Kwanini mnawahukumu mno single mothers?

Kwanini mnawahukumu mno single mothers?

Tunaskia baba mwenye mtoto anytime akiamua kupasha kiporo hawakatai ata wakiwemo kwenye ndoa hii imekaaje
 
Kheri ya pasaka waungwana!

Ningeanza na kusema kwenye kila jambo kuna pande mbili za shillingi.

Katika pitapita zangu nyingi nimegundua kuna uzi nyingi katika jukwaa hili la MMU zinazowakandamiza na kuwaponda single mothers! Mnasahau kama hao walowatia mimba single mothers nao ni single fathers?

Nakubali katika maisha kuna kukosa na kukosoana lakini ningependa tuwekane sawa katika hili, haimaanishi kwasababu BAADHI ya single mothers hawana msimamo na vigeugeu basi wote wapo hivo.

Na kingine kama mtu ni single mum lazima uelewe kuna sababu ilopelekea hilo sidhani kama kuna mtu anaependa kulea mtoto peke yake bila ya sababu ya msingi.

Au ukiachilia mbali hilo kuna baadhi wanaoamua kulea mwenyewe kwasababu the other part is not the right father figure for their child! Naamini si kila anayeweza kumimbisha mtu anapaswa kuwa baba!

Ningependa tuwekane sawa kuwa kuna single mother wa aina nyingi:

1. Kuna wadada wengi wanaoamua kujizalia tu kwasababu hakuna wanaume wanaoeleweka ambao wanakidhi viwango vyao na umri umeshatupa mkono mtu anaona ajizalie tu apate mrithi, wa aina hii naamini wanaweza kujimudu na kuhudumia watoto wao bila msaada wa mtu na ni watu wanaojielewa.

2. Kuna walopewa mimba ambazo wawili hao walikubaliana kuzaa pamoja na wakatengana kwasababu tofauti. Hawa mara nyingi wapo mguu ndani, mguu nje kwasababu kulikuwa na mapenzi na makubaliano kati yao kwahio ni rahisi kukumbushiana

3. Kuna walobeba ujauzito kibahati mbaya na mwanaume hayupo tayari kubeba majukumu. Wanawake wa kundi hili hawatakagi mahusiano na maex zao kiujumla kwasababu wanakuwa wameumizwa vyakutosha na wakishasonga mbele wamesonga.

4. Kuna walojibebesha mimba kwa matumaini ya kuolewa au kupata mwenza wa maisha au mteremko wa maisha(hawa ni wale ambao wanazaa hata na wanaume za watu). Hawa ni kundi jingine ambalo pia ni mguu ndani, mguu nje yaani anytime anarudiwa na kuachwa madhali yake yanamuendea.

But all in all mwishoni mwa siku kuna mwanaume alihusika katika hili kwa njia moja au nyingine. Kama ni kinga wanapaswa kutumia wote kujikinga na ujauzito usotarajiwa sasa ikiwa wewe unaenda kulala na mwanamke ambaye huna future nae bila kinga yoyote(kondom au uzazi wa mpango) unategemea nini hasa?

Tusihukumu single mothers kama wakosaji ni wao tu na wanaume ndo malaika mbona hamwahukumu single fathers? Au mnataka kusema wao ni tofauti kwasababu hawajabeba ujauzito.

Mtoto siku zote ni wamama ndio maana wamama ndio wanapata jukumu la kulea lakini tukipiga tathimini ya wanaume au ambao wamezaa tu ni single fathers naamini imepiku idadi ya wanawake.

Single fathers pia wanaweza kwenda kwa ex zao na kubinjuana so hakuna tofauti ya kusema ni single mothers tu sio Wife material kwasababu mnahofia wataliwa. Then tunaweza kusema Single fathers nao sio Husband material. This goes both ways kwa jinsia zote.

La muhimu ni kujuana vyema huyo single mum/ dad kabla ya kuanzisha mahusiano naye na mahusiano alokuwa nayo na ex wake lakini sio kuhukumiana!

TUNASEMA TABIA ZAO SIO WAO
 
Wanachepuka sana ila tunawaongea wao coz wimbi la single mom limeongezeka kitaa, tunachotaka tuwarekebishe baadhi yao waliokua hawajatulia
Yamkini ongezeko la single mothers ni matokeo ya kupungua kwa matukio ya utoaji mimba. Sasa yupi bora single mother au 'mama marehemu'?

Kuwaandama single mothers tu hakutatosha kumaliza tatizo katika jamii zetu bali kuna haja ya kuwalea watoto katika maadili mema ili kudhibiti wasije wakajiingiza katika uzinzi wangali wadogo.
 
Yamkini ongezeko la single mothers ni matokeo ya kupungua kwa matukio ya utoaji mimba. Sasa yupi bora single mother au 'mama marehemu'?

Kuwaandama single mothers tu hakutatosha kumaliza tatizo katika jamii zetu bali kuna haja ya kuwalea watoto katika maadili mema ili kudhibiti wasije wakajiingiza katika uzinzi wangali wadogo.
Hatujawaandama ila tunarekebishana
 
Hilo nalo neno!
Mkuu mi nime notice kitu, hapa single mother anaesemewa ni yule wa tandale kwa mtogole au kinyantila ambae either ni mchuuzi wa kijasiriamali au yule ambae hata kitunguu kununua ni mahesabu makali..."total dependant".

Single mother wenye mapesa huwezi sikia wanapiga ndulu za namna hii. Wako sooo relaxed na hawana kinyongo na mtu.

Ni hizi chloroquine zetu kitaa ambazo hata bundle mpaka iungwe ndio zinaleta fujo dunia nzima.
 
Once a man always a man. Therefore, regarding your discourse, I hereby precisely and boldly say that WOMEN ARE DESERVED TO BE BLAMED as they are the root of all evils in the world.
 
Uliwahi kuona single mother mwenye pesa nyingi anahukumiwa?!
Mchawi pesa tu. Jamii maskini ina hukumu vibaya kila kitu.
Hao ni wangapi katika jamii yetu ukipiga mahesabu ya haraka haraka?

Hahukumiwi kwasababu anajitegemea lakini wanaoathirika na kudhurika zaidi ni watu wa kawaida na wanaotokea kwenye familia duni!
 
Hao ni wangapi katika jamii yetu ukipiga mahesabu ya haraka haraka?

Hahukumiwi kwasababu anajitegemea lakini wanaoathirika na kudhurika zaidi ni watu wa kawaida na wanaotokea kwenye familia duni!
Basi tatueni tatizo la umaskini kwanza ili msihukumiwe.
That will save you all.
 
Jamani single mothers walioajiriwa nimekoma nao, hawa wahuni utadhani majini ya kujengea ghorofa kariakoo.

Mimi hawa wadudu hapana kwa kweli shida zenu mpelekeeni waziri wa fedha.

Ni hayo tu

Wadiz
 
single mother mmoja asifanye wote wawe hawafai, wapo wengi wazuri tuu
 
Back
Top Bottom