MWANDENDEULE
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 4,099
- 7,466
Very trueSababu mji mdogo mtu mmoja anaweza ambukiza mji wote
View attachment 461162
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia takwimu mbali mbali kupitia vyombo mbali mbali kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi na waathirika wa UKIMWI.
Swali langu ni la kidadisi(curiosity). Napenda kusikia toka kwa wataalamu na watafiti(kama tafiti zipo), kwanini isiwe majiji na mikoa mikubwa kama Dar, Mwanza, Mbeya n.k? Kama awali ilikuwa mkoa wa Kagera ndiyo ulioripotiwa mgonjwa wa kwanza na baadaye kuwa na waathirika wengi, ilikuwaje HIV iliruka mikoa ya hapo kati(Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida...) na kuufanya mkoa wa Njombe kuongoza?
Kama ni tohara kwa wanaume je, ni mikoa mingapi Tanzania hii walichelea kufanya tohara? Kwanini mikoa hiyo haijaathirika kiasi hicho? Japo kwa zamani(ninavyokumbuka) wilaya ya Makete(Njombe) ndiyo iliyokuwa ikiongoza na kwa sasa sina taarifa rasmi, bado ni jambo ambalo sina majibu yake, ilikuwaje mkoa wa Njombe uongoze kwa maambukizi?
Naomba wenye kufahamu majibu ya swali langu la msingi wanisaidie.
Kwanini Njombe?
Dah bora aisee ngoja nasi tupumue maana Kagera mmetusema sana.
Takwimu nazo za kuangalia. Tunaposema sehemu fulani inaongoza, kwangu mimi, idadi ya watu lazima iwe sawa halafu upande mmoja waathilika wawe wengi. Huku kuongoa kwa asilikia siyo realistic sana... kwa mfano, mmoja katika wawili ni 50% na wawili katika wanne ni 50%. Sasa hapo kusema maambukizi yapo sawa pande hizo mbili nayo nna mashaka nayo
Takwimu za kiutafiti hazihitajiki saaaaaana, hasa ukijua kuwa njia kuu ya kusambaza VVU katika nchi yetu ni uzinzi na uasherati. Kwa sababu hiyo nashawishika kuchangia kuwa viwango vikubwa vya maambukizi katika mkoa wa njombe na maeneo jirani ni viashiria vya tabia hatarishi walizonazo wakazi wa maeneo hayo ambazo zaweza kuchangiwa na elimu ndogo juu tatizo hili la VVU/UKIMWI. Wakati tunasubiri wenye tafiti kutoa majibu yao kwa swali hili, ebu kila mmoja atafiti tabia yake mwenyewe, kugundua tabia gani hatarishi aliyonayo, ili abadilike kabla haijamletea VVUlete takwimu za Ukimwi Zanzibar ndio inaongoza kwa maambukizi kidogo kupita sehemu zote
Nashangazwa kidogo na hili maana nimeshasikia hata wataalamu was afya wanaunga mkono hoja hii ila mi sikubalianinayo. Sorry.Watu wa njombe wanatamaduni ya kupima zaidi ya sehem moja huku akitumia majina tofauti kila kituo hasa ikitokea amekutwa na vvu hivyo takwimu zikichuliwa inaonesha waathirika ni wengi lakini si kweli kuwa njombe inaongoza
I see wakati nasoma hili jibu kwenye uzi wako, sikuwa nimeona kama umeweka msisitizo kwenye sababu ya tatu lakini moja kwa moja niliikubali sana.Kuna sababu mbalimbali zinazochangia maambukizi ya VVU kuwa makubwa katika mikoa ya Njombe na Iringa. Sababu hizo ni kama ifuatavyo
1. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa kazi za ndani
Wasichana wengi wamekuwa wakitoka katika hiyo mikoa kuja kufanya kazi za ndani na hawa wamekuwa wahanga wa ngono kutoka kwa mabosi wao. Wengi wamekuwa wakiambukizwa HIV na kisha kurudi kwao ambako wamechangia kuambukiza watu wengine
2. Kuoa wajane. Hii ni mila ya kawaida miongoni mwa hawa watu ambao wamekuwa wakirithi wake wa ndugu zao.
3.Ukaribu na nchi za kusini husani Afrika Kusini. Ukiona serotype ya HIV inayoathiri watu wa mikoa hiyo ni tofauti na aina za maeneo mengine isipokuwa nchi za Afrika Kusini. Inaaminika serotype hiyo imetoka huko na kuathiri watu wa mikoa hiyo. Aina hiyo ya virusi iko katili kidogo kuliko virusi wengine. Subtype C iko Afrika Kusini na maeneo ya Afrika Mashariki ni A na D .
4. Pia mikoa hiyo kuwa katika maeneo ya mpakani, kuwa na centre na route nzuri za biashara kumechangia maambukizi kuwa juu.
Nchi kama Uganda walifanikiwa kupunguza maambukizi kutokana na kuongeza matumizi ya kondom na kupunguza mapenzi miongoni mwa wasichana wadogo.
NB: Sababu ya tatu ni ya muhimu sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Braza, kwa hili labda aje Papa Mobimba mimi utanionea.Yani bado tu watu wanadanganywa na hii sayansi feki ya HIV.hakuna propaganda ya kipuuzi kama hii ya Kitu kilichopewa Jina la HIV. Kifupi Hakuna kitu kinachoitwa HIV zaidi tu ya uzushi wa kina Robert Gallo .Tabho mbeki alipoteza uraisi wake baada ya kutoa hii Siri wenye miradi yao wakamshughuliki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo achana nae, maana ana macho lakini haoniBraza, kwa hili labda aje Papa Mobimba mimi utanionea.
Mkuu umewafika Njombe ukafanya observation yako mwenyewe?
Ulitembelea huko kwa lengo la utafiti au jingine?uhalisia wa hali ya maambukizi ya ukimwi kwa njombe haupo kama tunavyotangaziwa,nimetembelea vijiji vya wilaya ya makete uhalisia haupo kama tunavyotangaziwa