Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikishuhudia mijadala mikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtandao wenye nguvu katika kuhamasisha mabadiliko na kutoa maoni. Hata hivyo, kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini na serikali dhidi ya Twitter, wakidai kwamba ina athari hasi kwenye maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Leo viongozi wa dini wameeleza wasiwasi wao kwamba Twitter inachangia katika kuharibu maadili ya vijana kwa kuruhusu na kukuza maudhui yanayohusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, ambayo yanakinzana na maadili, mila, na desturi za Kitanzania. Wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kufungia mtandao huo ili kulinda maadili ya taifa.
Kwa upande mwingine, kumewahi kuwa na ripoti kwamba serikali imetumia sera ya hakimiliki ya Twitter kama njia ya kunyamazisha wanaharakati. Hii inaonesha kwamba Twitter inaweza kuwa inapigwa vita si tu kwa sababu za maadili, bali pia kama njia ya kudhibiti uhuru wa kujieleza na kukosoa serikali.
HOJA👇
Wataka X ifungwe
Wataka X ifungwe
Mohamed Kawaida- Jumanne, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida alisema wamesikitishwa na baadhi ya mitandao ya kijamii inavyohimiza mapenzi ya jinsia moja.
"Tumeona kupitia Serikali yetu pendwa ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania mitandao yote yenye maudhui ya namna hii wameifungia sasa umefika wakati Serikali na mtandao huu nao kuufungia," alisema.
Amesisitiza kama wataondoa maudhui yanayofundisha mapenzi ya jinsia moja wako tayari kuendelea kutumia mtandao huo lakini kabla ya yote mtandao huu unapaswa ufungiwe.
"Serikali ya Tanzania imeshawahi kufungia mitandao ya kijamii ambayo ilikuwa inajihusisha na maudhui yasiofaa, hivyo basi waufungie mtandao huu kama mitandao iliyopita," alisema.
Allen Siso - Mbali na UVCCM, wito huo pia umetolewa na baadhi ya viongozi wa dini akiwamo Katibu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Allen Siso aliyeutuhumu mtandao wa X kwa kuchochea mapenzi ya jinsia moja na kuiomba serikali kuufungia.
"Naungana na viuongozi wa Taifa hili, kukemea kwa dhati ushoga, mapenzi ya jinsia moja katika Taifa letu, kukemea ulawiti na vitendo vyote vinavyoharibu taifa letu," amesema Siso katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Sheikh Hilal Yusuf - Naye Sheikh Hilal Yusuf maarufu Sheikh Kipozeo amesema: "Tunaiomba Serikali iliangalie kwa kina jambo hili na itusaidie kuiufungia Twitter (X) isiendelee kufanya kazi kwa sababu inatuharibia jamii."

Wapinga X kufungwa
Hata hivyo, maoni ya Kuifungia X yamepingwa na chama cha ACT Wazalendo wakisema ni njama za Serikali katika mwendelezo wa kuzuia haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni.
Rahma Mwita - Taarifa iliyotolewa na Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa chama hicho, Rahma Mwita imesema Serikali ya CCM imekuwa na utamaduni wa kutovumilia maoni, mitazamo na fikra tofauti zinazotolewa na wananchi kuhusu viongozi na sera zao.
"Mara zote inatumia hila za namna tofauti ili kutimiza dhamira hiyo kandamizi," amesema.
Alitaja mbinu hizo alizoita ni kandamizi kuwa pamoja na Sheria ya Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta ya 2010, Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015 na Sheria ya Takwimu ya 2015.
"Watanzania wamekuwa wakipitia mazingira magumu kutokana na hila za Serikali kudhibiti uhuru na maoni yao dhidi ya watawala," amesema.
John Pambalu - Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Pambalu ameandika katika ukurasa wake wa X akiikosoa UVCCM.
"Kwamba UVCCM waliposikia tu mtandao unaitwa X tu wakajua utakuwa na mambo ya X (ngono). Kwa nini waliposikia mtandao unaitwa X akili yao haikuwatuma kwenye zile hesabu za darasa la saba za tafuta thamani ya X na Y? Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo."
Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo amesema wanaopiga kampeni hiyo ni maadui wa uhuru wa kujieleza wanaotumia visingizio vingi kuhalalisha dhamira yao kwa kujua kwa kutojua.
"Sera ya mtandao wa X siyo mpya na imekuwa ikieleza wazi kwamba unaweza kukubali kuangalia maudhui yoyote unayotaka," amesema.
Ameitaka Serikali kupeleka malalamiko yake X kueleza mambo inayolalamikia na itafute suluhisho.
"Kama Serikali ina malalamiko basi iwaandikie barua iwaeleze mambo wanayotaka yarekebishwe kwa mfano maudhui yanayoharibu watoto, kwa sababu Tanzania kama nchi huru ina wajibu wa kulinda raia wake, lakini siyo kutaka ufungiwe kabisa".
"Kama Mwalimu Julius Nyerere alivyosema ukishaanza kula nyama ya mtu, hautaacha, hivyo mkishaanza kufungia mtandao mmoja, hamtaishia hapo, mtaenda Instagram, kisha Facebook, Tiktok, halafu mtahamia kwenye magazeti, redio na televisheni," amesema.
Ameshauri Serikali kutumia jumuiya za kikanda kufikisha malalamiko yake ikiwamo (Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika), SADC Afrika Mashariki (EAC) au Umoja wa Afrika (AU).
Ernest Sungura - Mdau wa vyombo vya habari, Ernest Sungura amesema juhudi zozote za kuzuia uhuru wa kujieleza zinakwenda kinyume na Katiba na maazimio ya kimataifa ya haki za binadamu.
"Uhuru wa kujieleza ndio haki ya Kikatiba unaostahili kulindwa siyo tu na Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayostahili kulindwa, bali pia matamko na maazimio ya kimataifa na kikanda na Serikali zinapaswa kuheshimu hilo," alisema.
Frank James- Mmoja wa watumiaji wa mtandao huo, Mkazi wa jijini Mwanza, Frank James amesema:
"Tunachokiona tunakwenda kwenye uchaguzi, sasa isije kuwa ni mkakati wa kutaka kuufunga kwa hofu tu ya nini kitatokea kama utaachwa. Serikali isikubali kuingia mtego huu wa kuufunga kwani hautakuwa na afya."
Fila Samson - Mfanyabiashara na mjasiriamali, Fila Samson aliitaka Serikali kuangalia namna ya kushughulika na wanaosambaza na maudhui yasiyofaa na kuwachukulia hatua wapotoshaji badala ya kufuga mtandao mzima nchini.
Kwa sababu yeye binafsi mtandao huo ndiyo unaomfanya kuendesha maisha yake baada ya kujiwekeza na kutengeneza jina ambalo watu wamelizoea jambo linalomuwezesha kupata wateja wengi.
"Nguvu zetu ziko Twitter (X), tunakula kupitia huko ukifunga unamaanisha kuwa tutafute njia nyingine ya kutafuta hela na wateja, taani tuanze upya, ujue unapata wapi wateja, kuwezekeza kupata wateja itatuathiri haijakaa sawa," amesema Samson ambaye hutengeneza picha mbao, saa, vikombe vyenye ujumbe mbalimbali na kuuza.
Mdau - Mfanyabiashara ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kufungia mtandao wa X haiwezi kuwa suluhisho la kuzuia maudhui wanayoyapiga vita bali kutafuta namna ambayo wanaweza kushughulika nayo.
"Kufunga ni kuonyesha udhaifu mkubwa kwamba vyombo vyetu husika vimeshindwa kuchukua hatua za kudhibiti maudhui yanayolalamikiwa na hawatoshi kukaa pale, kufunga siyo suluhisho, watu wanaweza kuhamishia kitu hicho hicho katika mitandao mingine, wajitathimini," amesema.

Kauli ya Serikali
Mobhare Matinyi - Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alipoulizwa amesema wameshaanza mazungumzo na kampuni ya X.
"Ni kweli kwamba wiki iliyopita vyombo vya habari duniani vilitangaza kwamba mtandao wa X sasa utaruhusu maudhui ya picha za ngono kurushwa hewani.
"Bado Serikali inalitafakari jambo hili na kimsingi ilishaanza mazungumzo na wamiliki wa X kabla ya jambo hilo ili waheshimu sheria yetu ya usalama mtandaoni na kanuni za maudhui lakini bado hawajatoa ushirikiano," amesema.
Amesema mitandao mingine hufuata maelekezo ya Serikali ili kuzuia maudhui yasiyofaa kuingia Tanzania na hivyo kuruhusu wananchi wetu kuendelea kuitumia kwa shughuli zao.
"Ni matarajio yetu hata X nao watatoa ushirikiano. Kwa sasa Serikali bado haijachukua hatua. Serikali haifanyi mambo kwa papara bali inatumia sheria, utaalamu na kutanguliza mbele maslahi ya jamii ya Watanzania. Ikichukua hatua itatoa taarifa kupitia mamlaka au wizara inayosimamia sekta hii,"amesema.
Hata hivyo, yapo maswali ya msingi ya kujadili kama jamii ikiwa pamoja na;

- Je, ni sahihi kwa serikali na viongozi wa dini kupinga matumizi ya Twitter kwa misingi ya maadili na utamaduni?
- Je, kuna njia mbadala za kushughulikia wasiwasi wa maadili bila kuzuia uhuru wa kujieleza?
- Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba maadili na mila za Kitanzania zinalindwa katika zama za utandawazi?
- Kutoa nafasi kwa wanajamii kueleza maoni yao kuhusu sababu za Twitter kupigwa vita nchini Tanzania, na iwapo inapaswa kufungiwa.
- Kujadili uwiano kati ya kulinda maadili na uhuru wa kujieleza katika jamii.
- Kupata maoni mbalimbali kuhusu jinsi gani jamii inaweza kulinda maadili yake katika zama za utandawazi bila kuzuia maendeleo ya teknolojia.
Nakaribisha michango yenu yenye tija na hoja zenye mantiki kwa mjadala huu muhimu unaogusa dhana ya haki na uhuru wa kujieleza kwa kila
ANGALIZO
Mjadala huu umetengenezwa kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayoathiri jamii yetu. Tunaheshimu maoni na imani za kila mtu na tunasisitiza mjadala wenye heshima na staha.