Kwanini Mungu akikuchagua usaidie watu anakupa Roho wa Bwana(holy spirit)?

Kwanini Mungu akikuchagua usaidie watu anakupa Roho wa Bwana(holy spirit)?

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
Mathayo 12:18
Tazama, mtumishi wangu niliyemteua; Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

Mungu akikuchagua kuhubiri neno lake au kusaidia jamii(nation/world) anakupa roho wa bwana(holy spirit).

kazi ya roho wa bwani nin?

1.hekima, roho wa bwana anakusaidia kuwa mtu mwenye hekima, hekima kwenye kutoa maneno yako, hekima kutumia kwa wanao pinga injiri au ushauri wako

mfano negative comment, hekima ni kitu muhimu sana unapofanya kazi ya kusaidia watu maana kila mtu ana uelewa tofauti juu ya maisha na Mungu.

Mathayo 13:54
Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?


2.Uwezo wa uponyaji(healing), roho wa bwana pia anakusaidia kuwa na uwezo wa uponyaji kupitia maneno(ushauri) wako mtu anapata tumaini,
kujua trauma(vifungo) kwa watu.

kutatua matatizo ya watu kama bwana yesu alivyokuwa anaponya viwete, viziwi, anatoa pepo kwa watu hii yote ni msaada wa roho wa bwana(holy spirit).soma(Mathayo 12:22) na
Mathayo 12:28
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.


3.Ufahamu wa kiroho(discernment), roho wa bwana ukiwa naye anakusaidia kujua maeneo au watu ambao sio sahihi kwako,

watu wote wenye roho wa bwana wanakuwa wana beba light hivyo wanajua mazingira au watu wenye nguvu za giza(dark energy) .

4.Lakini pia roho wa bwana anasaidia kuelewa vifungu wa bibilia,
hivyo ni vizuri kabla ujasoma bibilia omba Mungu akuongoze uelewe ni kitu gani ana maanisha na kinakusaidiaje katika hali ulionayo kwenye maisha yako.

5.Watu wenye roho wa bwana inawafanya kuwa wapole na unyenyekevu,

Mungu akiwa anafanya mabadiliko ya maisha yako kwa ajili ya kukuinua lazima utapitia changamoto zitakazokufanya uwe mnyenyekevu

Mathayo 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
 
Mungu akiwa anafanya mabadiliko ya maisha yako kwa ajili ya kukuinua lazima utapitia changamoto zitakazokufanya uwe mnyenyekevu💪🏿📌🔨
 
Back
Top Bottom