Kwanini mtaani watu wasipokuelewa mishemishe zako wanakuita Usalama wa Taifa?

TheGreatest Of AllTime

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2025
Posts
207
Reaction score
679
Kuna namna unaishi inapelekea wale wajomba wanaokaa vijiweni na kwenye gahawa wanaanza kukujadili hadi kuja na conclusion kuwa wewe ni usalama wa taifa kumbe kijana wa watu hata bastola haujai kuiona live.

Unashangaa hata mtaani watu wanakuchukulia tofauti sana na hata ukienda mahala watu wanapiga stori unashangaa zinabadirika ghafla kuwa za simba na Yanga🀣
 
Hiyo hali sio nzuri maana utakosa madili kutoka kwa hao watu pia ukikataa ndo utazidi kuikoleza na itaonekana kweli hivyo usikubali wala kukataa acha mambo yajiendee hivyo
 
Mitaa yetu madongo kuinama..
Kuna mtaa mmoja nilibahatika kukaa pahala..wenyewe walikuwa wako America huko..aiseee...nilihama..maisha yalinishinda...kule kila Nyumba wanatoka na Range,Lc 200 ukiona saaana ni Prado hizi wa Wakuu wa Wilaya...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Muda wa mtu kukuona upo Usalama labda uwe ukuta wa Nyumba au Maua na Miti..πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…