Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

jibu ni moja tu. kwasababu mtu mmoja katukanwa, basi watz wote wasiangalie twitter. hivi ukitukanwa kama unachotukaniwa ni cha uongo, ukinyamaza kimya unapungukiwa nini? just ignore, mtukanaji kama ni mwongo uongo wake utajidhihirisha tu na atachoka na watu watamdharau. ila ukibishana naye, basi inaelekea kile anachokisema ni cha kweli.
 
Na machawa wote wameona ngao yao kubwa ni kusingizia mambo ya ushoga. 😂
Hawana propaganda nyingine mpya zaidi ya hiyo 🙄🤠
Bure kabisa. 🙄🤠
wajinga leo tz kama taifa maskini ,ndo wa kusema X kama mtandao ufungiwe ,kwanza hawajui viongozi wakuu katika dunia hii wakiwemo Marais ndo mtandao unaotumika na kuheshimika, mfano hawa UVCCM Mbona mwenyekiti wao yupo na account kule ? Na mara nyingi ata Salam za misiba na majanga mengine kwa marais wenziwe ,hutumia account bila kujali nani anaiendesha kwa niaba yake , sasa hawa uvccm kupitia chawa mkuu wao ,mwenyekiti wa Uvccm Taifa anakuja na mihemuko ya kijinga kabisa.

Ok wafunge sote na akiwemo na mwenyekiti wao ,nawataule wake wote hatutatumia ,ujinga mtupu
 
Ni mtandao pekee ambao unatumiwa walau na kundi la watu wanaojitambua hivyo kule kiongozi wa CCM kurudishwa darasani kwa hoja ni suala la dakika.

Japo yapo makapi kama ilivyo kwenye msafara wa mamba na kenge wanakuwemo hapo ndio unawakuta Lumumba buku 7 ambao ndio wanafuatilia.

Ukifuatilia mjadala wa kufutwa kwa toto afya card na kuondolewa kwa dawa kwenye scheme ya NHIF utaona vile nguvu ya mtandao huo ilivyokuwa kubwa

Maana waziri wa afya ambaye kwangu namuona ni waziri wa hovyo kushika nafasi ile hoja zilimzidi hakuwa na cha kujibu account yake, wizara ya afya na NHIF wenyewe walibidi kufunga uwanja wa comments kutokana na kutokuwa na majibu kwa maswali yanayoulizwa.
 
Sababu ni moja twitter ndo imeshika nafasi ya JF 2007-2017,

Jf baada ya 2017 si chochote si lolote
Yamejaa matangazo ya kuuza viwanja na uganga! JF kwa sasa HAINA tofauti na global publisher au Gazet la mwananchi!

ZILE be first to know haziko Tena JF, na JF si tishio Tena,

Nondo za zamani watu walizokiwa wanamwaga akina
Mchambuzi, Kashaija butege, Kalamu, Mkandara, kiranga, Mag33 siku hizi wakiziweka zinafutwa muda huo huo ,
Hivo kule X au twitter mtu ana ji moderate mwenyewe ! Atajua afiche vipi ID zake ! Lakin Mara nyingi kwa sasa mabadiliko makubwa ya Jamaa na elimu na ujuzaji wa Habari za kutisha yapo X

Kuna account ya Exmayor Ubungo, kuna account ya Tanzanialeakes, kuna account za akina Tanzania Abroad TV, na akina lema nnaa wengine zinatema mambo Mpaka unashangaa kwamba kumbe nchi ndo ilivyo

Britanicca
Napinga jf bado ipo imesimama ,shida machawa kule hawana hoja kama ambavyo tumekua tunawaona hapa jf wakija na hoja mfu , badala watetee na kujenga chama chao ccm , wapo na ya chadema na vyama vingine , inataka miaka 20 ijayo kujenga tena vijana wenye uwezo wa kupangua hoja na kuleta hoja makini ndani ya ccm , alafu wapo pale kazi kuitana comrady
Na machawa wote wameona ngao yao kubwa ni kusingizia mambo ya ushoga. 😂
Hawana propaganda nyingine mpya zaidi ya hiyo 🙄🤠
Bure kabisa. 🙄🤠
 
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikishuhudia mijadala mikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtandao wenye nguvu katika kuhamasisha mabadiliko na kutoa maoni. Hata hivyo, kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini na serikali dhidi ya Twitter, wakidai kwamba ina athari hasi kwenye maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Leo viongozi wa dini wameeleza wasiwasi wao kwamba Twitter inachangia katika kuharibu maadili ya vijana kwa kuruhusu na kukuza maudhui yanayohusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, ambayo yanakinzana na maadili, mila, na desturi za Kitanzania. Wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kufungia mtandao huo ili kulinda maadili ya taifa.​
Kwa upande mwingine, kumewahi kuwa na ripoti kwamba serikali imetumia sera ya hakimiliki ya Twitter kama njia ya kunyamazisha wanaharakati. Hii inaonesha kwamba Twitter inaweza kuwa inapigwa vita si tu kwa sababu za maadili, bali pia kama njia ya kudhibiti uhuru wa kujieleza na kukosoa serikali.​
Hata hivyo, yapo maswali ya msingi ya kujadili kama jamii ikiwa pamoja na;​
  1. Je, ni sahihi kwa serikali na viongozi wa dini kupinga matumizi ya Twitter kwa misingi ya maadili na utamaduni?​
  2. Je, kuna njia mbadala za kushughulikia wasiwasi wa maadili bila kuzuia uhuru wa kujieleza?​
  3. Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba maadili na mila za Kitanzania zinalindwa katika zama za utandawazi?​
Mjadala huu unalenga;
  • Kutoa nafasi kwa wanajamii kueleza maoni yao kuhusu sababu za Twitter kupigwa vita nchini Tanzania, na iwapo inapaswa kufungiwa.​
  • Kujadili uwiano kati ya kulinda maadili na uhuru wa kujieleza katika jamii.​
  • Kupata maoni mbalimbali kuhusu jinsi gani jamii inaweza kulinda maadili yake katika zama za utandawazi bila kuzuia maendeleo ya teknolojia.​
Nakaribisha michango yenu yenye tija na hoja zenye mantiki kwa mjadala huu muhimu unaogusa dhana ya haki na uhuru wa kujieleza kwa kila​

ANGALIZO
Mjadala huu umetengenezwa kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayoathiri jamii yetu. Tunaheshimu maoni na imani za kila mtu na tunasisitiza mjadala wenye heshima na staha.
Video ngona twiter nyungi. Kila siku nguvu za kiume zinaisha kwa kuzipigia punyeto
 
Na mara nyingi ata Salam za misiba na majanga mengine kwa marais wenziwe ,hutumia account bila kujali nani anaiendesha kwa niaba yake
Swali Kutoka X (Twitter) 👇.
IMG_20240612_163832.jpg
 
Swali Kutoka X (Twitter) 👇.
Umepiga penye , kwa ushahidi huu Mwenyekiti wa Uvccm taifa ajiuzulu mwenyewe kabla sijamfuata ofisini kumchapa vibao au fuatwa na mkono wa mungu, mashehe wote waliochafua mtandao wa X kwa uchawa wachukuliwe hatua kali , maana wamemshambulia Rais wa nchi wakidhani wanajenga kumbe wanabomoa , kama accout ya rais ipo kule na sio yeye tu karibia marais wote Dunian wao ni nani ndani ya dunia hii shambolia mtandao huu kisa uchawwa ilihali marais wa dunia nzima kama sio wote wako kule achana na mawaziri , na sector mbalimbali ni mchawi anaweza sema x ifunguwe tz
sie ni nani , jaribu muone.

Biden yupo humo , rais wa USA sembuse kikorogosi cha uvccm kutoa maneno ya kijinga , hivi uyu dogo mpaka sasa anajua amearibu pakubwa, anajua tz zipo barozi mbalimbali ? Ccm kama chama sina shida nacho ,shida wameruhusu akili ndongo ongoza akili kubwa ,hii ndo shida , sasa fungeni tuone , ccm hamuijui dunia japo mwazurula kila nchi ,
 
MJADALA UPDATES👇.

IMG_20240612_181405.jpg
=========================================​
By Asia Gamba June 12, 2024
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kinapinga vikali na kukemea kwa nguvu zote kauli za CCM na Mashabiki zake za kutaka kufungwa kwa mtandao wa X (zamani Twitter) ambapo ACT imesema ni wazi kuwa kauli hizo ni njama za Serikali katika mwendelezo wa kuzuia haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni kupitia majukwaa mbalimbali ya habari.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 12,2024, Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo, Rahma Mwita amesema Serikali ya CCM imekuwa na utamaduni wa kutovumilia maoni, mitazamo na fikra tofauti zinazotolewa na Wananchi kuhusu Viongozi na sera zao, na mara zote inatumia hila za namna tofautitofauti ili kutimiza dhamira hiyo kandamizi.

Itakumbukwa Juni 11,2024 Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM aliitisha mkutano na wanahabari na kutoa tamko la kuishinikiza Serikali kufungia mtandao huo kwa madai kuwa unahamasisha ngono.

Hivi karibuni tumepokea taarifa ambayo kidogo Vijana wa CCM imetushtua kidogo kupitia mtandao wetu huu ambao unaitwa mtandao wa X(Twitter) na sisi wengine tulishtuka mapema, kwanza ukitazama tu jina lake lenyewe limeshaanza kuitwa X maana yake Saikolojikali tumeaanza kuandaliwa ili kila kitu kinachokuja ndani yake tuone nicha kawaida sasa ndugu zetu hawa wametoa tangazo la kuruhusu kwamba maudhui yote ya kingono na mengineyo ambayo ukifuatilia tamaduni zetu kama Watanzania unaona ni vitu ambavyo hatuendani navyo, na tumeona kupitia Serikali yetu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mitandao yote yenye maudhui ya namna hii wameifungia, sasa umefika wakati, Serikali yetu na mtandao huu kuufungia”- Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM.

Hatua hii imehusishwa na nia ovu ya Serikali kutaka kutekeleza jambo hilo wakati huu ambapo Tanzania inajiandaa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema Serikali ina nia ya kutaka kuzima maoni huru ya wananchi dhidi ya watawala.

Mbinu hizo zinaanza na sheria kandamizi kama vile Sheria ya Magazeti ya 1976, Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta 2010, Sheria za Makosa ya Kimtandao 2015, Sheria ya Takwimu 2015 na nyingine nyingi, Watanzania wamekuwa wakipitia mazingira magumu kutokana na hila za Serikali kudhibiti uhuru na maoni yao dhidi ya Watawala.Serikali imekuwa ikitoa mashambulizi kwa Wananchi kwa sura mbalimbali, wapo wanaotishwa, kutozwa fidia na kufungwa jela kwa kutoa maoni tofauti ambayo Serikali inayaita ‘makosa ya uchochezi’, vilevile tunashuhudia kufungiwa na kufutwa kwa vyombo vya habari, alimradi kuvifanya visifanye majukumu yao kwa uhuru”

Aidha wameitaka Serikali kutumia sheria zilizotungwa kudhibiti wanaotumia mitandao kuhamasisha ngono na sio kuifungia

Hoja za maadili zinazotolewa na wapambe ni dhaifu, makosa ya maadili yamewekewa sheria na utaratibu wa kushughulikiwa, kama kuna Wananchi wanafanya makosa yoyote ya kimaadili mtandaoni (Twitter) zipo sheria sio kufunga mitandao, Serikali iache kujificha kwenye kichaka cha maadili, ACT Wazalendo inaungana na watanzania waliojitokeza kupinga chokochoko za Wapambe na baadhi ya Viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, tunatoa wito kwa Wadau wote kushikamana ili kulinda uhuru wa kupata habari Nchini kwa kupinga hila zozote za Serikali kukandamiza haki hiyo”

Wakati ACT Wazalendo wakitoa kauli hiyo tayari baadhi ya viongozi wa dini wameunga mkono hoja hiyo ya UVCCM

=========================================
UPDATE
SISI TANZANIA YAUNGANA NA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA UVCCM KATIKA KUUNGA MKONO SUALA LA MTANDAO WA X (Twitter) KUFUNGIWA
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, Mkurugenzi wa taasisi ya Sisi Tanzania, Bw. Medot Mashaka Medot, alieleza kuwa wameandaa barua yenye mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Mkurugenzi wa TCRA na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia. Barua hiyo inapendekeza serikali kuchukua hatua za kudhibiti mitandao ya kijamii, hasa X (Twitter), ambayo inadaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Video👇.

=========================================
UPDATE
JUMIKITA :SERIKALI ISIINGIE KWENYE MTEGO WA KUFUNGIA MTANDAO WA 'X ' ZAMANI TWITTER
habarimpyatv_-20240612-0001.jpg
Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania

Leo Juni 12,2024, Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Ndg.Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Uongozi makini wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii

"Ni kama ilivyo Instagram ,Facebook na YouTube, 'x' au Twitter ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha 'x' "​

Taarifa ya Jukwaa imeongeza kua
"JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo"

=========================================
UPDATE
ABDUL NONDO: "ukiangalia hii picha yote unaona kuna jambo linapikwa, ukiniuliza mimi, nitasema kuna jambo linapikwa"

Kuhusu mtandao wa X (Twitter) kupigwa vita, kwa upande wake Mwenyekiti wa ngome ya vijana ya ACT Wazalendo Bwn. Abdul Nondo amesema anaona kuna suala linapikwa na serikali na si sababu za maadili kama wanavyo sema.

Video 👇
 
Hawa huwa wa zee kufuata upepo
Binafsi kama ambavyo mjinga mmoja kapendekeza yule wa uvccm ,wafunge tukose wote , na tuone dunia itawaelewa kama wajinga au waelevu. UVCCM NA MASHEHE wazalilisha kiti cha nchi nikimanishq Rais na Taaifa kwa upunguani wa akili , kwamba Rais wa nchi ambae amekua na anayo account ya x before (tweeter) hajui jema mpaka account ipo kule ?

CCM ELEWA RAIS NI WETU WOTE AKISHACHAGULIWA BILA KUJALI AMETOKA CHAMA GANI ,MSIJITWIKE USHAWISHI USIO KUA NA HUALISIA ,KAENI KITAKO MJENGE CHAMA, MDA MWALIMU
 
wajinga leo tz kama taifa maskini ,ndo wa kusema X kama mtandao ufungiwe ,kwanza hawajui viongozi wakuu katika dunia hii wakiwemo Marais ndo mtandao unaotumika na kuheshimika, mfano hawa UVCCM Mbona mwenyekiti wao yupo na account kule ? Na mara nyingi ata Salam za misiba na majanga mengine kwa marais wenziwe ,hutumia account bila kujali nani anaiendesha kwa niaba yake , sasa hawa uvccm kupitia chawa mkuu wao ,mwenyekiti wa Uvccm Taifa anakuja na mihemuko ya kijinga kabisa.

Ok wafunge sote na akiwemo na mwenyekiti wao ,nawataule wake wote hatutatumia ,ujinga mtupu
Bure kabisa hawa jamaa. 🙄
 
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikishuhudia mijadala mikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtandao wenye nguvu katika kuhamasisha mabadiliko na kutoa maoni. Hata hivyo, kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini na serikali dhidi ya Twitter, wakidai kwamba ina athari hasi kwenye maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Leo viongozi wa dini wameeleza wasiwasi wao kwamba Twitter inachangia katika kuharibu maadili ya vijana kwa kuruhusu na kukuza maudhui yanayohusiana na ushoga na mahusiano ya jinsia moja, ambayo yanakinzana na maadili, mila, na desturi za Kitanzania. Wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kufungia mtandao huo ili kulinda maadili ya taifa.​
Kwa upande mwingine, kumewahi kuwa na ripoti kwamba serikali imetumia sera ya hakimiliki ya Twitter kama njia ya kunyamazisha wanaharakati. Hii inaonesha kwamba Twitter inaweza kuwa inapigwa vita si tu kwa sababu za maadili, bali pia kama njia ya kudhibiti uhuru wa kujieleza na kukosoa serikali.​
Hata hivyo, yapo maswali ya msingi ya kujadili kama jamii ikiwa pamoja na;​
  1. Je, ni sahihi kwa serikali na viongozi wa dini kupinga matumizi ya Twitter kwa misingi ya maadili na utamaduni?​
  2. Je, kuna njia mbadala za kushughulikia wasiwasi wa maadili bila kuzuia uhuru wa kujieleza?​
  3. Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba maadili na mila za Kitanzania zinalindwa katika zama za utandawazi?​
Mjadala huu unalenga;
  • Kutoa nafasi kwa wanajamii kueleza maoni yao kuhusu sababu za Twitter kupigwa vita nchini Tanzania, na iwapo inapaswa kufungiwa.​
  • Kujadili uwiano kati ya kulinda maadili na uhuru wa kujieleza katika jamii.​
  • Kupata maoni mbalimbali kuhusu jinsi gani jamii inaweza kulinda maadili yake katika zama za utandawazi bila kuzuia maendeleo ya teknolojia.​
Nakaribisha michango yenu yenye tija na hoja zenye mantiki kwa mjadala huu muhimu unaogusa dhana ya haki na uhuru wa kujieleza kwa kila​

ANGALIZO
Mjadala huu umetengenezwa kwa lengo la kujadili masuala muhimu yanayoathiri jamii yetu. Tunaheshimu maoni na imani za kila mtu na tunasisitiza mjadala wenye heshima na staha.
Unawatia shoo viongozi hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom