Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

😂😂😂😂Haoni...duu hivi mbona hivi vitu vinatokea kwenye hadithi za watu tu na sio maisha tunayoishi jamani
 
Mwamposa anadili na mambo ya Giza,

Sasa unaumwa malaria wakati si mambo ya giza.mahospitali kunamda unaumwa madaktari wanakwambia jiongeze,nenda kienyeji

Mwamposa anadili na mambo ya Giza,sio magonjwa ya kawaida
Mambo ya Giza na magonjwa ya kawaida unatofautishaje? Mbona wanaenda watu wa ukimwi, vilema etc si medical problems zile...mambo ya Giza ni Nini Sasa?
 
Na madaktari,manesi na wafamasia wataishi vipi sasa
 
Mkuu nasikia kuna dini nyingine nyingi tu zaidi ya hizi mbili ambazo zinatumia Bible na Quran, hizo dini nyingine zinatumia vitabu gani?
Navyosema dini sio lazma iwe organized religion..hata babu zetu walikuwa na dini zao...ila the oldest religion ni Hinduism coz Ina maandiko yanaenda miaka 3000 BC
 
Mwamposa akienda Mbeya wanaopona wanatoka Dar au sehemu zingine, akirudi Dar wanaopona wanakuwa wanatokea Mbeya au sehemu tofauti. Umewahi sikia mtu wa Kawe hapo hapo kapona na katoa ushuhuda? Au kawe hakuna wagonjwa?
 
Kama Mwamposa ana uwezo wa kuponya angeponya tu wagonjwa bila hiyo CONDITION ya imani.

Huwezi kuniambia wale watu wote Ocean Road waliolala hawana imani hata kidogo.
Ukitaka kujua vizuri hao watoa ushuhuda jiulize kuna mkazi wa hapo hapo kawe aliyepona? Ina maana kawe hakuna wagonjwa au wote hawana imani
 
Sasa si aende huko Ocean road akawaponye hao wanaoumwa maana tayari yamewakuta
 
Mwamposa anadili na mambo ya Giza,

Sasa unaumwa malaria wakati si mambo ya giza.mahospitali kunamda unaumwa madaktari wanakwambia jiongeze,nenda kienyeji

Mwamposa anadili na mambo ya Giza,sio magonjwa ya kawaida
So ni mshirikina?
 
Ache wivu. Ukiona anafaidi sana na wewe jaribu. Bora huyo watu wanamfuata wenyewe kuliko nyie mnaoiba kwa kalamu ofisini na kujiona wasafi kuliko wengine.
 
Navyosema dini sio lazma iwe organized religion..hata babu zetu walikuwa na dini zao...ila the oldest religion ni Hinduism coz Ina maandiko yanaenda miaka 3000 BC
Sawa mkuu, ila hujasema vitabu vinaitwaje? Au havina majina?
 
Sasa si aende huko Ocean road akawaponye hao wanaoumwa maana tayari yamewakuta
Kwanini usiende kuwahimiza walioko ocean road waende? Hata wengi walioponywa na mitume na manabii including Yesu walikua wanamfuata alipo. Kiponywa ni suala la imani. Kumfuata mtu ni dalili ya kumlazimisha.
 
Mkuu so Lazaro alimfata Yesu ili amfufue au Yesu alimfata Lazaro?
 
Pale unapona kama ulirogwa. Kipindi nahudum hospitali ya kata Kuna mama alikuja kuleta mwanae mwenye child disorders ambaye alishindikana madhabahu yote daresalaam hii.

Kwa suguye, kuhani Musa sijui mwamposa kote walienda. Na hata hum Kuna wana jamii forum wamepata kazi kwa kupeleka vyeti pale.. mmoja wapo kwenye kila mada za uchawi anapingaga kuwa uchawi hakuna
 
Lazaro alikua hospitalini?
Umesema mwenye uhitaji ndiyo anamfata nabii kwani nabii akimfata itakuwa kama anamlazimisha. Ndiyo maana nikakuuliza kama Lazaro alimfata Yesu ili afufuliwe au Yesu alimfata Lazaro?
 
Inverted Cross phylosophy.
Zamani watumishi wa Mungu waliwafuata na kuwalisha na kuwaponya maelfu ya watu,siku hizi maelfu ya watu wanawafuata waliko watumishi wa Mungu.
 
Maumivu wanayoyapata hiwezi waletea usanii.
Anawazuga wale waliomaliza shida zao za mhimu,yeye anachukua tu chenji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…