A
Anonymous
Guest
Katika miezi ya hivi karibuni, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imekuwa ikituma bili za maji kwa wateja bila kuonesha idadi ya units zilizotumika kwa mwezi husika.
Hali hii inatia wasiwasi, hasa kutokana na changamoto za upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo, ambapo wakati mwingine tunalazimika kununua maji kwa madumu. Pamoja na changamoto hiyo, bili bado zinakuja zikiwa na kiasi kikubwa cha malipo bila kuonesha units zilizotumika.
Kwa sasa, bili hizo zinaonesha zaidi control number, jina la mteja na kiasi cha deni, jambo linalomfanya mteja kukosa uwazi wa kujua ametozwa kwa matumizi gani na kwa kiasi gani.
Tunaomba MWAUWASA kurekebisha hali hii na kuhakikisha bili za mwezi wa Agosti zinaonesha wazi idadi ya units zilizotumika kwa mwezi mzima. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uwazi, kuondoa malalamiko na kumwezesha mteja kuthibitisha usahihi wa bili anayodaiwa.