Kwanini mtu akiua huwa anaandamwa na wenge karibu hapa fundi samico nikujuze

Kwanini mtu akiua huwa anaandamwa na wenge karibu hapa fundi samico nikujuze

Au avuke tu mpaka aende hapo Congo.
Ukimuua "an innocent person" unakuwa mentally unstable. Acha ubishi ndio maana askari 80% wanatumia Pombe na sigara kupunguza wenge kwa sababu kazi zao ni za kuua na kudhulumu raia.

Yule askari aliyejichimbia karibu na kuchonga jeneza lake, unafikiri kapenda?? Lile ni wenge.
 
Ukimuua "an innocent person" unakuwa mentally unstable. Acha ubishi ndio maana askari 80% wanatumia Pombe na sigara kupunguza wenge kwa sababu kazi zao ni za kuua na kudhulumu raia.

Yule askari aliyejichimbia karibu na kuchonga jeneza lake, unafikiri kapenda?? Lile ni wenge.
Ulifanya lini na wapi utafiti ukajua 80% ya askari wanatumia pombe na sigara na kwamba matumizi hayo yamesababishwa na kuua watu wasio na hatia??
 
Sisi waganga tunacho chombo cha uchunguzi ...alipouwawa mtu chota ule mchanga tuletee tukipiga ramli tunaona kupitia mchanga
Waganga siku hizi mmeadvance, hadi huku mpo, zamani tuliamini kumpata mganga (wa kweli) ni mpaka uingie huko ndani ndani.
 
Siyo kila jambo halali lazima liwe na marejeo kutoka kwa wachunguzi wa kale ndipo uthibitishe kwamba ni kweli au uongo!

Yapo Mambo mengi ya uongo yamethibitishwa kwa marejeo ili kuupotosha umma na baadhi ya mambo ya ukweli yalifutwa au kufichwa kwa kutokuandikwa popote duniani ili kuficha jambo flani.
Hivyo kuuliza marejeo kwenye kila jambo lengo nikuifunga akili yako isiwaze inje ya box ili ubakie kuamini kile kile kilichopo.

Tuendelee na mada yetu
Kwanini mtu akiua hupatwa na wenge?

Iko hivi mazingira ya huu ulimwengu yote yana mawasiliano!

Yaani kila kitu unachokiona kuanzia mchanga, mawe, udongo, mimea, wanyama, majengo yaaani kila kitu unachokiona chenye uhai na kisicho na uhai vina mfumo wa mawasiliano ambao mwanasayansi hawezi kuuchunguza kisayansi!

Naona wengi hawajaelewa, iko hivi tazama mfano huu:

Kwa mfano mwizi au kibaka au mtu yoyote anaepewa mzigo wa mtu halafu akaiba!
Mazingira papo kwa papo Humrebo mtu huyo kuwa Siyo mwaminifu kwa maana hiyo hata uende wapi, ile rebo ya kutokuwa mwaminifu inakuandama kama vile inzi anavyotembea na mzoga.

Popote utakapofika kwenye nafasi ya kuaminiwa HUTAAMINIKA KAMWE Labda ulazimishe kwa kuhonga au ulazimishe kuaminika kinguvu!

Hii elimu hata vibarua wangu katika ufundi kabla sijamchukua kijana yoyote kufanya kazi pamoja nami huwa namwambia HAKIKISHA USICHUKUE MALI YA BOSI kama hajakupatia kama unataka mafanikio yako!

Kama katika maisha yako unaona kila ukiomba nafasi ya kuaminiwa HUAMINIKI Tambua ya kwamba yale mazingira YALIKUREBO kwa makosa uliyowahi kufanya zamani na UKAPOTEZA UHALALI wa mazingira kukutetea katika nafasi ya kuaminiwa!

Mazingira yana macho, masikio, mdomo, mikono, tumbo n.k

Kwa ufupi mazingira yanafanya kazi zote kama binadamu, YANATOA USHAHIDI Kwa anayestahili HAKI au HUKUMU.

Ukiua Mtu morogoro na mazingira yakashuhudia hayo mauaji HATA ukimbilie wapi unatambulika kwa rebo ya muuaji!

Hivyo hata kama hautakamatwa leo lakini kila wakati mazingira utahisi yanakuzomea au yanakusema na ndiyo hapo utajiona kama umeingiwa wenge!

Mfumo wa mazingira una network ambayo isiyo ya kawaida.

Siku mwanasayansi ataekuja kugundua kifaa cha kuyasikiliza mazingira kama shahidi namba moja ndiye atakua tajiri namba moja na dunia itakuwa sehemu salama kuanzia hapo hatuta hitaji upelelezi wa polisi tena.

Kwanini mtu anaeua hupatwa na wenge inaendelea?

Mfumo wa Mazingira unafanya kazi kwa mzunguko (recycling).

Roho ni mfumo wa kila kiumbe ambacho kinahitaji uhai!
Roho ni kama simkadi au microchip
Roho Inapokuwa ndani ya kiumbe huwepo kwa kazi maalum ya kukiwezesha hiko kiumbe kufanya kazi!

Na mwenye mamlaka ya kuondoa roho huondoa kwa utaratibu maalum endapo mwili umechoka au hauwezi kusomana na roho.

Na roho hiyo inapotolewa huwekwa kwenye kiumbe kipya! (Recycle) kwa utaratibu.
Sasa wewe unaooua ghafla wakati mazingira hayaja andaa mwili mpya ile roho ikatumike,

Unakuwa umeyakosea sana mazingira kwasababu hayajaandaa mwili na utawajibika kwa kosa hilo.

Je, KUUA INARUHUSIWA?

Ndiyo kuua inaruhusiwa, LAKINI LAZIMA UTOE TAARIFA KWA MAZINGIRA kwamba
1. Unaua kwa FAIDA ya mazingira yenyewe yamekuagiza
2. au kwa faida kitoweo kwa maana unachokiua lazima ule.
3. Kuua kwa kujihami

Ndiyo maana baadhi ya dini zinazuia KUUA!
Hii si binadamu, bali hutakiwi kuua kiumbe chochote kama hakipo kwenye hizo kanuni tatu.

Unapo taka kuua kwa ajili ya chakula unatakiwa ukisemee hiko kiumbe kwamba nakuua nipate kula n.k

Kama huniamini nenda kawagonge hata mbwa waliopumzika kwa makusudi ndipo utakuja kunielewa baadae.

Wewe hapi ulipo ulikuwa Roho ya kiumbe flani kilikufa roho ikapachikwa kwako, na wewe ukifa roho yako itapachikwa kwa kiumbe chochote hadi pale ROHO yako izunguke kwenye viumbe wooote waliopo duniani ndipo itahukumiwa!

Ndiyo maana waliokufa zamani na watakakufa baadae SIKU YA HUKUMU itakuwa moja baada ya kumaliza mzunguko wa roho yako!

Ukiwahudumia viumbe wenzako vizuri unajiweka mazingira ya roho yako kutunzwa katika kiumbe kijacho!

Kuna watu muda wote wanatabia ya kufoka foka tu kumbe zamani roho yao ilikuwa MBWA na hawataki kubadilika.

Kufupisha somo hili naomba kuishia hapa.
Mada nyingine nitaeleza nani amuoe nani na utambuaje!
Hapo umetuingiza cha kike. Mbona Kagame, M23, Wapalestina, Osama, Al-shabab, Boko Haram n.k hawana wenge?
 
Hapo umetuingiza cha kike. Mbona Kagame, M23, Wapalestina, Osama, Al-shabab, Boko Haram n.k hawana wenge?
Wana nawenge makubwa sema tu hujui, kung'ang'ania madarakani unazani wanapenda, ni ishara ya mawenge
 
Ulifanya lini na wapi utafiti ukajua 80% ya askari wanatumia pombe na sigara na kwamba matumizi hayo yamesababishwa na kuua watu wasio na hatia??
Pole kama umeshawahi kuua! Tafta namna ya kupata na mazingira kama ulishiriki mauaji uko rebodi utawajibika kwa hilo siku moja hata kaa siyo leo
 
Jamaaa,anadai roho ya mtu lazima ipitie ndani ya kila kiumbe duniani,Sasa Hadi chawa,kenge,nguruwe nk ??
Hii sii kweli
Lazima ipitie kila kiumbe, hadi inzi wanaoishi siku saba na kufa, mzunguko woooote lazima upitie ndipo HUKUMU INAFUATA
 
Lazima ipitie kila kiumbe, hadi inzi wanaoishi siku saba na kufa, mzunguko woooote lazima upitie ndipo HUKUMU INAFUATA
Hii elimu ya wapi hii,mhhhhj,Mimi najua baada ya kufa mwili huu tulio nao,kifuatacho Ni hukumu,hakuna jingine
 
Always make ur hands clean

Ukishaua MTU /WATU unapoteza utulivu wauaji nadhani wataelezea vizuri wakija hapa .


Ila kuua MTU ni kitu kibaya hasa ukiua kwa makusudi you create a bad karma
 
Back
Top Bottom