Kwanini mtu aliyeanza ARVs akija kuacha ana kufa?

Kwanini mtu aliyeanza ARVs akija kuacha ana kufa?

Makosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
1,183
Reaction score
2,622
Nimejiuliza maswali mengi sana Ila sijapata jibu, Luna kijana tumemzika leo kwa bahati mbaya alikuwa ni HIV Positive na alikuwa anatumia hizi dawa lakini baada ya kuona amekuwa na afya nzuri aliamua kuacha kimya kimya mpaka ilipokuja kugundulika.
Sasa swali langu wataalamu hizi dawa zina kitu gani kinachofanya mtu aliyezikacha afe ghafla?
 
Sasa kaacha kutumia dawa,lazima load ya virusi iongezeke kwenye bloodstream.Na hapo lazima virus wasambaratishe cells.Kitakafochofuatia hapo ni kukosekana kwa kinga kabisa so magonjwa and eventually kifo.
 
mimi binafsi naona; unakufa kwa sababu binadamu wa kawaida huwezi kula dawa daily...zinajijenga ndani ya mwili, na sio Arv tu kun best yangu ameugua ukichaa anatumia dozi,ambayo ankunywa daily mwaka wa 3 sasa na sio chini ya dawa tano kwa siku
sasa anapotumia akili inatulia anafanya mambo yake kawaida anafanya kazi na huwezi kujua chochote, kosa aziache ukichaa unarudi mara2
nahisi ni kwasababu dawa zimejijenga mpaka zimeshakua mfumo wa mwili sasa, bila zenyewe huwezi
kwahiyo;
zile dawa ni sawa n chakula,kwasababu unapozinywa kila siku zinaenda kuwa moja ya basic need kwa mgonjwa kwamba akikosa, kwa muda fulani kama vile ukikosa chakula ndani ya week labda unakufa.
 
Kuacha kutumia ARV'S unawapa virus nafasi ya kujenga resistance, wanatoka mafichoni na kuingilia CD4 s ili kuzaliana, CD4 ndiyo kinga yako kama lilivyo jeshi la ulinzi kwenye nchi. Virus wenye resistance wananguvu sana na muda si mrefu wanakuwa wamezaliana na CD4 kupungua.

Kwakifupi low levels of CD4 and high levels of viraload = AIDS.
 
Back
Top Bottom