Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Shekhe anasema watu wanatumia X kufundishiana ushoga[emoji1]
Hivi Twitter ina watumiaji kiasi gani had waogope inasambaza ushoga? Afu mbona ukitazama ni mashoga wachache wako Twitter na hasa wale waliopita shule.

Waache uoga was kijinga, maadili hayafunidishwi Twitter, ni huko majumbani.
 
Hoja kutoka X (Twitter)👇.
Screenshot_20240611-210908.jpg
 
Viongozi wa dini waiomba serikali kuufungia mtandao wa kijamii wa Twitter ( X ) nchini kwani mtandao huo umeonekana ukivunja maadili na taratibu za nchi kwa kuhamasisha ushoga na usagaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 11,2024 Mwenyekiti mstaafu wa Baraza Kuu la Waislam Vijana Tanzania na Mhadhiri mkubwa Shekh Alhaji Sulle amesema kufuatia na Dunia kuingia katika utandawazi kumepelekea kumomonyoka kwa maadili na kupelekea kuharibu taswira ya nchi.

Amesema mtandao wa Twitter (X) umekuwa ukihamasisha mapenzi ya jinsia moja na ushoga jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

"Tunawajibu wa kuyapima mambo ambayo tunaletewa ambayo yapo kinyume na maadili tunapaswa kuyapinga vikali ili kulinda maadali na tamaduni zetu za Kitanzania na kulinda kizazi kilichopo sasa na kijacho," amesema.

Kwa upande wake, Askofu Allen Siso amesema madhara yanayotokana na kuruhusu mtandao huo kwa jamii ni kukosa kizazi chenye maadili na kuvunja tamaduni za nchi ambapo ameiomba Serikali kupitia Bunge na Wizara husika ichukue hatua za haraka kuufungia mtandao huo ili kulinda tamaduni na maadili ya nchi lakini pia kufuata maandika ya neno la Mungu ambayo yanapinga vikali vitendo hivyo vya usagaji na mapenzi ya jinsia moja.
 
Attachments

  • VID-20240611-WA0099.mp4
    7 MB
Hivi Twitter ina watumiaji kiasi gani had waogope inasambaza ushoga? Afu mbona ukitazama ni mashoga wachache wako Twitter na hasa wale waliopita shule.

Waache uoga was kijinga, maadili hayafunidishwi Twitter, ni huko majumbani.
Bora wangefungia TikTok 🤦
 
Hivi Ushoga wanafundishana? Najua kuna ushawishi ila inabaki suala la muhusika kukubali au kukataa.

Kwahiyo huko Twitter hakuna mada zingine zinazopatikana ila ni ushoga tyuu? Serikali iache kuhadaa umma, waseme wazi wanaogopa kukosolewa na kule watu wako smart ktk kupiga spana.

Mange yujo winja winja kulee na atawanyoosha sana.
 
Kulishapoa! Kaingia yule jini Mange Kimambi ndio kumeamka tena. Hawapambani na X wanapambana na Mange.
Kabisa aisee na mange aje huku jf afu asema anapatika jf kudadeki itajaza sana. Sema kwann wanatumia nguvu kubwa kupambana na mange. Kuna kitu naweza sema mange anajua na ameanza watajuta. Mpare yule harudishi miguu nyuma
 
Hivi Ushoga wanafundishana? Najua kuna ushawishi ila inabaki suala la muhusika kukubali au kukataa.

Kwahiyo huko Twitter hakuna mada zingine zinazopatikana ila ni ushoga tyuu? Serikali iache kuhadaa umma, waseme wazi wanaogopa kukosolewa na kule watu wako smart ktk kupiga spana.

Mange yujo winja winja kulee na atawanyoosha sana.
.ᴉzᴉɯɐpuɐʍɯ ɐɓoɥS
 
Kabisa aisee na mange aje huku jf afu asema anapatika jf kudadeki itajaza sana. Sema kwann wanatumia nguvu kubwa kupambana na mange. Kuna kitu naweza sema mange anajua na ameanza watajuta. Mpare yule harudishi miguu nyuma
Kutanoga sana hasa kuelekea uchaguzi mkuu
 
.ᴉzᴉɯɐpuɐʍɯ ɐɓoɥS
Bado hujasemaaa!!!
Afu ni hivi, hii vita hamuwezi shinda kamwee, straight uchwara mnabaki kulia lia kila leo

Afu sio mwandamizi, mie ni Katibu muenezi kanda ya Africa Mashariki, Karibu kundini bwasheeeee.

Njoo tuunge juhudi, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom