu kuwa ni kweli hawa Wazee wanadhulimiwa naweza kuwaFace? Eti unatunzia mstaafu 67% ukimpa kidogo kwa Miaka 12 na nusu. Pension wamenyimwa wanapewa Tu Ile lump-sum ya Kiinua mgongo.
 
Ni aibu sana! Hili ndo lilomkimbiza mana hasingeweza kulikwepa pale. Wazee wamefanya kazi kwa nguvu na muda wao wote sasa wanatakiwa kupumzika na familia zao lakini wanawapangia Cha kuwalipa na namna wakati ni michango yao. Inasikitisha na kuhuzunisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…