Kwanini muujiza wa kwanza wa Yesu ulikuwa kubadilisha maji kuwa divai na sio kutengeneza Biblia?

Kwanini muujiza wa kwanza wa Yesu ulikuwa kubadilisha maji kuwa divai na sio kutengeneza Biblia?

Kama pombe ni mbaya kwanini Yesu aliitengeneza kwanza na hakutengeneza Biblia?

Nawakaribisha wana zuoni mliokomaa katika mjadala huu.
Kwa sababu Biblia haikuwa bado ipo kama kitabu. Wakati Yesu alianza huduma yake, Agano Jipya lilikuwa halijaandikwa. Waandishi kama Mathayo, Marko, Luka na Yohana waliandika baadaye, baada ya maisha, kifo na ufufuo wa Yesu.

Muujiza wa kwanza wa Yesu ulikuwa kubadilisha maji kuwa divai kwenye harusi ya Kana. Muujiza huo haukuwa tu kuhusu divai, bali ulikuwa ishara ya kuonyesha utukufu wake, kuleta furaha, na kuanza kuonyesha mamlaka yake kwa watu.

Kwa hiyo, swali "kwa nini hakutengeneza Biblia?" linatokana na kulinganisha mambo ya nyakati tofauti. Yesu alikuja kwanza kuishi, kufundisha na kuwa mfano; maandiko ya Agano Jipya yaliandikwa baadaye na mashahidi wa maisha yake.

Hivyo, Biblia ni ushuhuda wa Yesu—si kitu alichokuja kukitengeneza kwa muujiza.
 
Kama pombe ni mbaya kwanini Yesu aliitengeneza kwanza na hakutengeneza Biblia?

Nawakaribisha wana zuoni mliokomaa katika mjadala huu.
Maswali mengine baada ya kusoma kabla ya kuyajibu unaanza kwanza kucheka maana yana full comedy.

Ilifaa kwanza kufahamu Biblia ni nini?
Biblia ilitokana na nini?
Mara ya kwanza neno Bibilia lilianza kutumika wapi?
Neno Biblia asili yake ni lugha gani?
 
Kwanini neno Biblia halimo kwenye Biblia (hamna mstari wowote kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo umetaja jina Biblia)?
 
Maswali mengine baada ya kusoma kabla ya kuyajibu unaanza kwanza kucheka maana yana full comedy.

Ilifaa kwanza kufahamu Biblia ni nini?
Biblia ilitokana na nini?
Mara ya kwanza neno Bibilia lilianza kutumika wapi?
Neno Biblia asili yake ni lugha gani?
Muuliza swali mtego wake uko hapa
Kwanini Yesu hakuanza na kutengeneza kitabu cha muongozo wa yale maneno matakatifu ya Mungu anayofundisha akaanza na vitu kama kutengeneza divai?
 
Muuliza swali mtego wake uko hapa
Kwanini Yesu hakuanza na kutengeneza kitabu cha muongozo wa yale maneno matakatifu ya Mungu anayofundisha akaanza na vitu kama kutengeneza divai?
Kimsingi, Yesu mwenyewe alisema wazi kuwa hakuja kuitengua Torati au Manabii, bali alikuja kuikamilisha (Mathayo 5:17). Torati inajumuisha vitabu vitano vya kwanza vya Biblia ambavyo kimapokeo vinajulikana kama Vitabu vya Musa. Hata hivyo, kulingana na uchambuzi wa kihistoria na waandishi wa Biblia, vitabu hivyo havikuandikwa kikamilifu na Musa mwenyewe pekee, bali vilikusanywa na kuhaririwa kupitia mapokeo na waandishi mbalimbali kwa karne nyingi.

tukirudi kwenye uzi inafaa kueleweka pamoja na kwamba Yesu alianza huduma yake ya miujiza kwa kubadilisha maji kuwa divai huko Kana ya Galilaya, hakuwahi kuandika kitabu chochote cha Biblia mwenyewe. Kwa Sababu kuu zifuatazo:
1. Ujumbe wake ulikuwa wa ana kwa ana na Vitendo: Lengo kuu la Bwana wetu Yesu Kristu lilikuwa kufundisha kwa njia ya mdomo, kuishi mafundisho yake, na kutimiza kazi ya wokovu kupitia kifo na ufufuo wake. Kwa hiyo yeye alichagua kuwekeza maisha yake ndani ya wanafunzi wake badala ya kuandika andika.
2. Kuweza kufikisha ujumbe ulio na uhai badala ya photocopy. Maana yake ni nini, Yesu mwenyewe ndiye anayetajwa kuwa "Neno Aliyefanyika Mwili" (Yohana 1:14). Kazi yake haikuwa kuleta kitabu kipya cha sheria, bali kuwa utimilifu wa sheria hiyo na kuleta maisha mapya.
3. Alikusudia piaujumbe wake Kuenezwa kupitia Mashahidi au Mitume: Inaeleweka Yesu aliwakabidhi mitume na wanafunzi wake jukumu la kushuhudia yale waliyoyaona na kuyasikia, soma Mathayo 28:19-20. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, wanafunzi hao na waandishi wa Agano Jipya ndio waliokuja kuandika Injili na Barua nyingine baadaye ili kuhifadhi ushuhuda huo kwa vizazi vinavyofuata vya wakina Bujibuji
 
Muuliza swali mtego wake uko hapa
Kwanini Yesu hakuanza na kutengeneza kitabu cha muongozo wa yale maneno matakatifu ya Mungu anayofundisha akaanza na vitu kama kutengeneza divai?
Wewe ndio umeelewa vyema swali langu
 
Back
Top Bottom