Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

HOJA Kutoka X (Twitter), 👇.
IMG-20240612-WA0001.jpg
 
Ndoto za Abunuwasi hizo Yaan wewe Mange aitishie Serikali?ni vile tu hawajaamua mbona kitukanio chake wamekifungia.
 
Fatma amejibu vizuri sanaa,Ukitaka content za ngono utanipa ta?Ukitaka hata hapa JF utazipata tuu.
 
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikishuhudia mijadala mikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtandao wenye nguvu katika kuhamasisha mabadiliko na kutoa maoni. Hata hivyo, kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini na serikali dhidi ya Twitter, wakidai kwamba ina athari hasi kwenye maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Leo viongozi wa dini wameeleza wasiwasi wao kwamba Twitter inachangia katika kuharibu maadili ya vijana kwa kuruhusu na kukuza maudhui yanayohusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, ambayo yanakinzana na maadili, mila, na desturi za Kitanzania. Wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kufungia mtandao huo ili kulinda maadili ya taifa.​
Kwa upande mwingine, kumewahi kuwa na ripoti kwamba serikali imetumia sera ya hakimiliki ya Twitter kama njia ya kunyamazisha wanaharakati. Hii inaonesha kwamba Twitter inaweza kuwa inapigwa vita si tu kwa sababu za maadili, bali pia kama njia ya kudhibiti uhuru wa kujieleza na kukosoa serikali.​
Hata hivyo, yapo maswali ya msingi ya kujadili kama jamii ikiwa pamoja na;​
  1. Je, ni sahihi kwa serikali na viongozi wa dini kupinga matumizi ya Twitter kwa misingi ya maadili na utamaduni?​
  2. Je, kuna njia mbadala za kushughulikia wasiwasi wa maadili bila kuzuia uhuru wa kujieleza?​
  3. Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba maadili na mila za Kitanzania zinalindwa katika zama za utandawazi?​
Mjadala huu unalenga;
  • Kutoa nafasi kwa wanajamii kueleza maoni yao kuhusu sababu za Twitter kupigwa vita nchini Tanzania, na iwapo inapaswa kufungiwa.​
  • Kujadili uwiano kati ya kulinda maadili na uhuru wa kujieleza katika jamii.​
  • Kupata maoni mbalimbali kuhusu jinsi gani jamii inaweza kulinda maadili yake katika zama za utandawazi bila kuzuia maendeleo ya teknolojia.​
Nakaribisha michango yenu yenye tija na hoja zenye mantiki kwa mjadala huu muhimu unaogusa dhana ya haki na uhuru wa kujieleza kwa kila​

ANGALIZO
Mjadala huu umetengenezwa kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayoathiri jamii yetu. Tunaheshimu maoni na imani za kila mtu na tunasisitiza mjadala wenye heshima na staha.
Si X pekee, hata vikundi vya kwaya makanisani navyo huharibu vijana.
 
Wenye kuupromoti Ushoga ni CCM wenyewe na kile kitengo chao cha kupakazia Ushoga wapinzani wao !

Kila wanayemuogopa kwa hoja zake huwa anapakaziwa kuwa ni shoga !
Vijana wadogo wakisikia hizo habari wanaona kumbe Ushoga ni kitu cha kawaida tu kwa mtu yeyote kuufanya 🙄
Wanakuwa interested na hayo mambo 🙄
CCM wanaiharibu Nchi na Jamii kutoka kila angle kwa sababu ya Ulafi wa madaraka 😳🙄
 
Personally, nina muda kidogo toka niache kuingia twitter so sijui kipi hasa kinaendelea humo. Kilichonikimbiza humo ni hii mambo ya video za ngono kila kona hata hata ukizinyima kuonekana kuna namna utakutana nazo tu. So tukiweka politics aside hoja yao inamashiko.
🤣🤣🤣 you get what you search/view
 
Hili swali zuri sana.
Ni sawa na watu kusema ooh telegram kumejaa watu wanajiuza, kuna watu wanataman wawaone hao wanaojiuza telegram ila hawawaoni maana ni hadi usearch, sometimes uwe na connection ama ulipie kabisa kupewa link..

Ko unakuja kuona kwamba ni mtu mwenyewe kwa tamaa zake kasearch makitu ya ajabu, nafsi yake ikianza kumsuta kua anafanya dhambi basi anawatupia lawama wengine na sio yeye.
Umeangalia porn mwenyewe, umejichukulia sheria mkononi mwenyewe, kwenye kujuta unaanza kuilaumu telegram au X.
 
Back
Top Bottom