Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Kama naanza kusikia kijiharufu fulani
Mkuu hizi ni sanaa. Hivi MO hamjamjua mpaka sasa? Jamaa ni msanii mzuri sana kwenye kutafuta fedha. Kuna kitu kinapangwa hapa. Hivi mhindi ni mtu wa kuomba serikali kama anataka kufunga biashara yake? Watu wanaandaa mazingira ya kufanya kupiga fedha ndefu sana hapa. Hii awamu ndiyo itakuwa mama wa ufisadi na mafisadi wataibuka kila kona.
 


Tunapenda sana kujisahaulisha juzi tu wawakilishi wetu wa Tanzania wame sign kuleta chai kutoka Kenya! leo hii tunahitaji maongezi!
 


 
Kwa vile hujui alinunua viwanda vingapi akaviunganisha kwenye bishara zilziokuwa za baba yake. Unasamehewa!

Huelewi viwanda vilivyokuwa vinaitwa Polytex, Magunia, National Milling na vinginevyo vidgo vidgo viliishia
Kuwa na mwekazaji kama dewji ni hasara kubwa kwa taifa ni mjanja mjanja mjanja sana
 
Kwa hiyo mtu anaweza kulazimishwa kuendesha viwanda hata kama yeye anataka kufunga viwanda vyake?
Inawezekana kabisa haswa Biashara kubwa inayoguswa uchumi wa wananchi wengi
Wanaweza kumzuia kwa muda Fulani serikali ikitafuta njia nzuri ya kuhandle hasara ya wananchi wake

Unadhani kwanini alitoa ombi rasmi la kufunga kiwanda chake
Kwanini asingefunga tu bila taarifa

Hata kampuni kufunga Ina mchakato mrefu Sana INGAwa ni ya kwako mwenyewe
 
Katika muktadha huu, wote.

Huyu Mo anatafuta njia apendelewe.

Bashe naye ni mjanja, anatafuta nguvu ya Umma.

Mitafaruku hii, sikuwahi kusikia wakati Reginald Mengi akiwa katika nafasi ambayo MO yumo sasahivi.

Ana nyodo.
Mkuu,

Mbona Mengi naye kashatafuta kupendelewa mpaka rais Mwinyi kampa eneo prime la real estate katikati ya mji wa Dar?

Inawezekana kabisa Mo anafanya mbinu za kibiashara ili apendelewe, hili jambo ningependa lifanyiwe uhakiki zaidi ili tusiweke speculations zaidi ya facts.

Lakini, mbona tunataka kumpaisha sana Mengi, Mengi alifanya hayo yote, tena vibaya sana mpaka kukwepa kodi na kuwacheleweshea eafanyakazi wake mishahara kwa faida zake za kibiashara.

Mbona tunamuwekea hagiography Mengi wakati watu tunajua mengi kumhusu Mengi?
 
Kwangu mimi hii habari ni alama ya inefficiency katika uchumi. Kwenye habari, kutangaza fursa, kwenye mifumo ya kodi, kwenye falsafa, corruption, kuna sehemu kuna inefficiency kubwa.

Otherwise hata kwenye supposedly quasi-free market yetu, ilitakiwa Mo aweze kusema sitaki biashara hii naiuza, na watu wa kuinunua wawepo wengi. Wa nje na ndani.

Na kama serikali inahofia wananchi kukosa kazi, kukosa soko etc, hata kwenye mfumo wa serikali ku support critical industries, local production, basic justifiable protectionism etc, tulitakiwa tuweze kuwa na wafanyabiashara kadhaa wakubwa wa ku step in anapokataa Mo, au hata kuwezesha hao wananchi kuwa na co-ops.

Naona kama tunatengeneza a few oligarchs ambao wanakuwa "too big to fail", halafu, wananunua viwanda kutoka serikalini on the cheap, wakitengeneza faida inakuwa yao, wakipata hasara wanapata bailout/tax breaks/ wanabembelezwa etc, na pengine hawakutaka hata kufanya biashara, walitaka kutumia viwanda na mashamba kama collateral na kama njia za kupata subsidies.

Mo naona kama anachanganya on one hand oligarchs wa Russia walivyofanya baada ya USSR kusambaratika na mashirika ya umma kuuzwa on the cheap, na on another hand, wakulima wakubwa wa Marekani wanavyotumia ardhi na viwanda kama strategy ya kupata subsidies za serikali na collateral ya mikopo.

Ikiwa niko sahihi, kumbembeleza mtu kama huyo ni hatari. He is just gamind the system. Hana nia ya kufanya hiyo biashara.

Mtambembeleza leo na kumpa bailout, kesho atawafanyia sabotage kufunga biashara kwa njia ambayo hamuwezi kumlaumu.

Anaishia kula pesa zenu na biashara anafunga vile vile.
 
Ohoòooo
 
Ni mfumo wa kishenzi sana , kote huko ilipofanyika hii kitu imeishia kutengeneza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na kutajirisha mabwanyenye wachache ambao wanahodhi uchumi na kuongeza wealth gap Kati ya wasio nacho na wenye nacho
 
Biashara za ndani zicompete kwenye fair ground na ziruhusiwe kufail , kuwe na competition ya kutosha kwenye uzalishaji humu ndani na ndio tija itaonekana
 
Hicho kiwanda Mo hajajenga ni vile viwanda vya Enzi za mwalimu ambavyo watu waligawana kijanja Janja. TANGU wachukue hivyo viwanda hawajwahi Fanya ukarabati, wala kununua mashine zaidi ya kutumia zile zile za TANGU ya Enzi za mwalimu. Niliwahi tembele kiwanda cha chai pale Tanga, huwezi amini mpaka nyasi zinaota darini. Mitambo na majengo Yale Yale TANGU Enzi zile za mkoloni. Yaani ni aibu Kwa kweli. Hayo mashamba yenyewe haijawahi panda chai mpya anachuma Ile Ile ya TANGU Enzi za mwalimu. Hawa Wahindi hawa ninmufilisi Kwa kweli. Anajua sasa hv Hana la kupoteza ataakiamua kukifunga maana ameshachuma vya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…