Nimejikuta nimekumbuka mbali!!
Wakati hayati Kigoma Malima anaagwa pale Viwanja vya Mnazi Mmoja ili akazijwe huko kwao, ghafla manyunyu yakaanza wakati wanajiandaa kubeba jeneza lenye mwili kupakia kwenye gari.
Rais Salmin Amour "Komandoo" alikuwa ni mmoja ya waombolezaji na hakusita kujumuika na wananchi waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho pale Mnazi Mmoja.
Sasa kwakuwa kuna manyunyu, mlinzi wa Rais, akatoa mwamvuli na kumkinga Rais Salmin na manyunyu ya mvua.
Kitendo hiko kikapingwa na Sheikh Ponda akisema iweje wengine mkingwe na mvua na wengine tuloe hali ya kuwa wote ni binadamu na tupo msibani.
Basi Salmin Amour akamuamrisha mlinzi wake ashushe mwamvuli na aloe kama wengine!!
Hapo ndipo macho na masikio ya watanzania walipoanza kumjua Sheikh Ponda!!