Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kuna katabia kapo hata sijui aliyekaanzisha nani aisee, ka kuamini kila mwanamke anataka kuolewa na ndio lengo au ndoto za maisha yake.
Utakuta wanaume wanamtongoza mwanamke akikataa wanaanza kusema anaringa kwa kuwa bado umri haujaenda, ukienda ataokota yoyote aliye mbele yake ili aolewe, wakati huo jua lishazama.
Wakikataa wanakutana na maneno kama; kalenda inaenda wewe changamka, unaringa wakati una miaka 30? Unaringa hujui mwanamke anazeeka haraka! Unaringa na jua lishazama? Endelea kuringa utakosa soko wewe! Una miaka miwili tu ya kupata mtoto hapo si uolewe?!
Kwani aliyewaambia huyo mwanamke anataka kuolewa nani? Tamaa zenu tu ndio zinawafanya muwapangie wanawake wakifika umri fulani waolewe, matokeo yake pressure wanayopewa wanakubali yoyote hata wasiomtaka.
Kwa hiyo mnataka binti ajizolee yoyote ili mradi kuuwahi umri? Kwanza nani kawaambia lazima kila binti aolewe? Kwani asipoolewa ataumwa au atakufa kwa kutokuolewa? Mwacheni dada wa watu atimize malengo yake, ataolewa hata na miaka 70 kama akitaka kuolewa. Kwani hakuna wanaoolewa na miaka 80?
Acheni kuwapa pressure ya ndoa wanawake kwa kigezo cha umri, nao wana malengo na ndoto zao za kutimiza kabla ya kuingia kwenye hizo ndoa.