Kwanini mikate mingi ina mchanga siku hizi?

Kuna mda kula mikate ni dalili ya kuficha umasikini. Mkate wa buku unauwakika wa kula siku 3-4 ila magimbi/gombi la buku unaweza kula siku 1-2 kwa maeneo ya mjini.
 
Tatizo mda wa kupika hayo magimbi
 
Viwanda vya Mikate saiv NI mingi Sana ,na ubora upo chini Sana ,kwanza ni michachu,inavunjika hovyo,ukifungua tu mkate bac kesho huwez ukaula Tena inawahi haribika.mkate mzuri ni ile brand ya zamani adi Sasa ipo.
 
Bidhaa nyingi za ndani ziko chini ya kiwango ukilinganisha na zile za Kenya.
 
Itakuwa ile tekinolojia ya zamani ya kukandia miguu imerudi.

Umeme hamna kila wakati unakatika. Mwenye kiwanda atafanya nn hata ungekuwa wewe.

Japo napenda sikonsi sijui nifanyeje duuuu
 
Mkate hautafunwi..
Unachovya kwenye kikombe cha chai au maziwa ukilainika unaufyonza na kuuweka sawa usawa wa njia ya koromeo na kumeza
 
Mihogo inanunuliwa!

Navyojua, mtu anang'oa shambani kwake na kuja kuchemsha.

Hili la kununua sijawahi lisikia mie!
Hahaaaaaa hahaaaaaa.
Kwani kila mtu analima mkuu???
Hujawahi kwenda masokoni ukaona mihogo inauzwa?
Kama unavyonunua mchele dukani, hata mihogo inauzwa sokoni na vibandani (au na mchele unajilimia?)
Dar wanakula mihogo inayotoka sehemu za pwani, Tanga, Lindi na Mtwara.
Duuuh sikutegemea kama mpo.
 
backary zimekuwa nyingi mno alafu unakuta baadhi yao mazingira ya uandaaji ni local sana mtu ana fanya backing ya vipande vya mkate alafu anaweka zakafuni ambapo hapaeleweki ki vile unategemea nini wanacho angalia ni fedha na wala si afya za walaji ndio maana mambo ndio kama haya.Cha msingi kabla ya kununua fanya utafiti wa kampuni ya waandaaji yenye viwango kama unataka kuepuka hayo.
 
Ni kweli si jambo jipya ila hapo kilicholeta mshtuko ni uhusiano wa huo mchanga na kukandia miguu...kwamba mtu anatoka kukanyaga mchanga moja kwa moja anaingia kwenye unga?
Umetoka kwenye mazoezi ya mpira kisha unapitia bekari kwenye kibarua cha kukanda unga, unaosha miguu kisha unatembea mpaka kwenye bafu la kukandia unga, hapo ndipo unapobeba mchanga.
 
Mbona kama umekuja na povu badala ya suluhisho la alichouliza mleta mada?
 
Tbs wapo, tfda wapo, afisa afya wapo hakuna kinachofanyika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…