Kwanini Mpiga Solo Gitaa hatari Nene Tchacou hakuimbwa sana kama Wenzake Diblo Dibala na Dally Kimoko?

Kwanini Mpiga Solo Gitaa hatari Nene Tchacou hakuimbwa sana kama Wenzake Diblo Dibala na Dally Kimoko?

Binafsi namuona ni soloist bora baada ya Dally Kimoko “King” hapa duniani na hususani kwenye Congolese music scene!!

Haikuwa na haja ya kuimbwa au kutajwa kwenye nyimbo alizohusika maana alipopewa jina la Tchakou yaani “kasuku” sababu gitaa lake liliongea lenyewe[emoji4]. Kitu cha ziada alichowazidi Dally na Diblo ni uwezo wa kupiga gitaa zote 3 kwa ufasaha wa hali ya juu. Pia alikuwa ni music arranger bora sana, jaribu kusikiza wimbo wa Massapa wa Alain Kounkou utajua uwezo wake hasa namna aliyopangilia rhythm ya nyimbo nzima.

Watu waliomtaja sana kwenye tungo mbalimbali alizoshiriki ni msanii mwenye vipaji vingi kuliko wote ndani ya Soukous Stars namuongelea “SHIMITA EL DIEGO” na atalaku / animator bora zaidi katika Congolese music scene yaani “3615 Code Niawu” au “Cherry Niawu” au “Papa na Renzo”[emoji23]

RIP NENE TCHAKOU “Papa na Melody”.

GENTA hebu sikiliza solo ya Muchana.

Masahihisho: Kwenye Bazo solo guitar lilipigwa na Dally Kimoko.
Samahani, kwenye wimbo wa Billi wa Kanda Bongo Man nani atalaku mule!?
 
Yule Aliyecharaza Gitaa kwenye Wimbo wa Biliii ni Hatari sana Sijui ni Nani?
 
Yule Mwamba Anajua kucharaza Gitaa Aissseeee Hapa nipo zangu nasikiliza Ile Na Muchana Aaaii Lemisile🔥🔥
Hakuna mpiga gitaa aliyeshiriki nyimbo nyingi na kuitendea haki style ya soukous kumzidi Nene Tchakou, jamaa gitaa lake ni la kipeke yake wala staili yake hafananii na wapiga gitaa wengine. Alain kounkou, Damien Aziwa, Yondo Sister, Bongo Man Ngouma Lokito, 3615 Code Niawu, Nene Tuty, Aurlus Mabele, n.k kuna mikono.
Kwenye upande wa soukous Nene tchakou ni mkali zaidi ya wote, kwenye upande wa sebene Diblo dibala ni habari nyingine kwangu ndio mpiga gitaa bora zaidi.
 
Back
Top Bottom