Ni matokeo ya siasa za kidunia, hazina sababu za msingi za wananchi wa kawaida wa Afrika.
Mapinduzi haya, yanaratibiwa na mataifa yenye nguvu kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.
Sio mapinduzi yanaratibiwa na kusukumwa na uhitaji wa ndani ya Afrika.
Kinachoendelea kwenye wimbi hili la sasa ni regime change na sio philosophical reforms. Falsafa inabaki ile ile, watu serikalini ndio wanaobadilika.
Mfano: Kitendo cha Marekani kulipua bomba la Urusi kutoka Urusi- Ulaya (Nord-stream) ndio sababu Kuu ya Mapinduzi ya Gabon. Usiniulize kwa namna gani, chekecha kichwa utapa jawabu.
Kwasasa, Hakuna mapinduzi yatakayo ratibiwa na wananchi wa kawaida (Afrika) wenyewe yatakayofanikiwa bila kuhusisha maslahi ya mataifa yaliyoendelea kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia.
Kwasasa wamiliki wa uchumi, jeshi na teknolojia wa ulimwengu wameshagawana vitalu vya kuvuna kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni mkongwe.
Hivyo, sio rahisi kwa wananchi wa kawaida kuanzisha na kufanikiwa kufanya mapinduzi.