Kwanini mnatupiga picha bila ridhaa yetu?

Kwanini mnatupiga picha bila ridhaa yetu?

Mmmh Yani from no where mtu akupige picha tena usiku, ukiona hivo Kuna jambo
 
Ni kinyume cha sheria kumpiga mtu picha bila ridhaa yake! Labda kama kasogea kwenye eneo binafsi la nyumba ya mtu! Lakini mtu anapita njani au barabarani makamera yanapiga picha tutakuja kuzivunja hizo camera kwa mawe ya manati!
Inakuwaje? Mbona pale mahakamani ambako ndo Sheria inasimamiwa/inatekelezwa naona Mahabusu, Mapolisi au Askari Magereza picha zinapigwa/wanapigwa na zinarushwa kwenye mitandao?
 
Unapita mtaani usiku mida ya saa2au sa4 usiku ghafla kamera inatowa mwanga mkali kumbe kamera inatupiga picha si poa. Yani tunarudi kwetumakamera yenu yanatuphotowa jamani!!!!.
Mtusamehe tu ni ajira mpya ya kisasa. You tube vlog inalazimisha kupiga picha.
Mie ni mmoja wa wapiga picha wa mitaa na watu shule japo bado sijakolea.
Waafrika tusikatae kupigwa picha hasa kama sio kwa ubaya au maeneo ya starehe. Nikiangalia picha za miaka ya 60, 70 80, 90 napata taswira jinsi maisha yalivyokuwa. Tuweke kumbu kumbu kwa vuzazi vijavyo kwa kila kitu tunachofanya
 
Back
Top Bottom