Kwanini Mwl Nyerere alipiga marufuku waTanzania kuangalia Tv?

Kwanini Mwl Nyerere alipiga marufuku waTanzania kuangalia Tv?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Hili ni swali mtu yeyote mwenye
Majibu achangie

Imagination zangu

Baada ya uhuru wa Tanzania watu wengi hawakuwa na elimu wala shughuli yeyote ya kiuchumi, ujinga na umasikini ulikuwa kwa asilimia 99%

Nyerere akaona kuwaruhusu watu hawa kuangalia Tv ni kulizika Taifa mchana kweupe

Akaamua kupiga marufuku watu kuangalia Tv

Je, kwa maoni yako kwanini Mwl Nyerere alipiga marufuku watu kuangalia Tv?
 
Hakutaka watu wajue yanayoendelea kwenye nchi zingine baada ya uhuru. Ingesababisha waasi kuwa wengi kwasababu wangejifunza mbinu mapema.

Watu wangeacha kazi zao na kuangalia tv hivyo uzalishaji kupungua

Hakutaka watu wajifunze tamaduni za west ambapo zingeharibu kabisa mila na desturi zetu (hili tunalishuhudia kwasasa)

Aliona tukiendekeza starehe sana (gari na tv) taifa litabweteka
 
Hili ni swali mtu yeyote mwenye
Majibu achangie

Imagination zangu

Baada ya uhuru wa Tanzania watu wengi hawakuwa na elimu wala shughuli yeyote ya kiuchumi, ujinga na umasikini ulikuwa kwa asilimia 99%

Nyerere akaona kuwaruhusu watu hawa kuangalia Tv ni kulizika Taifa mchana kweupe

Akaamua kupiga marufuku watu kuangalia Tv

Je kwa maoni yako kwanini Mwl Nyerere alipiga marufuku watu kuangalia Tv?
Alipiga Marufuku au TV zenyewe hazikuwepo?
 
Unaweza kutupa ushahidi wa bandiko la gazeti au barua au tangazo la katazo la watu kutokutazama tv?

Nikukumbushe tu miaka hiyo hakukuwa na vyombo vya habari kama sasa ila kuna watu walikuwa wanafunga madishi makubwa sana kuvuta mawimbi ya television,wengine walitumia antena. Ila ilikuwa ni nadra sana kukuta nyumba zina television.

Hakukuwa na katazo ila ni mawazo ya watu wa nyakati hizo kama hivi sasa baadae kuna watu watakuja kusema miaka ya 2025 serikali ilikataza watu kumiliki magari ya kimagharibi ya bei kali kama Ferrari, Bugatti, Aston Martin, etc kwasababu tu miaka yao hayakuwapo kwa wingi Tanzania na watu hawakuwa wakiyanunua.

Watu waongo waongo kila enzi huwa hawakosekani.
 
hilo jambo ni UZUSHI hakukuwa na jambo km hilo
miaka ambayo TV zinaingia NCHI ilikuwa imetoka kwenye VITA so ni miaka ambayo ambayo SERIKALI ilitaka vitu vingi vya anasa kudhibitiwa ambapo TV nadhani vilikiwa ni mojawapo

AFRKA mashariki yote NZANZIBAR ndio ilikuwa NCHI ya kwaza mwanzoni kabisa kuazisha TV STESHENI

je wangepatahe hizo taarifa Bila kuwepo TV STESHENI
bila shaka ilikiluwa ni gharama kubwa kupata STESHENI ukiwa na TV
ndio mana baada kuazishwa vituo binafsi vya tv basi TV zikaanza kuzagaa mwanzoni mwa miaka ya 90

Ni Uzushi tu kama ule wa miaka ya 90 ndege zikipita ANGANI zimefunga matangazo kwenye SHUKA linapepea watu wakawa wanasema inatangaza VITA ni mambo ambayo watu walikuwa wanajitungia then yanapitishwa kqenye VIJIWE vya kupiga soga
 
Tuwa tag jamii check? Jamii check
 
TV Zilizuiliwa wapi? Mimi nina watu wengi nawafahamu walikuwa na TV. Shida ilikuwa gharama ya kumiliki ni kubwa tena kipindi cha miaka ya 70 hadi 80 watu walikuwa wanatumia kwa ajili ya VHS tu, maana dish 📡 wakati ule peke yake ilikuwa kama 5M ya sasa na kuagiza nje njia ambayo ilikuwa mtu akisafiri ndio umuagize (kipindi kile dish za nyavu ndio ulikuwa unaweza kupata tv channel sio hizi kama za azam au dstv) kwa hiyo ndio maana hakukuwa na ma dish mengi na pia wakati ule antenna za kawaida kama sonnet ilikuwa useless maana ulikuwa haupati channel zozote.

Kuhusu JKN kuzuia kuangalia TV ni story za vijiweni maana waliojiweza waliitazama dunia vizuri tu.
 
Back
Top Bottom