Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Mimi ni mmoja wa watu ninaokubali kabisa kuwa Manara alikuwa 'very unprofessional' mara nyingi sana. Na hata hiyo nafasi nimewahi Shauri Sana atolewe ..yeye na Jerry Muro niliwahi shauri watolewe wote huko nyuma.

Naweza sema Mimi sio mshabiki wa Manara lakini baada ya hili sakata. Nimegundua kitu kwa watu aina ya Manara...
Pascal Mayalla huwa anasema watu aina ya Manara 'wana hidden power'..

Hiki ndo nimekiona kwa Manara na naamini Mo hataweza kabisa kumzima Manara. Ukimtazama Manara anapoongea na historia yake yote utagundua kitu kimoja.

'passion'
Huoni 'Proffesionalism'..
Huoni 'ethics'
Huoni 'unafiki wala woga'
Manara siku zote amekuwa Manara
Anaishi kwa sheria zake ..lakini most important ana enjoy ushabiki wake..

Wanaosema nafasi ile inahitaji mtu more Proffesional wako sahihi lakin wanasahu kitu kimoja Tu..je mangapi hatuyafanyi ki Proffesional?
Wananchi watazoea hiyo Proffesionalism inayozungumzwa?
Utamaduni wetu na timu zetu za Kariakoo
Unaruhusu 'Proffesionalism' hiyo?

Au tunasahau na mashabiki wetu na mpira wetu watu kama Manara ndo haswaa wanazalishwa na kupendwa zaidi..?Pengo la Manara likijitokeza tutawapa nini mashabiki?

Manara alikuwa shabiki mkuu wa Simba zaidi kuliko mfanyakazi wa Simba.

Alikuwa maarufu kuliko yeyote Simba.

Hakupata hiyo kazi kwa kuomba.

Aliombwa.

Why watu wamtarajie aje a behave kama muajiriwa mwingine?

Bado atabaki shabiki mkuu wa Simba kuliko Mo hata kama hana title official hapo Simba.

Watu wenye passion na wako genuine bila kujali risks za kuwa open na genuine na wanayo ongea mara zote hushinda vita.

Manara ukimsikiliza anapoongea utaona.

Anaongea kama mshabiki na sio kama muajiriwa hajali lolote mradi anausikiliza moyo wake..Mo hatamuweza Manara..
 
Tukubali Manara kuna level alishafika huwezi kummaliza kirahisirahisi bila kupasua club. Kudeal na mtu kama Manara ni rahisi sana ila si kwa kumuundia skendo mbuzi.

Kitakachotokea ni kuvurugana na kutoaminiana na hapo mwisho wake ni MO kujitoa.

Kwa ufupi bila suluhu Simba haitobakia kama ilivyokuwa maana MO mwenyewe hana ngozi ngumu! Kama viongozi wa Simba wangeweza kufocus kwenye malengo yao na kuachana na kelele za Manara tungetoboa lakini sio hilo likitokea zaidi ya malumbano ambayo Haji atashinda tu.
 
Kuna mambo nayafikiria, yananifanya nisiamini kuwa Manara amekosea ktk hili sakata.

Je ile tume sijui shirikisho la ushindani wa kimasoko/hisa lilikosea kuhoji uwekezaji wa Mo? Walikosea kuuliza Mo amekuwaje Mwenyekiti wa Simba? Yote yale waliyozungumza walikosea?

Tuachane na ile tume, vipi kuhusu Kigwangala? Aliwahi kuhoji mengi mno kuhusu uwekezaji wa Mo Simba.

Twende mbele turudi nyuma, tuweke shahada zetu na stashahada zetu mifukoni, tujadili hili. Simba imeperfom vyema michuano ya kimataifa na ndani pia. Ni kweli Simba imeendeshwa kwa hasara?

Yanga ambayo haina makombe, haijacheza michuano ya nje n.k imeweza tengeneza faida, sembuse Simba ambayo inapeak sana muda huu kuliko timu yoyote East Afrika?

Wakuu embu tuwekeni ushabiki pembeni na tuwe wawazi na wakweli ktk hili.
 
Nimeshangaa Sana Manara ana nguvu Sana Ila itabidi azoee
 
IMG_3981.jpg
 
Back
Top Bottom