Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Nimeanza kuamini kauli ya Makonda alivyosema wapo watu wanamtukana Rais ,mie hakuna mtu namchukia kama makonda, Sabaya wenda ni viongozi walitarajiwa kuwa wazuri ila wamelinajsi taifa kipindi cha mwendazake ,nasema ipo siku nitakutana nao Mbinguni na ole wao na wengine wanikute nyampala wa mbinguni !

Nasema kwa sababu tu Makoda mda mwingine kama sio kutumiwa vibaya wenda angeweza kuwa mtu safi , na amewahai sema kuna watu wanamtukana rais ila mpaka leo hakutaja majina ila alisema wengine ni mawaziri.

Ila namkosoa tu wengine wenda sio mawaziri ,ni hawa wananao sena mtandao wa X ufungwe kisa unaeeneza mambo mabaya kwenye jamii ikiwemo ushoga, wakati mwenyekiti wao na marais wenzake wapo humo kwa nia njema uyu uvccm na baadhi ya mashehe mengine wameyatoa wapi?

Uvccm mmelizlalisha taifa, mmezalisha Rais na watz wote ,jiuzuluni mara moja
 
Kwenye mitandao kuna kitu kinaitwa algorithms

Inakuletea vitu kutokana na mwenendo wako wa mambo unapenda kutazama au kusoma
Mitandao yote ya kijamii ukiacha x na telegram haina content za active porn. Kote kule algorithm zitakuletea picha na video zenye kutamanisha au nusu uchi. Youtbe tu ukiupload sexual contents achilia mbali porn unafitiwa kabisa channel kama sio kupigwa strike. Kule hata wewe ukitaka chukua porn clip au clip ya mashoga wanazini hakuna anayekujali.

Hiki ndio namaanisha
 
Mitandao yote ya kijamii ukiacha x na telegram haina content za active porn. Kote kule algorithm zitakuletea picha na video zenye kutamanisha au nusu uchi. Youtbe tu ukiupload sexual contents achilia mbali porn unafitiwa kabisa channel kama sio kupigwa strike. Kule hata wewe ukitaka chukua porn clip au clip ya mashoga wanazini hakuna anayekujali.

Hiki ndio namaanisha
Active porno zipo X kwa anayezitafuta au nakosea?
 
Mitandao yote ya kijamii ukiacha x na telegram haina content za active porn. Kote kule algorithm zitakuletea picha na video zenye kutamanisha au nusu uchi. Youtbe tu ukiupload sexual contents achilia mbali porn unafitiwa kabisa channel kama sio kupigwa strike. Kule hata wewe ukitaka chukua porn clip au clip ya mashoga wanazini hakuna anayekujali.

Hiki ndio namaanisha
Ukiona kwenye mitandao hii ,unaletewa upuuzi, umeanza wewe chokonoa huko mwenyewe , sasa uvccm, na baadhi ya mashehe wasihalibu taswira nzima ya ml 60 na kuzidi za wa tz , huu utakua ujinga, kwamba mashehe 2 au kumi na uvccm wapo na akili kuliko watz mil 60 ikiwemo no moja wa nchi hii ambaye ni Rais? Ambaye yupo na account kule achia mbali wateule wake. Mataifa ambayo ni msaada kwetu ikiwemo USA rais ananyoshewa kidole na matusi live bado maisha yanaenda sembuse sie , na yupo kwenye mtandao tajwa wa tweeter zamani ,kwa sasa x waitwa

Uongozi uvcc ujiuzulu na mara moja hii ni kashifa kuu kwa nchi, kiongozi wa wa nchi ambae ni mshirika na mdau kama walivyo marais wenzake Duniani kote yupo na account kule, uvccm na baadhi ya ma shehee wameidhalilisha dunia si tz tu

Note

Kama huu mtandao upo na madhara why hapa tz mawaziri na viongonzi wengine wapo kule ? Kwamba na uvccm na baadhi ya mashee wameona mapungufu haya? Mbona viongonzi wa dini wengine wapo ? Akiwepo Papa , kwamba nao hawaoni huu mtandao unaliangamiza jamii?
Ila tu uvccm ndo wamechunguza kwa makini na baadhi ya mashehehe kwamba haufai tz ,

Mwisho uvcc uongonzi mzima jiuzuru na Bwana amebarki ,fedhea gani hizi jamani watz wenzangu
Amani ya Mungu na ikawe nanyi,aisee Mungu bariki taifa hili
 
Personally, nina muda kidogo toka niache kuingia twitter so sijui kipi hasa kinaendelea humo. Kilichonikimbiza humo ni hii mambo ya video za ngono kila kona hata hata ukizinyima kuonekana kuna namna utakutana nazo tu. So tukiweka politics aside hoja yao inamashiko.
It means ulikuwa mdau
Algorithm haidanganyi
U get what ur interested in
 
MJADALA UPDATES👇.

View attachment 3015638
======================================​
By Asia Gamba June 12, 2024
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kinapinga vikali na kukemea kwa nguvu zote kauli za CCM na Mashabiki zake za kutaka kufungwa kwa mtandao wa X (zamani Twitter) ambapo ACT imesema ni wazi kuwa kauli hizo ni njama za Serikali katika mwendelezo wa kuzuia haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni kupitia majukwaa mbalimbali ya habari.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 12,2024, Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo, Rahma Mwita amesema Serikali ya CCM imekuwa na utamaduni wa kutovumilia maoni, mitazamo na fikra tofauti zinazotolewa na Wananchi kuhusu Viongozi na sera zao, na mara zote inatumia hila za namna tofautitofauti ili kutimiza dhamira hiyo kandamizi.

Itakumbukwa Juni 11,2024 Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM aliitisha mkutano na wanahabari na kutoa tamko la kuishinikiza Serikali kufungia mtandao huo kwa madai kuwa unahamasisha ngono.

Hivi karibuni tumepokea taarifa ambayo kidogo Vijana wa CCM imetushtua kidogo kupitia mtandao wetu huu ambao unaitwa mtandao wa X(Twitter) na sisi wengine tulishtuka mapema, kwanza ukitazama tu jina lake lenyewe limeshaanza kuitwa X maana yake Saikolojikali tumeaanza kuandaliwa ili kila kitu kinachokuja ndani yake tuone nicha kawaida sasa ndugu zetu hawa wametoa tangazo la kuruhusu kwamba maudhui yote ya kingono na mengineyo ambayo ukifuatilia tamaduni zetu kama Watanzania unaona ni vitu ambavyo hatuendani navyo, na tumeona kupitia Serikali yetu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mitandao yote yenye maudhui ya namna hii wameifungia, sasa umefika wakati, Serikali yetu na mtandao huu kuufungia”- Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM.

Hatua hii imehusishwa na nia ovu ya Serikali kutaka kutekeleza jambo hilo wakati huu ambapo Tanzania inajiandaa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema Serikali ina nia ya kutaka kuzima maoni huru ya wananchi dhidi ya watawala.

Mbinu hizo zinaanza na sheria kandamizi kama vile Sheria ya Magazeti ya 1976, Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta 2010, Sheria za Makosa ya Kimtandao 2015, Sheria ya Takwimu 2015 na nyingine nyingi, Watanzania wamekuwa wakipitia mazingira magumu kutokana na hila za Serikali kudhibiti uhuru na maoni yao dhidi ya Watawala.Serikali imekuwa ikitoa mashambulizi kwa Wananchi kwa sura mbalimbali, wapo wanaotishwa, kutozwa fidia na kufungwa jela kwa kutoa maoni tofauti ambayo Serikali inayaita ‘makosa ya uchochezi’, vilevile tunashuhudia kufungiwa na kufutwa kwa vyombo vya habari, alimradi kuvifanya visifanye majukumu yao kwa uhuru”

Aidha wameitaka Serikali kutumia sheria zilizotungwa kudhibiti wanaotumia mitandao kuhamasisha ngono na sio kuifungia

Hoja za maadili zinazotolewa na wapambe ni dhaifu, makosa ya maadili yamewekewa sheria na utaratibu wa kushughulikiwa, kama kuna Wananchi wanafanya makosa yoyote ya kimaadili mtandaoni (Twitter) zipo sheria sio kufunga mitandao, Serikali iache kujificha kwenye kichaka cha maadili, ACT Wazalendo inaungana na watanzania waliojitokeza kupinga chokochoko za Wapambe na baadhi ya Viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, tunatoa wito kwa Wadau wote kushikamana ili kulinda uhuru wa kupata habari Nchini kwa kupinga hila zozote za Serikali kukandamiza haki hiyo”

Wakati ACT Wazalendo wakitoa kauli hiyo tayari baadhi ya viongozi wa dini wameunga mkono hoja hiyo ya UVCCM

==========================================
UPDATE
SISI TANZANIA YAUNGANA NA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA UVCCM KATIKA KUUNGA MKONO SUALA LA MTANDAO WA X (Twitter) KUFUNGIWA
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, Mkurugenzi wa taasisi ya Sisi Tanzania, Bw. Medot Mashaka Medot, alieleza kuwa wameandaa barua yenye mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Mkurugenzi wa TCRA na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia. Barua hiyo inapendekeza serikali kuchukua hatua za kudhibiti mitandao ya kijamii, hasa X (Twitter), ambayo inadaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Video👇.

==========================================
UPDATE
ABDUL NONDO: "ukiangalia hii picha yote unaona kuna jambo linapikwa, ukiniuliza mimi, nitasema kuna jambo linapikwa"

Kuhusu mtandao wa X (Twitter) kupigwa vita, kwa upande wake Mwenyekiti wa ngome ya vijana ya ACT Wazalendo Bwn. Abdul Nondo amesema anaona kuna suala linapikwa na serikali na si sababu za maadili kama wanavyo sema.

Video 👇

Aisee kumbe jambo lipo serious kiasi hichi 😳
 
Kama ni hivyo kuna haja ya kuifungia X?
Kama nchi imeona zile mitandao zinaathari kitaifa, waongee na Musk ili waweke filter kwa hizo contents kwa Tanzania.

Mengine yanayoendelea hapo x hayana shida. Kama spana wapigane tu. Mwenyewe x ni mtandao ambao ninautumia kupush contents zangu kwenye niche za kiroho.
 
Kama nchi imeona zile mitandao zinaathari kitaifa, waongee na Musk ili waweke filter kwa hizo contents kwa Tanzania.

Mengine yanayoendelea hapo x hayana shida. Kama spana wapigane tu. Mwenyewe x ni mtandao ambao ninautumia kupush contents zangu kwenye niche za kiroho.
Ni watanzania wangapi wanatumia X?
 
Back
Top Bottom