To propose.... kupiga magoti sio utaratibu wa kiafrika, na kupropose kwa kumvalisha pete ya uchumba sio utamaduni original wa kiafrika. Kwa makabila mengi utaratibu ilikuwa unawatuma wazee/washenga, then binti anaitwa na kuulizwa kama anakufahamu na anakukubali, akisema ndiyo basi inapangwa siku ya MAHARI, na mkishalipa mahari tu basi binti anakuwa officially mkeo. Ndo maana kwa makabila mengi, after send off upande wa mwanaume huomba familia ya mwanamke iwatunzie mke wao mpaka siku ya harusi ya kidini.
Kwa nini mwanaume kupiga magoti? Kwa mujibu wa utaratibu wa wenzetu, kupiga magoti kunamaanisha mambo mawili.
1. Kuonyesha kwamba wewe ni gentleman
2. Na ambalo ndo zito zaidi, unaonyesha kwamba kwa dakika hizo mbili tatu utakazokuwa umepiga magoti, mdada anakuwa na mamlaka kushinda wewe, maana jibu lake ndo litakalobeba mustakabali wa maisha yako.
Kwa sisi Wahehe ni mwiko kumpigia magoti mwanamke, so hata mimi sikupiga magoti.
Lakini, maadam tumeshaingiza sana Mungu kwenye tamaduni zetu, soma mazingira yako then act accordingly. Wanasema, WHEN IN ROME, DO AS THE ROMANS DO.