Kwanini mnawapangia wanawake ukomo wa umri wa kuolewa?

Kwanini mnawapangia wanawake ukomo wa umri wa kuolewa?

Kuna katabia kapo hata sijui aliyekaanzisha nani aisee, ka kuamini kila mwanamke anataka kuolewa na ndio lengo au ndoto za maisha yake.

Utakuta wanaume wanamtongoza mwanamke akikataa wanaanza kusema anaringa kwa kuwa bado umri haujaenda, ukienda ataokota yoyote aliye mbele yake ili aolewe, wakati huo jua lishazama.

Wakikataa wanakutana na maneno kama; kalenda inaenda wewe changamka, unaringa wakati una miaka 30? Unaringa hujui mwanamke anazeeka haraka! Unaringa na jua lishazama? Endelea kuringa utakosa soko wewe! Una miaka miwili tu ya kupata mtoto hapo si uolewe?!

Kwani aliyewaambia huyo mwanamke anataka kuolewa nani? Tamaa zenu tu ndio zinawafanya muwapangie wanawake wakifika umri fulani waolewe, matokeo yake pressure wanayopewa wanakubali yoyote hata wasiomtaka.

Kwa hiyo mnataka binti ajizolee yoyote ili mradi kuuwahi umri? Kwanza nani kawaambia lazima kila binti aolewe? Kwani asipoolewa ataumwa au atakufa kwa kutokuolewa? Mwacheni dada wa watu atimize malengo yake, ataolewa hata na miaka 70 kama akitaka kuolewa. Kwani hakuna wanaoolewa na miaka 80?

Acheni kuwapa pressure ya ndoa wanawake kwa kigezo cha umri, nao wana malengo na ndoto zao za kutimiza kabla ya kuingia kwenye hizo ndoa.
Kwa hiyo hamtaki ndoa....this is gud news
 
Ata 100 wee subiri mr ryt apatikane. Kwanza kwani kuolewa kuna muhimu gani? Sii mna malengo yenu ebu yatimizeni kwanza kama alivyosema mleda mada
Malengo gani mm Nina 35 na sinachochote hata kiwanja nipo nipo tu
 
Kuoa na kuolewa kuna muda maalumu asikwambie mtu, jamii iliyostarabika inaoa na kuolewa kwenye early 20's sasa uoe au uolewe na miaka 40 uzae mtoto aje kufikia umri wako wa miaka 40 ww utakuwa na miaka mingapi? Hata wanawake wanahauriwa kuzaa mapema kipindi mayai yakiwa na rutuba ndo utapata watoto wenye akili, sasa unazaa na miaka 45 utatoa mtoto zezeta na asifundishika!

Wanasaikolojia wote wamegawa vipindi vya makuzi ya binadamu kuanzia tumboni mpaka kuzaliwa hadi kufa na kila stage ina mambo yake , ukivuka stage moja utaathiri stage nyingine kipindi cha miaka 30- 45 kila binadamu anatarajia kuwa tayari ana familia sasa familia uipate kwa miaka 70??
Kwa hiyo tuliozaliwa wazazi wako kwenye 40s ni mazezeta dogo heshima kitu cha bure

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
mwanamme kwa asili ni mbinafsi, dikteta na kandamizi. Ili hayo yafanikiwe sasa hutumia strategy ya kumfanya mwanamke ajione asiyefaa kabisa, asiyestahili upendo huruma wala heshima, njia mojawapo ni kumsakama mwanamke sababu ya umri wake kumfanya awe vulnerable kwa mwanamme na hii itamfamya apatikane bila usumbufu kwa mwanamme.
Hii sio kweli. Umeongea kwa msukumo wa fikra chuki na haujalenga uhalisia.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
mwanamme kwa asili ni mbinafsi, dikteta na kandamizi. Ili hayo yafanikiwe sasa hutumia strategy ya kumfanya mwanamke ajione asiyefaa kabisa, asiyestahili upendo huruma wala heshima, njia mojawapo ni kumsakama mwanamke sababu ya umri wake kumfanya awe vulnerable kwa mwanamme na hii itamfamya apatikane bila usumbufu kwa mwanamme.
Uko sahihi kabisaaa mimi nina miaka 29 saivi na wala sina pressure ya ndoa wala mtoto, walionizunguka wanaongea sana ila huwa nawaambia tumetofautiana ww kama kipaumbele chako mtoto zaa kama ndoa subiri uolewe.
Ila mimi nilishasemaga na moyo wangu kwamba ndoa au mtoto ni option na mindset za watu ukishafika umri fulani au ukishapata pesa kinachofuata ni ndoa au mtoto nani kasema?? Mmekarr.
 
Heshima ya mwanamke ni kuolewa kuwa mke na kuwa mama tena ndani ya ndoa iliyo hai tofauti na hapo mwanamke hana thamani.

Hivyo ilikulinda heshima yake mwanamke ni vyema mwanamke akaolewa pale anapo vunja uongo na siyo vinginevyo Wenye akili wamenielewa
 
Imagine. Ukomo uko kwenye fikra zako mwanamke.
JamiiForums1005092546.jpg
 
Back
Top Bottom