Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kuna mambo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya nchi hii yanashangaza sana.
Mchoro wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaani Kwangwa ulibuniwa mwaka 1975 na baadae mwaka 1977 ujenzi ulianza.
Baadae mwaka huo wa 77 ujenzi wa hospitali hii iliyoko Musoma, ulisimama na kendelea kidogo kabla ya kusimama rasmi mwaka 1980 na huo ndo ukawa mwisho wa kazi ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo kungeifanya kuwa moja ya hospitali kubwa za mkoa za Tanzania ikiwa na majengo makubwa matatu, jengo la wazazi yaani "Wing C" na jengo moja kubwa la "Wing B" lenye vitanda na jingo la "Wing A" ambalo litakuwa ni la matibabu maalum.
Ni miaka miwili ilopita ambapo raisi John Magufuli aliamua kuelekeza fedha kiasi cha shilingi bilioni 15 ili ujenzi wa hospitali hiyo ukamilishwe.
Na hiyo ilikuwa ni baada ya ushawishi wa mkuu wa mkoa Adam Malima na mkuu wake wa wilaya pamoja na ufuatiliaji wa Waziri Mkuui na wazri wa Afya.
Ujenzi huo unatarajia kukamilika rasmi mwezi August mwaka huu na ujenzi bado waendelea chini ya usimamizi wa shirika la nyumba la taifa NHC.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba imewachukua maraisi watano tangu ujenzi wa hospitali hii usimame yaani hayati raisi Nyerere mwenyewe, Ally Hassan Mwinyi, Benjaminui Mkapa, na raisi Kikwete ndipo raisi Magufuli aamue kutenga fedha za ujenzi huo.
Licha ya hivyo, wakuu wa mkoa wapatao 16 ambao wamepita kusimamia mkoa wa Mara bila hata kupata wazo la kutembelea gofu la hospitali hii na kuliacha kama lilivyo.
Jengo la "Wing C" linatarajia kukamilika hivi karibuni na litakuwa likihudumia mama na mtoto.
Hivyo, hatua ya Rais John Magufuli kuidhinisha fedha za kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo kiasi cha shilingi bilioni 15 ni ya kizalendo na inahitaji kupongezwa na kuungwa mkono.
Huduma ya Afya katika nchi yoyote ile hutegemea sana miundombinu ya hospitali na vituo bora vya afya.
Serikali imekuwa ikijitahdi kuelekeza fedha za maendeleo katika maeneo haya muhimu ya Afya na Elimu kwani masuala haya mawili ni moja ya mihimii ya ustawi wa taifa kimaendeleo na kiuerevu.
Hata yule mtu aliezaliwa mwaka 75 sasa hivi ana miaka 43!
Je, ni sababu zipi ziliwezesha kutokamilika kwa hospitali hii?
Je, wakuu wote hao wa mikoa waliiona jengo la gofu la hospitali hiyo na walichukua hatua gani?
Je, kutoendelea kwa ujenzi wa hospitali hii kumetokana na sababu za kisiasa?