Kwanini Mwalimu Nyerere hakujenga hospitali ya mkoa wa Mara? Ujenzi ulisimama kwa miaka 40 na sasa kukamilika mwaka huu!


mkuu, hata zaire ilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha namibia inakuwa huru pamoja na Africa ya kusini tena marekani ambaye ni mmoja wa hao mnaowaita mabeberu alitoa misaada mingi tu kwa zaire ikiwemo ya ki uchumi kutokana na juhudi za zaire kutetea uhuru , hata uganda pia ilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha zimbabwe inakuwa huru tena amin ali propose military intervention kabisa lakini uchumi wa nchi hizi mbili ulikuwa imara kuliko sisi
ni wakati watanzania tuseme ukweli pale tulipokwama tuache kujificha kwenye kichaka cha kupambania uhuru


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.

Wakati wazo la kujenga hospitali linabuniwa wananchi walianza kuchangishwa pesa za ujenzi huo, siku ya kwanza michango ilihamasishwa na marehemu Joseph Kizurira Nyerere aliyekuwa mbunge akiwakilisha mkoa wa Mara, wakati huo kulikuwa na mfumo wa wabunge wa mikoa,mbali na wabunge wa majimbo.
Wananchi walichanga pesa pale uwanja wa Karume ,kila mtu kwa kiwango alichokuwa nacho,pia walikuwapo wafanyabiashara mbali mbali wa Musoma wakatoa michango yao.
Hapo ukaundwa mfuko wa ujenzi wa hospitali ya Mkoa ya Kwangwa,chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Ili kupata mapato zaidi ,bidhaa mbali mbali kama vile mafuta, vinywaji nk.viliongezwa bei kwa ajili ya kutunisha mfuko wa ujenzi wa hospitali na ujenzi ulianza,ila sijui serikali ilichangia kiasi gani kwa wakati huo.
Tatizo kubwa la ufisadi lilijitokeza, mfuko ulishambuliwa na mchwa hakuna mfano,na hapo ndio ujenzi ukayumba na hatimaye kusimama jumla.

Nashangaa sana,maelezo yote yametolewa lkn ukweli huu haujatajwa ,Mungu atusamehe.
Hatimaye makato mbali mbali kwa ajili ya ujenzi wa hospitali yalisimamishwa na ndio kikawa kifo rasmi cha ujenzi huo.

Wengi wa mafisadi waliolamba pesa ya ujenzi wa hospitali ya Kwanga walikwishatangulia mbele ya haki, natumahi wanaendelea kujibu huko kwa waliyoyatenda.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa hiyo tunaanza kupata sababu :

1. Ubadhilifu na ufisadi.

Haya tuendelee...
 

..Je, mikoa yote Tz ina hospitali za mkoa?

..au wewe uko interested na mkoa wa Mara peke yake.
 
Kwangwa MWL Nyerere Memorial Medical centre kama inavyoitwa kwa sasa, ilianza kujengwa miaka ya 1977 kama wadau wengine walivyosema hapo juu, ujenzi ulianza kwa kutumia michango ya wananchi na watumishi wa umma nao walikua wakikatwa sehemu ya mshahara ili kufanikisha ujenzi.

Baadae ufisadi ulianza kwenye michango na kupelekea ujenzi kusimama kwa muda mrefu, kanisa Katoliki kiliingilia kati ili kuendeleza ujenzi lakini haikupata sapoti kubwa sana kutoka kwa serikali ili kuendeleza ujenzi.
Awamu ya kwanza wa Jakaya Kikwete, Lowasa akiwa waziri mkuu alipenda sana ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa ijengwe na kumalizika lakini alipata kikwazo kutoka kwa Wanamgambo waliokua wakimpinga wakiongozwa na RIP Samwel Sita (Mungu amlaze panapostaili) kisa ni urais tu. Si unajua angeonekana amemaliza Hospitali kwao Nyerere bwana....credit
Figisu ilianza adi Washauri waliokua site na ujenzi ukiwa unaendelea ofisi ya RAS ambao ndo walikua Washitiri wakala Pesa ya mradi kilichopelekea Wing B kutokumalizika, Washauri wakatupiliwa mbali na wakaondoka na mradi ukasimama.....watu walipiga pesa ndefu kuliko pesa uliowekwa kwenye ujenzi....(RAS Mara walikua mafisadi balaa).

Mwaka 2017 mwanzoni TBA walipewa fungu ili waweze kumalizia Wing B, baada ya kumalizika kwa Wing B na Hospitali zote kurudishwa kua chini ya Wizara ya Afya ikaonekana kua Hospitali ya Kwangwa kwasasa haikidhi vigezo vya sera za sasa za Wizara wa Afya hivyo kuna sehemu lazima zibomolewe na kuifanyia marekebisho.
Mwaka 2018 TBA wakapewa fungu la kuendelea na ujenzi Phase VI kwa kuanza na Wing C kuifanya wudi ya wazazi, wataalama wakakaa na kuiboresha ili iendane na sera ya sasa ya Wizara ya Afya. Baada ya Phase IV kuisha sasa Wing A na B zinaendelea kujengwa na NHC kwa phase VIII.

Iwapo Hospitali zisingerudishwa kua chini ya Wizara ya Afya, Hospitali nyingi zisingeisha make ofisi za RAS bado zimejaa siasa na RUSHWA kubwakubwa sana.
 
Mngeweka picha ya hilo jengo ningewaelewa Zaidi
 
Upo sahihi kabisa kumbuka budget ya nchi inaanza kutumika july sasa 1978tupo vitani 1980mpaka1982 Njaa 84 mkuu ana ng’atuka 85mpaka 95ruksa tupo kwenye mpito wa kiuchumi na kisiasa
Mimi nadhani baada ya Ruksa walio fuata wangeuliziwa lkn sio wezee wetu Mchonga na Ruksa
Lkn kanda ya ziwa kuna rufaa bugando wananchi walipata huduma,za juu kama vile kanda ya kaskazini kuna KCMc kanda ya nyanda za juu kuna Mbeya ruffaral hosp na pwani ni muhimbili kati kuna benjamin mkapa
Awamu ya Jk wapil yeye alideal sn na shule na maabara barabara mzee Jpm yeye ni hosp kwenye vijiji
 
Zaire ile ya Mobutu aliyemuu Patrice lumumba? Na uganda ile ya Amin iliyokuwa inachinja watu kama mbuzi? Au umekengeuka?
 
Wakyura tupo imara hatuumwiumwi kizembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maendeleo bora kabisa kwa Mtanzania

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Marais waliofuata baada ya NYERERE km NYERERE mwenyewe waliangalia zaidi maslahi ya taifa..... huyu wa sasa ni aibu kubwa aliyonayo baada ya kuifanya chato km nchi kamili ili ionekane eti anakujali kwa BABA wa TAIFA kumbe anahalarisha uharamia wake........
Sio tu hospitaliz Nyerere hakujenga airport mara, hakujenga international airport, hakupele mbuga kijijini kwake, hakujenga ofisi za kisasa za tra wala hakuwahi kufanya utafiti wa kufungua tawi la benki kijijini kwake (rejea hotuba ya Kimei crdb walivolazimishwa kufungua tawi chato wkt hapafai).......haya yote kayafanya rais wa wanyonge ********....
 
Vita ya Kagera ni moja ya sababu zilizopelekea Mwalimu Nyerere kutoendelea na ujenzi wa hiyo Hospitali maana nchi iliyumba sana kiuchumi hadi alipoingia Mzee Ruksa mwaka 1985 kidoogo kukawa na mabadiliko hadi kufikia akina Kikwete lkn nani alikuwa na habari hiyo badala ya kujenga Bandari Bagamoyo...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaandika mengi tu, lakini kwa ufupi ni kwamba ufisadi na ubadhirifu ndio ulikwamisha ujenzi wa hospitali hiyo,pesa ilikuwapo ikitokana na makato mbali mbali, badala ya kujenga hospitali wahusika wakajenga matumbo yao.

Mfano mzuri ni jinsi mashirika mengi ya umma yaliyoanzishwa kwa juhudi za serikali ya awamu ya kwanza yalivyotafunwa na wajanja wachache na kusababisha kufilisika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…