SoC01 Kwanini misaada na mikopo haiwasaidii Waafrika ila inawafanya wawe masikini zaidi?

SoC01 Kwanini misaada na mikopo haiwasaidii Waafrika ila inawafanya wawe masikini zaidi?

Stories of Change - 2021 Competition

Ghost boss

Member
Joined
May 3, 2019
Posts
33
Reaction score
57
Nchi nyingi za kiafrika huwa zinapokea mikopo na misaada kutoka nje ya afrika, ila mikopo hii na misaada inaonekana kuto wanufaisha waafrika kiujumla ila zaidi inawaweka katika mzigo Wa madeni na mtego Wa masharti kandamizi, hapa panaitaji umakini zaidi na ndio maana nimeandika ili angalau tuone sasa mabadiliko yakipatikana, Mara nyingi viongozi wetu wanabeba msalaba mikubwa ya kuonekana mafisadi kwa kuiba pesa za misaada na mikopo inayoletwa afrika.

Ila ukweli ni kuwa viongozi wetu wanapaswa kuongeza umakini zaidi juu ya misaada wanayoipokea na mikopo wanayokopa kwani kama misaada na mikopo haiwezi kuwanufaisha waafrika basi ni afadhali wasikope au kupokea misaada maana kinyume chake wanakuwa wanaongeza utajiri wawazungu badala ya wote kunufaika(win win situation).

Mara nyingi kukosa umakini kwa viongozi wetu kunafanya nchi zetu za afrika kuchezewa kiuchumi na kushambuliwa kwa kukosa umakini, kwa maana asilimia kubwa ya mikopo inayoletwa afrika huwa na masharti ambayo kimsingi hana faida kwa maslai ya taifa kwa ujumla.

Unakuta serikali ya kiafrika inaomba mkopo benki ya dunia lakini inapewa masharti kuwa ili kutekeleza mradi ambao wanataka wakope basi ni lazima wawachukue wataalamu kutoka huko ulaya kana kwamba afrika hatuna wataalamu, na kama haitoshi pesa za mladi huo utolewa kwa awamu na kulipwa moja kwa moja kwa wataalamu yaani nikama pesa inarejeshwa kule ilipotolewa na sisi kubaki na madeni na ndio maana hatuoni faida ya pesa za mikopo katika mzunguko na zaidi pesa zetu zaidi uchukuliwa kulipia madeni ambayo kimsingi sisi hatukuiona pesa yake kwenye mzunguko kama wazawa wangepata tenda kwa mabilioni ya dola yanayotolewa basi nchi za kiafrika zingelikuwa na ukuaji mzuri Wa uchumi Wa watu kwani pesa ingekuwa inazunguka sana mifukoni mwa watu.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom