Kwanini msemaji wa Club ya Simba anatangaza bidhaa za pinzani kibiashara? Inawezekana vipi?

Kwanini msemaji wa Club ya Simba anatangaza bidhaa za pinzani kibiashara? Inawezekana vipi?

Kuna kitu sijakielewa na hiki ni vigumu sana kukiona kwenye nchi zilizo endelea hass Ulaya huko.

Haji Manara ni Msemajo wa Club ya Simba na Mdhamini au mmiliki wa Club no Mo,
Mo ana boadhara zake nyingi sana, ana maji, ana aina mbalimbali za vinywaji, ana unga wa ngano kwa kifupi ana product nyingi sana na ziko hadi kwenye jesi za timu.

Ila hii ya Manara kutangaza product za Azam sielewi inawezekana vipi, how come anaye jua anisaidie kwamba inawezekana vipi? Na product anazo tangaza no the same na zonazo zalishwa na Bosi wake.

Kwa wenzetu hiki hakiwezekano Milele.View attachment 1664410
Haji Manara amefanya alivyoweaza Kuinadi Simba SC ila kwa ninayoyasikia dhidi yake Yeye, Mo Dewji na CEO Gonzalez aachane tu na Simba SC.
 
Wewe ndo unaona ni tatizo lakini mwajiri wake hajaona hilo tatizo kwa sababu wanajua hakuna tatizo!!! Hivi kwa ufahamu wako, leo hii Mo Dewji amiliki TV Stations unaamini hatatangaza bidhaa za Yanga?! Au unataka kusema Azam TV hawawezi kutangaza bidhaa za Simba?!
Brand
 
Unamaanisha yanga inaweza ikakodi frem pale msimbazi jengo la simba na kuweka duka la jezi na vifaa vya michezo vya yanga?
Sababu tu ,,,frem zinapangishwa,,,?
Kwakuwa biashara haichaguwi wa kufanya nae?

Kwa anachokifanya manara,,tumeshafahamu matokeo ya kiporo cha ligi,,baina ya simba na Azam..
 
Hivi muheshimiwa mbowe anaweza kutangaza kofia na mashati ya ccm ?
Halafu ikajengwa hoja ya kumtenganisha mbowe na chadema?

Kwanini watanzania tunakubali kufanywa wapuuzi kwa hoja za kipuuzi?

Hivi manara popote pale utamtambulisha kama msemaji wa simba,,?
Au utamtambulisha kama nani?

Hapo mwambieni kakosea,,,angeweza kutangaza zingine na sio brand za watu ambao wapo kwenye ligi moja.

Kumbuka azam pia ni brand.
Kwanza, tofautisheni kati ya Kampuni ya Azam na Azam FC!! Pili, tofautisheni kati ya Simba FC na Mohamed Enterprises. Tatu, kwa mfano wa Mbowe ungeuliza "Ina maana Mbowe hawezi kutangaza bidhaa za Magufuli Engineering Company Ltd" assuming Magu angekuwa na hiyo kampuni?! Nne, nijibuni swali langu kwamba: Ina maana Azam TV haiwezi kutangaza bidhaa za Simba?!
 
We jamaa acha hayo mambo...Manara hana kosa lolote sio kazi yake kutangaza bidhaa za Mo.
Umezingua, hata kama ni account binafsi,
Huyu anafaa kufukuzwa kazi anahihujumu timu,
 
Unamaanisha yanga inaweza ikakodi frem pale msimbazi jengo la simba na kuweka duka la jezi na vifaa vya michezo vya yanga?
Sababu tu ,,,frem zinapangishwa,,,?
Kwakuwa biashara haichaguwi wa kufanya nae?

Kwa anachokifanya manara,,tumeshafahamu matokeo ya kiporo cha ligi,,baina ya simba na Azam..
Unachohoji ni: Yanga SC vs Simba SC, wakati mada ni Haji Manara (sio Simba) vs Azam Ltd (sio Azam FC)
 
Jibu swali langu kuhusu Azam TV!!
Atatangaza Yanga lakini si mfanyakazi wa timu au mtu anaisemea football club, atakuwa ni mtu mwingine ambae anamkataba wa kutangaza hilo Tangazo la Yanga
 
Utakauka koo broo bure.... Hawa hawaelewi
Dah! Kweli ndugu yangu, manake watu ni full kuchanganya madesa! Wanashindwa hata kutofautisha kati ya Azam na Azam FC! Ajabu nawauliza ikiwa Azam TV hawawezi kutangaza bidhaa za Simba SC, hili swali wanalikwepa!!!!
 
We jamaa acha hayo mambo...Manara hana kosa lolote sio kazi yake kutangaza bidhaa za Mo.
Lakini yeye ni brand ya Simba , Jina Azam linaleta ukakasi anapolitaja mtu ambae ni msemaji wa Simba, haya mambo ndo yameiua Toto ya mwanza. Tabia ya kuvaa ngozi mbili
 
Atatangaza Yanga lakini si mfanyakazi wa timu au mtu anaisemea football club, atakuwa ni mtu mwingine ambae anamkataba wa kutangaza hilo Tangazo la Yanga
Nimekuuliza "ina maana Azam TV hawawezi kutangaza bidhaa za Simba?" Sasa habari za mara Yanga, mara mfanyakazi zinatoka wapi?
 
Kwanza, tofautisheni kati ya Kampuni ya Azam na Azam FC!! Pili, tofautisheni kati ya Simba FC na Mohamed Enterprises. Tatu, kwa mfano wa Mbowe ungeuliza "Ina maana Mbowe hawezi kutangaza bidhaa za Magufuli Engineering Company Ltd" assuming Magu angekuwa na hiyo kampuni?! Nne, nijibuni swali langu kwamba: Ina maana Azam TV haiwezi kutangaza bidhaa za Simba?!
Nijibu hoja yangu ya kufunguwa frem pale jangwani na kuuza jezi za na vifaa vya simba,

Au kufunguwa frem pale msimbazi club ya simba na kuuza jezi na vifaa vya yanga..

Hebu tetea hoja yako hapo.

Jamaa mwambieni kateleza na atakosa sifa za kuaminika kama msemaji..

Ngoja tuendelee kuchochea kuni..

Aridhike na anachokipata kwa muajiri wake simba sports club na sio mo dewj,,

Kama ni kuoa wote tumeoa lakini hatujafikia kupagawa na njaa kiasi hicho.
 
Lakini yeye ni brand ya Simba , Jina Azam linaleta ukakasi anapolitaja mtu ambae ni msemaji wa Simba, haya mambo ndo yameiua Toto ya mwanza. Tabia ya kuvaa ngozi mbili
Hivi unaweza kunieleza nazi zinazotengenezwa na Simba SC zinaitwaje?!
 
Mbona mechi za Simba na Yanga zinaonyeshwa na hao hao Azam?

Hata kama mnamchukia Manara, leteni hoja sio viroja
 
Umezingua, hata kama ni account binafsi,
Huyu anafaa kufukuzwa kazi anahihujumu timu,
We unadhani mo haioni potential ya Manara kimatangazo

Usikute wanatafuta namna ya kumtoa hawamtaki

Sasa haji afe njaa kisa Simba

Haji hamia Yanga kabisa babako na mwanao Ni Yanga achana na mikia
 
Back
Top Bottom