Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Mimi nilitegemea hao viongozi wa dini wangeanza na wasanii wa bongo fleva. Wasanii kwa siku za karibuni ndiyo wamekua namba moja kwenye kuharibu maadili kupitia mashahiri na video za utupu zinazopigwa kila uchwao kwenye luninga huku watoto wakizitazama na kuimba. Wasanii wakubwa na maarufu ndiyo geti la maadili mabovu na wanajulikana tuanze nao hao kwanza ndiyo twende huko X.
 
Nakumbuka kwenye sakata la sukari,waziri Bashe alikuwa anajibu kwa maelezo mengi kule X,lakini alikutana na nondo za watu mpaka akaonekana muongo.

Waziri kama Ummy Mwalimu,huwa anapata shida sana kule X.

Kinacho hofiwa zaidi sio maadili,bali ni uoga wa watawala wetu juu ya mawazo kinzani na yao.
 
Wasanii wengi wanaharibu watoto akiwemo harmonize,diamond ,zuchu mbona hatuoni hizo kelelelele
 
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikishuhudia mijadala mikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtandao wenye nguvu katika kuhamasisha mabadiliko na kutoa maoni. Hata hivyo, kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini na serikali dhidi ya Twitter, wakidai kwamba ina athari hasi kwenye maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Leo viongozi wa dini wameeleza wasiwasi wao kwamba Twitter inachangia katika kuharibu maadili ya vijana kwa kuruhusu na kukuza maudhui yanayohusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, ambayo yanakinzana na maadili, mila, na desturi za Kitanzania. Wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kufungia mtandao huo ili kulinda maadili ya taifa.​
Kwa upande mwingine, kumewahi kuwa na ripoti kwamba serikali imetumia sera ya hakimiliki ya Twitter kama njia ya kunyamazisha wanaharakati. Hii inaonesha kwamba Twitter inaweza kuwa inapigwa vita si tu kwa sababu za maadili, bali pia kama njia ya kudhibiti uhuru wa kujieleza na kukosoa serikali.​
Hata hivyo, yapo maswali ya msingi ya kujadili kama jamii ikiwa pamoja na;​
  1. Je, ni sahihi kwa serikali na viongozi wa dini kupinga matumizi ya Twitter kwa misingi ya maadili na utamaduni?​
  2. Je, kuna njia mbadala za kushughulikia wasiwasi wa maadili bila kuzuia uhuru wa kujieleza?​
  3. Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba maadili na mila za Kitanzania zinalindwa katika zama za utandawazi?​
Mjadala huu unalenga;
  • Kutoa nafasi kwa wanajamii kueleza maoni yao kuhusu sababu za Twitter kupigwa vita nchini Tanzania, na iwapo inapaswa kufungiwa.​
  • Kujadili uwiano kati ya kulinda maadili na uhuru wa kujieleza katika jamii.​
  • Kupata maoni mbalimbali kuhusu jinsi gani jamii inaweza kulinda maadili yake katika zama za utandawazi bila kuzuia maendeleo ya teknolojia.​
Nakaribisha michango yenu yenye tija na hoja zenye mantiki kwa mjadala huu muhimu unaogusa dhana ya haki na uhuru wa kujieleza kwa kila​

ANGALIZO
Mjadala huu umetengenezwa kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayoathiri jamii yetu. Tunaheshimu maoni na imani za kila mtu na tunasisitiza mjadala wenye heshima na staha.
Hawataki watu wenye akili wanataka tuwe wapumbavu tunashinda insta tunabishania ujinga wakina diamond na kibushuti cha mtwara
 
Ni kwa sababu "Nani kama mama" kashambuliwa huko na kuhusishwa na mambo machafu..

Inashangaza kuwa mtu mmoja tu kushambuliwa kwa matendo yake ya hovyo, ligeuke kuwa janga la watu wote.

Tatizo siyo mtandao wa Twitter X bali matendo machafu na ya hovyo ya viongozi wetu. Wajirekebishe na waache mambo hayo. Hiyo ndiyo salama yao. Ukifunga Twitter X, uchafu wao (wizi na kufisadi mali ya umma, ushoga wao, ulawiti wao, usagaji wao nk), utatafuta njia nyingine ya kutokea na jamii ya dunia yote itajua tu!

Huwezi kuficha ukweli kudhihirika!!
 
d61b0a3f500486f83c289e48e6cc09b7.png
 
Nchi imefunga access za mitandao ya ngono. Hivyo hiyo imegeukq kuwa portal ya kubypass mpango huo ukiacha vpn.
Point watafute namba ya kufilterna kama ni policy ya Twitter kuhimiza ngono na ushoga basi iwekwe kando kwa sababu hizo.
Hujajibu swali

Picha na video za ngono zinakuja zenyewe au mtumiaji anazitafuta?
 
Back
Top Bottom