Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini kwa mwalimu wake anatii?

Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini kwa mwalimu wake anatii?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini mwalimu wake akisema afanye kitu au achapwe fimbo tano bila kufuta na inawezekana?
 
Inategemea na malezi ,Mtoto na jamii kwa ujumla huwa wanaamini Mwalimu ni muongoza njia
 
tEna kwa mwalimu analala vizur na anaweza hata asilie au kutoa chozi lakin nyumban hata kabla fimbo hazijamfikia huanza kulia
 
Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini mwalimu wake akisema afanye kitu au achapwe fimbo tano bila kufuta na inawezekana?
ww n mzazi umayedekeza....na mtoto wako ni junior au queen
 
Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini mwalimu wake akisema afanye kitu au achapwe fimbo tano bila kufuta na inawezekana?
atakua huyo wa kwako tu,

yaan kijana wangu nimwambie kwendraa chini halafu anigomee???

anakula kofi kali sana la kushoto ambalo halinaga fomula na kwakweli ni hatari sana kwa afya yake.

na bado atakwenda chini, nitamtandika viboko kumi na vi-nne ili akaamwonyeshe mama yake wakati wa kumwogesha....
 
Endeleani Kulea watoto kimayai mayai Badae wakiwa mashoga mnaanza kulialia [emoji23][emoji23]
 
Huo muda wa kumwambia alale chini kwanza sina,akikosea ni papo hapo anatandikwa makofi anaenda kulilia mbele huko!!
 
Kwanini mtoto wako ukimwambia alale chini au anyonyooshe mikono umchape anakaidi lakini mwalimu wake akisema afanye kitu au achapwe fimbo tano bila kufuta na inawezekana?
waalimu ni wakatili sana, ndio maana huwa hawafanikiwi maishani. wamejaa roho mbaya na wivu tu. wachache sana wanafundisha watoto kwa moyo, zaidi sana hao watoto ni sisi wenyewe tunawasaidia majumbani, ndio maana huwa wanawapa hata homework maeneo ambayo hawajafundisha, ati watoto wakafanye homework. wanachapa watoto sana.
 
Hakuna adhabu ya kipumbavu na kitumwa kama kumchapa mtoto , sio njia sahihi ya kumfundisha mtoto , ni kumfanya mtoto awe mwoga na kukandamiza hisia zake ndani yake kwa hofu , madhara yake ni makubwa sana kwenye afya ya akili ya mtoto.
 
Hebu nifafanue kidogo hapa...mtoto akiwa mdogo sana kabla hata hajaanza shule huwa na iman kubwa sana na wazazi, mzazi au hata mlezi...inategemea analelewa na nani kati yao...

Akiwa anacheza na wenzie na akadhurika bas kuna maneno atayatamka...labda atasema naenda kusema kwa mama..au naenda kusema kwa baba...au atasema mlezi anae mlea..hii yote ni iman kubwa kwake kwamba atapata msaada..

Lakin akianza shule...sasa muda mwingi anakuwa na walimu au mwalimu...na wengi wa watoto sio wasikivu hivyo basi walimu hupendelelea kuwaadhibu na hapa pia inategemea na aina ya shule mtoto anayosoma..,akipewa viboko au adhabu yeyote atakataa then kuhadhibiwa kwa lazima...na hapo ndipo atakapo tamka naenda kusema kwa baba au mama au mlez yeyote tu anae mlea.....

Na hivyo basi atafika nyumban atamsemelea mwalimu kuwa kamchapa..,sasa wazaz wengi hupuuzia..huku wakimtuliza kwa uongo aah tutamfata mwalimu tutamchapa usijal...sasa akifika shule atachapwa tena na atareport kwa mzaz..na mzaz atarudia yale yale ya kumpooza..na hapa kuna dhana itajengeka kwenye ubongo wake..

Dhana yenyewe ni hii..atahis mwalimu ana nguvu sana kuliko wazazi, mzazi au mlez..mbona anapigwa na mzazi hafanyi chochote bas dhana ya kutii kwa mwalimu inaongezeka kwa kasi...

Lakin kuna umri akifika hasa balehe...bwana eeh pale hakuna cha mzaz wala mwalimu..😂😂😂 kama ni mtoto wa kike aisee boyfriend ana nguvu haswa...hapo hasikii wala haoni..😂😂 dadeki
 
waalimu ni wakatili sana, ndio maana huwa hawafanikiwi maishani. wamejaa roho mbaya na wivu tu. wachache sana wanafundisha watoto kwa moyo, zaidi sana hao watoto ni sisi wenyewe tunawasaidia majumbani, ndio maana huwa wanawapa hata homework maeneo ambayo hawajafundisha, ati watoto wakafanye homework. wanachapa watoto sana.
Ushawahi kufundisha?
 
Yaani mtoto wangu nimwambie alale chini au anyoosje mkono? Aisee , ni bora umchape tu yaishe na sio kumharass kisaikolojia
 
Back
Top Bottom