Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Ukienda kuwauliza raia wa kawaida pale Marekani hii kitu "Bailout" hawaipendi na hawataki kuisikia , na ni kwasababu wanajua mwisho wa siku anayefaidika si raia wa kawaida ,ni sawa na kumkamua masikini ili kumfaidisha tajiri ,kitu ambacho si sustainable kwenye uchumi na kinazalisha mentality ya uzembe na kuua ubunifu ,maana huyo anayepewa Bailout kila siku atakuwa anatapanya resources ovyo ovyo na kuongoza biashara ovyo akijua kuna kodi za wananchi zitatumika kuja kuokoa biashara yake akikwama .
Mo aachwe afanye maamuzi anayoona yanafaa
 
Kwani MO hicho kiwanda cha chai alijenga yeye ? Na mashamba je ?? vyote alinunua bei chee toka serikanli wakati wa ubinafsishaji wa serikali ya awamu ya tatu.Arudishe serikalini wala asimtishe mtu !!
 
Kwangu Bailout ni mentality ya kijamaa na kijima na haifai kwa ulimwengu huu wa competition na utandawazi na mifumo ya kipebari
 
Duuuuuu
 
Upunguani,Bashe ndio Huwa anampa pesa za Kuendesha kiwanda?

Kama anapata hasara Kwa nini asifunge?
 
Mimi chuo hata sijasoma uchumi , Ila basic commerce studies za olevel tu zilinipa ideas kamili za jinsi economic wheel inavyofanya kazi , cha kushangaza kuna wapumbavu wameajiriwa humo kwenye wizara za viwanda , biashara na uchumi ili kufanya analysis na kutoa maamuzi ya vitu kama hivi ila ni vululu vululu .
Hii nchi ni failure kabisa ,na mpaka siku tutakapotatua tatizo Tulilo nalo ndio tutaanza kuona mwanga , ni aibu kila kitu mpaka Rais ahusishwe .
Yaani ni kama kwamba hao maamuma waliajiriwa kama mawaziri na watendaji wengine humo kwenye wizara na taasisi hawana akili timamu ya kutengeneza mifumo imara ya utendaji na kufanya implementations na kuhakikisha uchumi wa hii nchi unathrive , ni aibu kabisa
 
Utasikia jitu linasema " tunamwomba rais aingilie kati "
Hii ni indicator ya taifa la wafu ,hili taifa la wafu
 
Duh , mlolongo wa ukiritimba balaa
 
Kulinda ajira hata 3 ni Jambo jema.
At what cost ? Kulinda ajira za Makuli sita kwa kusababisha walaji milioni kadhaa kulipia bidhaa hafifu kwa gharama ya juu ?

Tunasema serikali isiingilie (kutokuwa na viwanda vya UMMA - vyote tubinafishe) alafu tunaowapa hatuishii hapo tunakikishe hawapati competition kwa kuzuia bidhaa nyingine..., Unaona hii ina-make sense ?

Kwanini hao private wasilete vya kwao na jamii / UMMA na yenyewe iwe na vya kwao hususan kwenye hizi Cash Crops...
 
Kwani MO hicho kiwanda cha chai alijenga yeye ? Na mashamba je ?? vyote alinunua bei chee toka serikanli wakati wa ubinafsishaji wa serikali ya awamu ya tatu.Arudishe serikalini wala asimtishe mtu !!
"Arudishe serikalini" maana yake nini?

Auze viwanda serikalini? Kwa bei gani? Serikali itakubali kununua kwa bei atakayoitaka baada ya yeye kukaa navyo kwa muda wote huu?

Serikali imeuza viwanda kwa kujitoa kwenye biashara, Mo arudishe viwanda serikalini ili iweje? Serikali irudi kwenye biashara?

Ikiwa serikali ilijitoa kwenye biashara mpaka kuuza viwanda, Kwa nini unataka Mo arudishe viwanda serikalini, asiviuze kwa wafanyabiashara wengine?
 
Huenda pamoja na kuwa na wataalamu wa uchumi na biashara kwenye hizo wizara ,Bongo zao hazijajua campetative advantage tuliyonao kama taifa ( yaani sisi ni mabingwa wa kuzalisha nini kwa ufanisi na bei cheap ambacho kinaweza kuliwa na mataifa mengine na mwisho wa siku kuleta faida na tija kwa mwananchi na taifa kwa ujumla ) , hapo ndipo tulipo kwama .
Tunakimbilia viwanda ,wakati wizara zetu na taasisi ni so poor kwenye kudeliver utendaji na kuhudumia miundombinu , na miundombinu yenyewe au kodi na mazingira ya biashara ni so poor .
Tunatakiwa tujiulize maswali magumu kama taifa na tufanye maamuzi
 
Mengi hakuwahi kuwaweka Watanzania-wakulima-Rehani. Nipo tayari kusahihishwa

Ni hivyo tu.
Mfanyabiashara yupo answerable kwa shareholder wake (profit) ndio alpha na omega... hio sio charity wala sio kazi yake kuangalia Welfare ya wakulima Hio sio kazi yake ni kazi ya watumishi wetu na watunga sera tunaowalipa (serikali)

Tukirudi kwa Mengi zunguka kwenye Media zake na pengine ni wangapi wanadai mishahara (sio kwamba nalaumu Kampuni sio Mengi hivyo kama Kampuni haizalishi sitegemei Mengi atoe pocket money yake kufidia biashara) i.e. Throwing Good Money after Bad...
 
Ndo maana tunasema kuwa CCM ikae pembeni waje wanasiasa wenye moyo wa kuikwamua nchi. Kuna mengi sana yanayosababisha CCM ing'ang'anie madarakani ikiwemo namna inavyowekeza indirectly kwa hawa mnaowaona ni matajiri wa kutisha leo.

Unakumbuka issue ya Deep Green na ile kampuni ya Uwakili?

Tanzania ni zaidi ya CCM na mamlaka zote za nchi. Tanzania ni watu na Katiba bora
 
Subiri utaona jibu
 
Na hapo mtamsingizia Magufuli? Na Bado mengi yanakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…