Kwanini miaka chini ya 2000 matikiti maji yalikua adimu?

Kwanini miaka chini ya 2000 matikiti maji yalikua adimu?

First of all let me dealer interest mimi ni afisa kilimo hivyo ngoja nikujibu kitaalam kidogo!
Pana mambo kama mawili au matatu hivi yaliyokua yanasababisha hiyo hali unayoiona lakini kubwa kabisa ni kilimo kutokua cha KIBIASHARA.
Utakubaliana na mimi kua kwa miaka ya hivi karibuni atleast watanzania tumeanza kukiona kilimo kwa mtazamo tofauti, na kuanza kulima kibiashara sasa hii imepelekea wakulima kuanza kulima si tu kwa kutegemea msimu wa mvua bali kwa kumwagilia kwa njia mbali mbali kuanzia visima, kumwagilia kwa kutegea maji mtoni mpaka kwa njia ya matone ikiwa ni mapinduzi ya kisayansi mpaka sasa katika sekta yetu ya kilimo.

Sababu nyingne kubwa zaidi ni uwepo wa mbegu za kisasa za mazao mbali mbali ikiwemo na hizo za matikiti kwani haya ya kisasa yamekuja na sifa ambazo zile mbegu zetu za asili hayakua na uwezo wa kua nazo ndo mana yakafanya zao hili kutokua maarufu!.
Mbegu za kisasa zmekuja na sifa za kukomaa mapema ndani ya siku 60 - 75 tayari linakua limekomaa tayari kwa kupelekwa sokoni pia matikiti yake yanakua makubwa (baadhi ya varieties zinaenda mpaka kilo 7 - 10 Kwa tunda moja) kitu ambacho matikiti yetu ya asili hayakua na uwezo huo wa kua makubwa kwa kiasi hiko pia varieties za kisasa matikiti yake ni matamu sana (sina haja ya kulielezea hili sote tunafahamu) na per one acre unaweza kuvuna zaidi ya tani 20
Kwa sababu hizi nadhani utakua umenipata!
Asante kwa jibu murua...

Kwa hiyo sasa tunakula tikiti chotara la maabara na asili, kama ilivyo btoiler chicken, ng'ombe wa kisasa n.k..
Hizi afya zetu zipo matatani...
 
Tokea nianze kupata ufahamu mwishoni mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, sikuwahi kuona mtu anakula tikiti maji wala mimi kula... Je Tunda hili limepata umaarufu kwa ajili ya nini ? Maana zamani kilikua chakula cha nguruwe na ng'ombe kama ilivyo malapu lapu ya mbwa siku hizi mnaita michemsho...
Tikiti maji kwa nini zamani hatukula?
Malapulapu umenikumbusha mbwa wangu
 
Umenena kweli mkuu na hili ndiyo jibu matikiti ya sasa hivi ni yale ya laboratory siyo ya asili ndiyo maana kila siku yapo tu hayana msimu zamani matunda yalikuwa yana msimu na unajulikana kipindi hiki ni msimu wa embe baadaye nanasi, machungwa nk siku hizi mambo ya mabadilika mwaka mzima matunda yapo maana ni matokeo ya laboratory tutaachaje kuumwa?

Ndiyo maana yale magonjwa waliokuwa wanaumwa watu wazima nayo siku hizi hadi watoto wanayo chanzo.....
Hata maembe ya asili hakuna tenazamani msimu wa maembe ukienda sokoni utasikia harufu ya maembe ila sasa hayana harufu wala ladha yyaan maji tupu
 
Hata maembe ya asili hakuna tenazamani msimu wa maembe ukienda sokoni utasikia harufu ya maembe ila sasa hayana harufu wala ladha yyaan maji tupu
Hakuna tunda wala zao la nafaka ambalo halijaboreshwa yote ni matokeo ya maboresho hayo mbegu za asili za zamani kama zipo ni chache sana na matokeo yake ndiyo haya tunayaona kila leo afya kuzorota, magonjwa mengi nk maana vile tulavyo ni sumu za kutosha ingawa zinaumiza taratibu
 
Mpaka parachichi???
 
Hakukuwa na wazalishaji wengi. Tunda hili halikupewa umuhimu mkubwa. Nakumbuka mimi nikiwa mdogo, nyumbani tulikuwa tunakula matikiti mara moja ama mbili tu kwa mwaka. Ilikuwa bidhaa adimu sana
 
Tokea nianze kupata ufahamu mwishoni mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, sikuwahi kuona mtu anakula tikiti maji wala mimi kula... Je Tunda hili limepata umaarufu kwa ajili ya nini ? Maana zamani kilikua chakula cha nguruwe na ng'ombe kama ilivyo malapu lapu ya mbwa siku hizi mnaita michemsho...
Tikiti maji kwa nini zamani hatukula?

Mkuu "Tikitimaji" ni Tikiti la aina gani?
 
Tokea nianze kupata ufahamu mwishoni mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, sikuwahi kuona mtu anakula tikiti maji wala mimi kula... Je Tunda hili limepata umaarufu kwa ajili ya nini ? Maana zamani kilikua chakula cha nguruwe na ng'ombe kama ilivyo malapu lapu ya mbwa siku hizi mnaita michemsho...
Tikiti maji kwa nini zamani hatukula?
Mkuu hili nalo litapita na malapulapu kua ni mchesho kwa kweli yajayo yanafurahisha...kaa tayari siti za mbele
 
Ni katika suala la kutafuta fursa na uhamasishaji;mfano nyama ya sungura ni nzuri,nyama na mayai ya kware yanaongeza CD4,asali inaongeza nguvu za kiume n.k hiyo yote ni kutafuta fursa na mwisho wa siku wanawekeza huko na uzalishaji unaongezeka.
 
Back
Top Bottom