pulex
JF-Expert Member
- Nov 3, 2023
- 536
- 2,213
CCM imeamua kujizika kwa kuruhusu uyu Samia kugombea URAISI, CCM ilikuwa inaenda kufa zaman, Magufuli akaja kuizindua kama zile mashine za kustua moyo mtu anapotaka kufa, Moyo ukawa umestuka kwa mbali uhai unakuja, mara Samia akaingia, Moyo unaenda kuzima, na anagombea awamu hii kwa mabavu ndo kabisa anaenda kuizika CCM, maana awamu ijayo kwa asilimia 💯, inaenda kuyatinganya zaidi, damu zitamwagwa sana, ufisadi utashamiri mara mia ya sasa.Naona kama vile kila siku zinavyosonga mbele kama vile kampeni za CCM zitakosa mvuto kabisa.
Hapa sababu kubwa ni Maza na Nchimbi kutokuwa waongeaji au wapiga kampeni wazuri.
Kwa kweli Maza anaoongea kama vile anahutubia mkutano wa ziara badala ya kuongea kama vile anapiga kampeni.
Na haya mambo ya matrector million 10, akina Kangi Lugola kukata viuno jukwaani, mwingine kudai Watawaloga wanaomkataa Maza inawafanya waonekane hawana sera wala jipya kwa miaka 5 ijayo.
yaani namuonea huruma uyo atakayekuja kugombea Uraisi ikiwa Chadema wako huru, na mambo kurekebishwa..yaani hii sioni CCM ikidumu kwenye vizazi vichache baadae, kwasasa inatumia jeshi ila hii ina mwisho.