Mkuu kifupi hakuna mwenye uwezo wa kukujibu sababu iliyopelekea Mungu kutoliangamiza hilo dubwana shetani, na badala yake (Mungu)akaamua tu tuishi nalo.
Ukiangalia mijadala mingi humu jamvini watetezi wa uwepo wa Mungu, hawajafua dafu kuangusha majibu maridhawa, pindi wanapobanwa juu ya nyanja mbalimbali zimhusuzo Mungu,wamekuwa hawajitoshelezi kimajibu.
Ndiyo dunia tuliyopewa..Acha kuitesa akili yako kwa maswali yaso majibu.Ishi.
Mungu aliamua kutufungia chumbani kimoja na joka na akatutaka tulipige na kulishinda, sasa usipolishinda, jehanamu itakuwa makao yako kama inavyosisitizwa.
Maswali ni mengi kuliko majibu.
Nyerere alipoulizwa juu ya Mungu..alijibu"Tumshike Mungu ili kama kweli tutamkuta baada ya kufa basi tusiwe na hasara, na kama hatutamkuta kama tulivyoelezwa bado tu hakutakuwa na hasara.