Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Bashe naye anaropoka tu , MO Dewji mbona alifunga hata kiwanda cha katani mwaka 2022 ?
Kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wa biashara ,kodi na uchumi wa hii nchi .
Sasa hili Taifa lililojaa mbumbumbu ,watu wataamini hayo maneno ya Bashe ya kisiasa ili kupumbaza watu , unaweza mlazimisha mfanyabiashara asifunge kiwanda au biashara ?
Hizo gharama za uendeshaji utampa wewe ?
 
Sababu ni ajira alizozitengeneza lakini pia mapato Kwa maana ya Kodi.
Hata hivyo inaweza kuwa ni sindicate ya kuongeza bei ya bidhaa kwa visingizio vya mwenye kiwanda.
Kwani Mo Dewji ana monopoly ya kutoa ajira na kulipa kodi Tanzania?

Hakuna mfanyabiashara mwingine yeyote anayeweza kutia ajira na kulipa kodi Tanzania Mo Dewji akifunga kiwanda?
 
Sio Financial tu Serikali inaweza kuvipunguzia Ushindani kwa kuvilinda na Bidhaa zilizoruzukiwa kutokea Nje kwa mfano Chai kutoka Kenya na Uganda inayoingia kiholela kwa njia za Panya kuongeza Kodi kwenye Chai inayotoka nje nk.
Kwa faida ya nani ?!!!! Kumbuka hivi viwanda ni vya watu Binafsi wala sio vya UMMA..., Na katika karne ya Teknolojia na Automation hata ajira zinazotolewa na hivi viwanda sio kubwa kivile (leaves a lot to be desired) Sasa ponea ya mwananchi angalau ushindani ukitoka nje na bei itashuka as well as quality (kutolazimishana kula makapi)...

By the way kama hawa ni enterpreneurs ma-gurus kwanini na wenyewe wasiuze nje kwenye soko ? Ukweli ni kwamba half measures never work..., inabidi tuelewe tunataka kwenda wapi Kama ni Soko Huria liwe Huria kweli sio Kutetea / viwanda vya ndani (which are non existent)..., wote waingie uwanjani kupambana na sisi kama walaji tuta-pick and choose
 
Duuuuh !
 
Watu hawaangalii maslahi ya nchi, wapo kwaajili ya personal gains, vinginevyo hii isingetokea katu hata siku Moja kuacha watu wachache wamiliki uchumi wa nchi
Ndio uchumi wa kibepari unavyofanya kazi hivyo , buncruptcy ni sehemu ya maisha kwenye uchumi wa kibepari , biashara zinazaliwa ,zinakuwa ,zinauzwa na kufa au kufirisika .
Huwezi kuzuia mfanyabiashara kufunga biashara , kwanza kampuni za MO Dewji ni sorely owned private companies na si public traded companies kama za Marekani kule ,ambapo watu wengi wanamiliki share za kampuni , mfano General Electric , United steel nk
 
Watu hawaangalii maslahi ya nchi, wapo kwaajili ya personal gains, vinginevyo hii isingetokea katu hata siku Moja kuacha watu wachache wamiliki uchumi wa nchi
Biashara sio charity ,biashara ipo ili kuzalisha faida , kama haiingizi faida ,hiyo biashara ni resources waster ( zombie company ) , na katika uchumi wa kibepari haitakiwi hii
 
Viwanda vingi vya chai mufindi na njombe kama vimejifia tuu. Wafanyakazi wanahari mbaya kupita maelezo
 
Bashe naye anaropoka tu , MO Dewji mbona alifunga hata kiwanda cha katani mwaka 2022 ?
Kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wa biashara ,kodi na uchumi wa hii nchi .
Naam sio kitu ni vitu havipo sawa ila huenda kosa la kwanza kufanya ni kubinafsisha hata katani zote willy-nilly bila kuangali future
Sasa hili Taifa lililojaa mbumbumbu ,watu wataamini hayo maneno ya Bashe ya kisiasa ili kupumbaza watu , unaweza mlazimisha mfanyabiashara asifunge kiwanda au biashara ?
Hapana wala kulazimishana ni zaidi ya udikteta sio Haki kabisa kama rahisi fanya wewe...., kwahio hapa hatalazimishwa bali atabembelezwa
Hizo gharama za uendeshaji utampa wewe ?
Naam Kodi yako wewe Mwananchi ndio utalipa through ruzuku atakazopewa
 
Umeme wenyewe huu wa kuunga na manati kwa nini viwanda visife , yaani nchi ya kipumbavu sana hii .
Mnataka kukuza sekta ya viwanda na biashara na hamjui umuhimu wa vitu critical kama nishati ya umeme kwenye hiyo sekta ?
Unawezaje kukuza sekta komavu ya viwanda na uzalishaji bila miundombinu imara na huduma za kuaminika katika nishati ?
 
Big Players wa Chai kwa Bongo ni wazungu wa Uniliver nao nasikia waliuza biashara zao sijui nani alitake over
Hii nchi ni mbovu sana kwenye uongozi na mfumo wa biashara .
Kama multinational corporation companies kama hao Unilever wameondoka Bongo tayari ,basi hii itoshe kuwapa watu picha jinsi hali ilivyo mbaya nchi hii kwenye biashara na uwekezaji
 
👊👍🙏🏼asante kwa Madini.
 


"lazima waendeele na uzalishaji hilo ni la lazima kisha tutakaa chini kujadiliana mambo mengine”

Wafanya biashara huwa tunakimbilia fursa, na kukimbia hasara /uwekezaji usio na tija au matarajio. Swala la lazima hiyo siyo Kanisa inayotoa huduma, waziri makelele kafeli.
 
Ni kawaida ya Mo kususa ili abembelezwe, kulanina zake kwanza chai ina faida gani kiafya?
 
Exactly , na ndicho nilichokuwa nasema ,hata huko Marekani watu wanaongelea ile kitu inaitwa " bailout packages " au ruzuku Kwa makampuni mfano kama ile ambayo ilitolewa 2008 kipindi cha kuyumba kwa uchumi wa dunia na Masoko ya mitaji na hisa au ile ya 2020 kipindi cha covid ,ile atleast inaleta mantiki lakini ,kiuhalisia mfumo wa kibepari ni kwamba serikali haipaswi kutoa pesa na kutapanya kuokoa makampuni binafsi na biashara binafsi ,maana huo ni mzigo kwa walipa kodi ,maana itarudi kumuumiza mwananchi kwenye makato ya kodi ambayo huwa inaambatana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma ,na makato ya mapato na mishahara
 
Biashara sio charity ,biashara ipo ili kuzalisha faida , kama haiingizi faida ,hiyo biashara ni resources waster ( zombie company ) , na katika uchumi wa kibepari haitakiwi hii
Je faida ni nini ni monetary pekee ? Kwa private company jibu ni ndo kwa jamii na state pia welfare ya community ni faida zaidi hata kama una-break even pekee... Na howmuch faida is faida (kwa Private company ni as much as possible) ila kwa state / jamii huenda faida ikahesabika zaidi kwa wellness ya wafanyakazi na wakulima....

Now that being the case huenda baadhi ya thinking ya kugawa hivi viwanda na other crown jewels tunazopanga kuzigawa huenda the results wont be as expected.....

 
Uchumi wa kibepari umejengwa kwenye filosofia ya competition , watu washindane kwenye soko na ukipigwa za uso ukae pembeni waachie wababe
 
Mohammed Dewji anataka kuwanyonya wakulima.

Kuna jamaa yangu kutoka nchi fulani iliyoendelea (kiufupi nahisi ni jasusi) alikuja kufanyakazi METL kwa miaka kadhaa. Ameondoka nchini na full picture ya Mo Dewji dhidi ya mifumo ya uchumi wa Tanzania. Pia hata ukaguzi wa mali inayoenda kwa walaji hufanyika in favor kwa sababu ya uduni wa viwango vya uzalishaji....

Hawa matajiri, wanaonekana kwenye Forbes kama leading moguls lakini ukija kwenye eneo la kulipa kodi hayupo kwenye top margins.

Mengine siandiki kwa sababu mfumo wanajua mengi sana na sijui ukimya wao kama ni tafsiri ya wanufaika wenza
 
Kazi ya serikali inatakiwa kuweka mazingira ya biashara kuwa sawa kwa wawekezaji na wafanyabiashara na hii na maanisha kuondoa ukiritimba ,rushwa na kulinda haki zao na mali zao na kujenga miundo mbinu kama mifumo ya nishati , usafirishaji na maji na kuhakikisha hizo huduma ni reliable na zinatolewa kwa ufanisi na bei cheap ili wawekezaji na wafanyabiashara wapige kazi zao kwa uhakika na bila vikwazo (kutengeneza fair platform Kwa kila muwekezaji kuwa huru kucompete ) .
Serikali zenye akili zinawekeza huko na si kulamba makalio ya watu ili kuficha failure na uozo wa kiutendaji kama huo ,
Wanachofanya akina Bashe ni kuficha aibu na failure ya utendaji wa serikali na taasisi zake
 
Kwa faida ya Ajira za Watanzania Viwanda vya Ndani ni lazima Vilindwe.
Nadhani ungenisoma tangia mwanzo nimekwambia hizo ajira zenyewe ni ngapi ?!! Au haukuona hilo swali ?

Ni kwamba ajira ni chache.....;
Product ikiwa chache bei inakuwa juu (watanzania wanalipia through bei) / Refer Sukari
Quality Mbovu (watanzania wanalipia)
Kuita wafanyabiashara mezani ili wafidie hasara yao (watanzania wanalipia)

Sasa niambia kwenye hio equation kama mwananchi hapati Raw Deal either way.... Nadhani ungekuwa na argument ya (Protectionism) kama kweli viwanda hivi vingekuwa vya UMMA (yaani wananchi wana stake)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…